Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 9/8 kur. 10-11
  • Namna Gani Wakati Ujao?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Namna Gani Wakati Ujao?
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kusudi la Kwanza Litatimizwa
  • Ishi Milele Juu ya Dunia-paradiso
    Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai?
  • Furahia Wanyama Milele
    Amkeni!—2004
  • Ahadi Iliyo Hakika ya Taratibu Mpya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Siku za Ushetani Zimehesabiwa
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 9/8 kur. 10-11

Namna Gani Wakati Ujao?

Kwa nini amani kati ya binadamu na mnyama ni yenye kuvutia sana? Ni kwa sababu binadamu waliumbwa pale mwanzoni wawe na amani na wanyama, hata wale wanaojumuishwa kuwa wakali.

Mungu alipoumba mwanamume na mwanamke wa kwanza, aliwaweka katika eneo la paradiso duniani ili waone shangwe ya maisha. Lilikuwa kusudi lake wapate watoto na kuendeleza mipaka ya Paradiso hiyo ya kwanza mpaka ifunike dunia nzima. Katika milki nzima hiyo, ainabinadamu ilipaswa kuwatiisha wanyama kwa amani.

Kitabu cha Mwanzo kinasimulia hivi: “Wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. . . . Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.—Mwanzo 1:26-31; 2:9.

Utiisho huu wa wanyama haukupasa kuwa wa ukatili. Wanadamu na wanyama walipaswa kuishi pamoja kwa amani. Hilo laweza kuonekana na uhakika wa kwamba wakati wanyama hao walipopita mbele za mwanadamu ili wapewe majina, yeye hakuwa na silaha. Na hakukuwa mtajo wa woga ulioonyeshwa na ama mwanadamu ama na mnyama.—Mwanzo 2:19, 20.

Kusudi la Kwanza Litatimizwa

Kwa kufurahisha, kusudi hilo la kwanza la Mungu litatekelezwa karibuni, wakati nafasi ya serikali zote za kibinadamu itakapokuwa imechukuliwa na Ufalme wa Mungu, unaotawala kutoka mbinguni. (Danieli 2:44; Mathayo 6:9, 10) Utawala wa Mungu ukiwa umeimarishwa kabisa juu ya dunia nzima, kusudi la kwanza la Mungu kwa dunia na wakaaji wayo wanadamu na wanyama litasonga mbele likatimizwe.

Matokeo ya mabadilisho ya utawala wa Mungu wenye uadilifu yanaelezwa vizuri katika unabii mwingi wa Biblia. Kwa mfano, ona kile Isaya alitabiri chini ya uvuvio wa roho: “Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua BWANA [Yehova, NW], kama vile maji yanavyoifunika bahari.”—Isaya 11:6, 7, 9.

Unabii mwingine pia waonyesha amani nyingi ambayo itapatikana katika ulimwengu mpya wa Mungu. Kuhusu jambo hilo Mika alitabiri: “Nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu.”—Miaka 4:3, 4.

Hakuna wowote wa wanyama wa mwitu atakayevuruga amani ya ainabinadamu, kwa kuwa neno la kiunabii la Mungu lasema: “Nitafanya agano la amani nao, nami nitawakomesha wanyama wakali kati yao; nao watakaa salama jangwani, na kulala misituni. . . . Nao watakuwa salama katika nchi yao.”—Ezekieli 34:25, 27.

Kwa hiyo amani na mapatano yatakayokuwa katika Paradiso hiyo iliyorudishwa yatakuwa kamili. Ndiyo maana hali huko zaweza kuelezwa kuwa hivi katika kitabu cha mwisho cha Biblia: “Naye [Mungu] atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.”—Ufunuo 21:4, 5.

Ndiyo, amini na kweli. Hii yamaanisha kwamba tunaweza kutegemea ahadi za Mungu, kwa sababu tofauti na wanadamu wasiokamilika, yeye ana uwezo, hekima, na nia thabiti ya kutekeleza makusudi yake. Kama vile mmoja wa watumishi waaminifu wa Mungu alivyosema nyakati za kale: “Halikuwapungukia ninyi hata neno moja katika mambo hayo mema yote aliyoyanena BWANA [Yehova, NW] Mungu wenu, katika habari zenu; yote yametimia kwenu, hapana neno lolote mlilopungukiwa.”—Yoshua 23:14; ona pia Isaya 55:11.

Tunaweza kuwa na uhakika huo huo kwamba karibuni, katika ulimwengu mpya wa Mungu, kusudi lake la kwanza kwa dunia hii, kwa wanadamu, na kwa wanyama litatimizwa. Amani itokayo kwa Mungu itakuwa halisi ulimwenguni pote. Na amani hiyo haitatawala kati ya wanadamu pekee bali pia itaonyeshwa katika enzi ya wanyama.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki