Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 7/8 kur. 12-13
  • Kutia Damu Mishipani— Je! Ndio Ufunguo wa Kuokoa Uhai?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutia Damu Mishipani— Je! Ndio Ufunguo wa Kuokoa Uhai?
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Njia Nyingi za Badala
  • Maswali ya Funzo la Kijitabu Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
    Huduma Yetu ya Ufalme—1988
  • Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
    Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
  • Kuokoa Uhai kwa Damu—Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Matibabu Mengine Bora Badala ya Damu
    Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 7/8 kur. 12-13

Kutia Damu Mishipani— Je! Ndio Ufunguo wa Kuokoa Uhai?

KATIKA 1941 Dkt. John S. Lundy aliweka kiwango cha kutia damu mishipani. Yaonekana bila ushuhuda wowote wa uchunguzi wa kikliniki, yeye alisema kwamba ikiwa hemoglobini ya mgonjwa, kile kisehemu cha damu chenye kubeba oksijeni, chashuka kufikia gramu kumi au chini zaidi kwa kila desilita ya damu, basi mgonjwa ahitaji kutiwa damu mishipani. Baadaye hesabu hiyo ikawa kiwango kwa madaktari.

Kiwango hiki cha gramu kumi kimefanyiwa ubishi kwa karibu miaka 30. Katika 1988 The Journal of the American Medical Association lilisema wazi kabisa kwamba ushuhuda huo hauungi mkono mwongozo huo. Tabibu wa dawa nusukaputi Howard L. Zauder asema ‘umefichika katika mapokeo, umefunikwa katika kutoeleweka vizuri, na hauhakikishwi na ushuhuda wa kikliniki wala wa majaribio.” Wengine huuita ubuni tu.

Ufichuzi wote huu ujapofanywa kwa bidii, bado ubuni huu waheshimiwa sana kuwa mwongozo timamu. Kwa matabibu wengi wa dawa nusukaputi, kiasi cha hemoglobini cha chini ya kumi huwachochea kutia damu mishipani ili kurekebisha ukosefu wa damu mwilini. Huwa ni kama jambo la kufanywa moja kwa moja.

Bila shaka, hiyo yasaidia kueleza sababu ya utumizi mwingi mno leo wa damu na vitu vilivyofanyizwa kwa damu. Dkt. Theresa L. Crenshaw, aliyetumikia katika Tume ya Kirais Kuhusu Mtokeo Mkubwa wa Vairasi kwa Kukosa Kinga Mwilini, akadiria kwamba katika United States pekee, visa kama milioni mbili vya kutia damu mishipani bila uhitaji hufanywa kila mwaka na kwamba karibu nusu ya visa vyote vya kutia mishipani damu iliyowekwa akibani vingeweza kuepukwa. Wizara ya Afya na Masilahi ya Japani walilaumu “utumizi wa kutia-tia damu mishipani bila uangalifu” katika Japani, na pia ile “imani ya kiupofu kwamba kufanya hivyo huponya.”

Tatizo la kujaribu kurekebisha ukosefu wa damu mwilini kwa kutia damu mishipani ni kwamba kule kutia damu kwaweza kuwa hatari kuliko upungufu wa damu mwilini. Mashahidi wa Yehova, ambao hukataa kutiwa damu mishipani hasa kwa sababu za kidini, wamesaidia kuthibitisha jambo hilo.

Huenda ikawa wewe umeona vichwa vikuu vya magazeti vikiripoti kwamba mmoja wa Mashahidi wa Yehova alikufa kwa sababu ya kukataa kutiwa damu mishipani. Kwa kuhuzunisha, ni mara chache ambapo ripoti hizo hueleza hadithi nzima. Mara nyingi, katao la daktari kupasua, au kupasua upesi vya kutosha, ndilo humletea Shahidi kifo. Wapasuaji fulani hukataa kupasua bila uhuru wa kutia damu mishipani ikiwa kiasi cha hemoglobini kimeshuka chini ya kumi. Hata hivyo, wapasuaji wengi wamefanikiwa kupasua Mashahidi huku kiasi cha hemoglobini kikiwa tano, mbili, na hata chini zaidi. Asema hivi mpasuaji Richard K. Spence: “Jambo ambalo nimekuta kwa Mashahidi ni kwamba kule kuwa na kiasi cha chini zaidi cha hemoglobini hakuhusiani na kufa hata kidogo.”

Njia Nyingi za Badala

‘Damu au kifo.’ Hivyo ndivyo madaktari fulani hueleza njia badala zinazokabili mgonjwa Shahidi. Hata hivyo, kwa uhalisi, kuna njia nyingi za badala za kutotiwa damu mishipani. Mashahidi wa Yehova hawapendezwi na kufa. Wao hupendezwa na matibabu ya badala. Kwa sababu Biblia hukataza kuingiza damu mwilini, wao hawaoni kamwe kutia damu mishipani kuwa ni njia badala.

Katika Juni 1988, Report of the Presidential Commission on the Human Immunodeficiency Virus Epidemic ilidokeza kwamba wagonjwa wote wapewe kitu kile kile ambacho Mashahidi wamekuwa wakiomba kwa muda wa miaka, yaani: “Idhini ya mgonjwa kutiwa damu mishipani au sehemu zayo yapasa kuhusisha maelezo ya kumpasha habari juu ya hatari zilizomo . . . na habari juu ya njia zifaazo badala ya utibabu wa mtu kutiwa mishipani damu ya mwingine yenye kufanana na yake.”

Ndiyo kusema, wagonjwa wapasa kupewa chaguo. Chaguo moja la jinsi hiyo ni namna fulani ya kutia mishipani damu ya mtu mwenyewe. Damu ya mgonjwa mwenyewe huhifadhiwa wakati wa upasuaji na kuzungushwa tena katika mishipa ya mgonjwa. Iwapo utaratibu huo ni mwenezo tu wa mfumo wa mzunguko-damu wa mgonjwa mwenyewe, unakubalika sana kwa Mashahidi walio wengi. Wapasuaji hukazia pia thamani ya kuongeza mweneo wa damu ya mgonjwa kwa vipanuaji visivyo na damu na kuacha mwili ujijaze tena chembe nyekundu zao wenyewe. Mbinu hizo zimetumiwa mahali pa kutia damu mishipani bila kuongezea idadi ya vifo. Kwa uhakika, zaweza kuleta maendeleo ya usalama.

Dawa yenye matumaini mema iitwayo kifanyiza-chembe-nyekundu imekubaliwa hivi majuzi kwa utumizi wenye mipaka. Hiyo huharakisha ufanyizaji wa mwili wenyewe wa chembe nyekundu za damu, kwa njia hiyo zikisaidia mtu kufanyiza kiasi kingi zaidi cha damu yake mwenyewe.

Wanasayansi wangali wanatafuta kitu chenye matokeo badala ya damu chenye kuiga uwezo wayo wa kusafirisha oksijeni. Katika United States, wenye kufanyiza vibadala hivyo waona ni vigumu kupata kibali kwa ajili ya vifanyizo vyao. Hata hivyo, kama alivyokataa mfanyizi mmoja wa jinsi hiyo: “Kama ungefikiria kuleta damu kwenye FDA [Usimamizi wa Chakula na Dawa] ili ikubaliwe, hungelazimika kuomba sana kwamba ichunguzwe kwa kuwa ina sumu sana.” Hata hivyo, kuna matumaini mengi kwamba kemikali yenye matokeo itapatikana ambayo itakubaliwa kuwa kitu chenye kusafirisha oksijeni badala ya damu.

Hivyo basi kuna njia nyinginezo za kutumiwa badala. Zile zilizotajwa hapa ni chache tu za zile zipatikanazo. Kama vile Dkt. Horace Herbsman, profesa wa upasuaji wa kikliniki, alivyoandika katika jarida Emergency Medicine: “Ni . . . wazi sana kwamba tuna njia za kutumiwa badala ya kujazia damu. Kwa kweli, labda maono yetu kuhusiana na Mashahidi wa Yehova yangeweza kufasiriwa kuwa yamaanisha kwamba hatuhitaji kutegemea kutia damu mishipani, ambako ni kwenye matatanisho mengi, kama tulivyofikiri hapo kwanza.” Bila shaka, kwa kweli hakuna lolote la hayo lililo jipya.” Kama lilivyosema The American Surgeon: “Uhakika wa kwamba mipasuo mikubwa yaweza kufanywa kwa usalama bila kutia damu mishipani umethibitishwa vya kutosha katika miaka 25 iliyopita.”

Lakini ikiwa damu ni hatari, na kuna njia zilizo salama badala ya kuitumia, mbona basi mamilioni ya watu hutiwa damu mishipani isivyo lazima—wengi wao bila kujua hivyo, kwa kweli wengine wakifanyiwa hivyo dhidi ya mapenzi yao? Ripoti ya tume ya kirais juu ya UKIMWI yataja kwa sehemu kushindwa kuelimisha madaktari na hospitali juu ya hizo njia badala. Yalaumu kisababishi kingine pia: “Vitovu fulani vya kijimbo vya damu vimekuwa vikisita kuendeleza mbinu zipunguzazo utumizi wa matibabu ya kutia mishipani, kwa kuwa mapato yavyo ya kuendeshea shughuli hupatikana kutokana na mauzo ya damu na vitu vilivyofanyizwa kwa damu.”

Ndiyo kusema: Kuuza damu ni biashara kubwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki