Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 4/8 uku. 17
  • “Mti Uliosimama kwa Kichwa”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Mti Uliosimama kwa Kichwa”
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • “Mti wa Uhai” Wenye Kushangaza wa Afrika
    Amkeni!—1995
  • Je, Kweli Huu ni Mti?
    Amkeni!—2008
  • Kilimanjaro—Kilele cha Afrika
    Amkeni!—1997
Amkeni!—1991
g91 4/8 uku. 17

“Mti Uliosimama kwa Kichwa”

HILO ndilo jina la utani la mbuyu wa Afrika. Unapofunikwa na majani na maua, mbuyu unavutia macho. Lakini katika kipupwe yale matawi mafupi matupu hutokeza kwenye shina nene na huonekana kama mizizi ya mti uliosimama kwa kichwa.

Kikundi kimoja cha mibuyu katika Botswana ya kaskazini chaitwa wale Dada Saba. Vilichorwa kwa rangi na msafiri-mchoraji Thomas Baines katika karne ya 19. Kama mtu akilinganisha uchoraji wa rangi wa Baine wa zaidi ya karne moja iliyopita na miti hiyo leo, ni tofauti chache sana zinazoonekana.

Hilo laonyesha kudumu na maisha marefu ya mbuyu. Hukadiriwa kwamba miti iliyo mikubwa zaidi ina maelfu ya miaka. Mbuyu husitawi katika majimbo yenye joto, yaliyo makavu ya Afrika na una mafaa mengi yenye kuendeleza uhai. Mabuyu yana mbegu nyeupe kama chokaa zenye ladha kama mtindi wa sukari guru. Ndovu hufurahia kula ganda na miti myororo, yenye umaji-maji mwingi. Kwa kweli, akiba za maji ya mvua hupatikana nyakati nyingine kwenye makutano yenye shimo ya matawi na mibonyeo iliyofanyizwa ndani ya mti huo.

Sehemu nyingine yenye kutokeza ya mbuyu ni uvimbe wao ulio mnene sana. Ulio mkubwa kati ya majitu hayo makubwa yaripotiwa uko kwenye mitelemko ya kaskazini ya Mlima Kilimanjaro katika Tanzania; una mviringo wa meta 28. Mbuyu mmoja wenye mbonyeo katika Zimbabwe ulitumiwa kuwa kituo chenye kifuniko cha wakati wa kusubiri basi na ungeweza kufunika watu zaidi ya 30.

Laonekana kuwa jambo la kushangaza kwamba binadamu mwenye akili afe baada ya miaka yake sabini na hali “mti uliosimama kwa kichwa” waweza kuishi kwa maelfu ya miaka. Kwa uzuri, tuna kila uhakikisho kwamba Muumba wa vitu vyote vilivyo hai atatimiza kwa ukamili ahadi yake kwamba siku za watu wake zitakuwa “kama siku za mti.”—Isaya 65:22; Zaburi 90:10.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki