Mbao Zinazosaidia Kukalisha Watu Wakiwa Wameamka
Na mleta habari za Amkeni! katika Sweden
KUCHAPISHWA kwa gazeti Amkeni! ambalo umeshika mkononi mwako hutegemea kwa sehemu kubwa utaratibu ambao huanzia msituni. Mashina ya mti hutoa mali ghafi ya karatasi. Hivyo ndivyo mambo huanza. Lakini acha sasa tuzuru kwa picha na kuona jinsi mti huwa gazeti kama Amkeni!
Chombo kilicho katika picha ya kwanza ni mashine ya ki-siku-hizi ya kuangushia miti, kikataji, ikifanya kazi. Si kwamba tu hiyo huangusha miti bali pia huondoa matawi. Zaidi ya hilo, hukata magogo kuwa urefu unaotakwa. Mbao hizo husafirishwa kwa lori au reli hadi kwenye kiwanda cha karatasi. Lori lililopakiwa kikamili huleta tani 20 kwa safari moja. Kwenye kiwanda cha karatasi ambacho Amkeni! lilizuru kwa ajili ya ripoti hii, mzigo mmoja wa mbao huwasili kila dakika 15 mchana kutwa. Fungu zima laweza kupakuliwa kwa upesi na mashine yenye vidole, kama inavyoonekana kwenye picha ya mwisho kwenye ukurasa 25.
Miti mingi kama hiyo huhitajiwa kwa ajili ya toleo moja tu la Amkeni! Kwa kuwa karatasi nyingi sana hutumiwa kila mwaka, miti mingi yapasa kukatwa. Hata hivyo, katika Sweden huo ni utaratibu unaoongozwa kwa uangalifu sana. Mamlaka huruhusu ukataji ikiwa tu maeneo yanayolingana yanapandwa tena, na kwa njia hiyo, misitu ya Sweden huendelezwa wakati wote.
Ramani kwenye ukurasa 25 yaonyesha utaratibu uliomo ndani ya mashine ya karatasi. Myeyusho humiminiwa kwenye mwisho mmoja, na karatasi hutokea mwisho ule mwingine. Lakini myeyusho huo hufanyizwaje?
Kwanza mbao hukatwa kuwa urefu unatakwa, na magamba huondolewa ndani ya mapipa makubwa. Kisha mbao hujitenganisha kwa kulingana na upana na urefu. Mbao zinazotimiza viwango fulani hufanywa kuwa myeyusho wa mbao zilizosagwa katika kisagio. Myeyusho huo ni mojawapo wa aina nne tofauti-tofauti ambazo hutumiwa katika kutengeneza karatasi kwenye kiwanda hiki. Mbao zinazosalia hukatwa-katwa vipande na kutumiwa kutengenezea myeyusho kwa kutumia moto na mashine na myeyusho wa salfa. Aina ya nne ya myeyusho hutokana na karatasi iliyoyeyushwa tena.
Myeyusho huo wa mbao zilizopondwa hutokezwa kwa kusaga mbao na pamoja na maji, chini ya msongo na zikiwa katikati ya mawe makubwa ya kusagia. Tokeo ni myeyusho uliofanyizwa kwa kutumia mashine.
Myeyusho wa kutumia moto na mashine hufanyizwa kwa kusafisha vipande vya mbao chini ya msongo mkubwa na joto ili kwamba nyuzi zitenganishwe. Hilo hutokeza nyuzi ndefu zaidi na zenye nguvu zaidi kuliko ule utaratibu wa kutumia mashine.
Myeyusho wa salfa hufanyizwa kwa kemikali. Hutayarishwa katika vyombo vikubwa vinavyoozesha vipande hivyo kwa kuvichemsha na magnesia bisalfa, kama vile katika sufuria ya msongo wa mvuke. Hilo hutokeza myeyusho wenye nguvu zaidi kushinda zile aina tatu za kwanza.
Aina ya nne, myeyusho wa karatasi iliyoyeyushwa tena, hutokezwa baada ya karatasi iliyokwisha tumiwa kuyeyushwa na kusafishwa wino na nta ya kale.
Mwishowe, kwenye kiviringio yale makunjo makubwa ya karatasi hukatwa kulingana na vipimo vya mnunuzi na kisha kupakiwa. Makunjo yaliyokamilishwa hutenganishwa kwa kulingana na mahali yanakoenda na kisha hupelekwa kwa mnunuzi kwa njia ya lori, reli, au mashua.
Sasa karatasi imefika kwenye matbaa kule Arboga. Kunjo hilo linatiwa ndani ya mashine inayokata karatasi kwa ukubwa unaotakwa kwa ajili ya matbaa mpya ya Sweden inayochapa kwenye karatasi zilizo mfano wa kurasa kwa rangi kamili. Matbaa mpya hiyo yaweza kufanya mizunguko ya kuchapa 15,000 kwa saa moja.
Kila toleo hupelekewa waandikishaji katika Sweden na ng’ambo. Kuongezea hilo, mabunda ya nakala za kutawanywa kwa umma hupelekewa mamia ya makundi ya Mashahidi wa Yehova kotekote nchini. Maelfu ya nakala kutokana na mabunda hayo huachwa na Mashahidi watembeleapo nyumba za watu au kuwakuta penginepo.
Ndiyo, lile shina la mti katika msitu limefika kwenye kao lalo la mwisho—gazeti Amkeni! Tafadhali, angalia kwamba Amkeni! hutia ndani makala zinazotoa habari na kuamsha wasomaji kuhusu maana ya matukio ya ulimwengu kulingana na nuru ya unabii wa Biblia. Hivyo husaidia wasomaji wajifunze juu ya Muumba wa binadamu na kusudi Lake kwa siku yetu. Maarifa hayo yatakusaidia uelewe maana ya yale yanayotukia katika wakati wetu na pia yatakusaidia ujenge tumaini imara la wakati ujao ulio bora zaidi.
[Sanduku[Mchoro katika ukurasa wa 17]
Mashine ya Karatasi
A. Myeyusho unaofikia mashine ya karatasi wafanana na uji mzito na husambazwa katika kiambaza chenye upana wa meta kadhaa juu ya mshipi unaozunguka wenye kichungi cha waya. Kufikia hatua hii myeyusho huwa ni maji karibu asilimia 99. Maji hayo yaliyo mengi yataondolewa wakati wa safari ya kuipitia mashine hiyo, ambayo ni ya karibu meta 8.6 kwa urefu.
B. Kiasi cha maji hupunguzwa kufikia karibu asilimia 60 katika eneo la msongo. Maji husongwa yakaondolewa na mashine, mara nyingi kwa kushirikiana na mfyonzo.
C. Katika eneo la kukaushia, utando wa karatasi hukaushwa juu ya mabamba-mviringo yenye kupashwa joto na mvuke.
D. Kupiga sulu hufanya karatasi kuwa laini zaidi, na hilo hufanywa kwa kuruhusu karatasi ipite baina ya vizungushio. Ni asilimia 5 pekee ya maji inayobaki karatasi inapoviringwa hatimaye kuwa makunjo.
[Mchoro] (Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Kisanduku kikuu Sehemu ya waya Eneo la msongo Eneo la kukaushia Kulainisha
Ncha yenye majimaji Kuviringa
[Picha katika ukurasa wa 18]
Tawi kule Arboga, Sweden
Makunjo ya karatasi yakipangwa