Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 8/8 uku. 3
  • Je! Kuna Mtu Yeyote Huko Nje?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Kuna Mtu Yeyote Huko Nje?
  • Amkeni!—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Kuchunguza Sauti za Angani Huko Australia
    Amkeni!—2003
  • Wakaaji wa Nje ya Dunia Hii—Kupata Jibu
    Amkeni!—1990
  • Wakaaji wa Nje ya Dunia Hii—Wako Wapi?
    Amkeni!—1990
  • Wajumbe Sita Kutoka Anga la Nje
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 8/8 uku. 3

Je! Kuna Mtu Yeyote Huko Nje?

KUNA mwanamume fulani katika Massachusetts, U.S.A., ambaye kama sehemu ya kazi yake kila siku huchunguza aone kama jumbe zozote zimeingia. Siku baada ya siku, hakuna zozote huingia. Kwa miaka kadhaa sasa, hakuna zozote zimeingia. Lakini bado yeye huchunguza kwa ukawaida, naye hukatishwa tamaa kwa ukawaida. Je! kwani yeye si mtu maarufu? Je! mashine yake ya kutolea jibu imevunjika?

Si lolote la hayo. Yeye huchunguza mashine fulani, lakini haikuunganishwa na kamba ya simu. Ni kompyuta iliyounganishwa na sikio kubwa la kielektroni ambalo limeelekezwa juu, mbali na ulimwengu wetu, ndani ya vina vya anga ya juu: darubini ya redio. Mwanamume huyu anasaidia kikoa cha wanasayansi kupekua nyota ili kupata ujumbe kutoka kwa wakaaji wa nje ya dunia hii wenye akili, wahai walio ng’ambo ya ulimwengu wetu.

Wengine, kama yeye, wamekuwa pia wakisikiliza kwa miaka 30 sasa. Katika 1960 mwanaanga Frank Drake akawa ndiye binadamu wa kwanza kusikiliza ishara za kama kuna wakaaji wa nje ya dunia hii wenye akili. Tangu wakati huo, kwa kweli mwanadamu ni kama ameweka masikio yake angani. Visa vipatavyo 50 vya utafutaji mrefu vimefanyika angani kufikia sasa.

Darubini za redio kokote ulimwenguni zimejiunga katika utafutaji huo—katika Ufaransa, Jamhuri ya Muungano ya Ujeremani, Uholanzi, Australia, Urusi, Argentina, United States, na Kanada. Kama vile mtu mmoja alivyoweka wazo hilo: “SETI [ambacho ni kifupi cha Kiingereza cha kusema “Kutafuta Wakaaji wa Nje ya Dunia Hii”] yaendelea kuwa shughuli ya kimataifa kama anga yenyewe.” Kikoa kimoja chenye kuzungumzia habari hiyo kilileta wanasayansi kama 150 kutoka nchi 18 zenye kuhusisha kontinenti zote tano.

Ingawa hivyo, mradi wa SETI wa kutafuta makuu mengi zaidi utafyatushwa katika 1992. NASA, shirika la Usimamizi wa United States wa Usafiri wa Kitaifa Angani, lapanga kutumia chombo kipya chenye nguvu ambacho kitafanya iwezekane kuangalia-angalia mawimbi yenye kuletwa na redio wakati ule ule mmoja. Utafutaji huo umekusudiwa kuendelea kwa miaka kumi kwa gharama ya dola milioni 90. Utachukua muda mrefu kama mara milioni elfu kumi kuliko utafutaji wote uliotangulia ukijumlishwa pamoja.

Lakini binadamu aulizapo hivi juu ya ulimwengu wote mzima ulio mkubwa sana, “Je! kuna mtu yeyote huko nje?” atahitaji vifaa thabiti vya tekinolojia ya juu ndiyo apate jibu. Kwa njia nyingi hilo ni swali la kiroho. Kwa kupapasa-papasa akitafuta jibu, mwanadamu afunua wazi baadhi ya matumaini yake ayathaminiyo sana: mwisho wa vita, mwisho wa magonjwa, labda hata kufikia kutokufa kwenyewe. Kwa hiyo thawabu zinazotafutwa ni nyingi. Baada ya karne nyingi za kujiuliza-uliza na miongo mingi ya kutafuta-tafuta, binadamu amekaribia jibu kwa kadiri gani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki