Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 8/8 uku. 3
  • Wewe Wawaonaje Watu wa Jamii ya Rangi Nyingine?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wewe Wawaonaje Watu wa Jamii ya Rangi Nyingine?
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Jamii ni Suala Kubwa Hivyo?
    Amkeni!—1993
  • Jamii Ni Nini?
    Amkeni!—1993
  • Tatizo Laenea
    Amkeni!—1998
  • Unaweza Kuvumilia Hadi Mwisho
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 8/8 uku. 3

Wewe Wawaonaje Watu wa Jamii ya Rangi Nyingine?

“Vichwa-upara Waamerika, walio kama vichwa-upara makakawana katika Ulaya, ni vijana waajiriwa wa jamii ya Kiarya.

Sisi tunapinga mabepari na wakomunisti ovyo wanaoiangamiza jamii yetu ya Kiarya. . . . Jamii ya wanyonyaji Wayahudi ndiyo tatizo letu kubwa.”

MANENO haya ni ya kikaratasi cha kutoka kwa genge la vijana vichwa-upara walio na makao yao katika Chicago. Wao ni vijana ambao hunyoa vichwa vyao, huvaa mavazi ya kipekee yaliyopambwa misalaba ya swastika, hutukuza jeuri, husikiza muziki unaotukuza “nguvu za weupe,” na kudharau Wayahudi, weusi, na vikundi vingine vya wachache.

Kiongozi mmoja wa genge liitwalo “Jeuri ya Msisimuko” aliambia kusanyiko la viongozi wenye kupendelea weupe kwamba kikundi chake “chawakilisha vita,” na akaongeza: “Mimi ni mtu mwenye jeuri. Naipenda jamii ya watu weupe, na ukipenda kitu unakuwa mtu mbaya sana duniani.”

Kama ilivyo kawaida ya harakati, vichwa-upara ni wachache. Maoni yao ni ya kupita kiasi. Ni watu wachache sana leo wanaoweza kujionyesha wazi kuwa shupavu na wagomvi. Lakini wengi wanaendeleza chuki kwa watu wa rangi nyingine kisiri na kutowaamini. Ulimwenguni kote watu huhukumiwa kulingana na hali ya macho na rangi ya ngozi yao. Je, kuna tofauti za kiakili na tabia za kihisia kati ya jamii za rangi mbalimbali? Ili kujibu maswali haya, kwanza na tuchunguze jinsi maoni mbalimbali juu ya rangi za kijamii yamesitawi kwa karne nyingi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki