Kutoka kwa Wasomaji Wetu
Upofu wa Kutopambanua Rangi Mume wangu amefanyiwa upasuaji wa jicho na kwa sasa hawezi kusoma. Tulipopata tu makala juu ya upofu wa kutopambanua rangi katika toleo Agosti 8, 1991, aliniambia nimsomee. Akiwa mtoto, hangeweza kutofautisha picha katika TV ya rangi nyeusi-na-nyeupe kutoka kwa ile ya rangi kamili, na hakuna yeyote katika jamaa yao alijali hilo. Wakati tu alipofanya mtihani wake wa leseni ya udereva ndipo aligundua kwamba yeye alikuwa kipofu wa kutopambanua rangi. Hivyo mume wangu anatoa shukrani zake kwa makala yenu. Kama lingekuwako mapema, angaliepuka hali nyingi zisizofaa!
M. D., Italy
Ushirikiano Kati ya Daktari na Mgojwa Asanteni kwa makala “Kuziba Pengo Kati ya Daktari na Wagonjwa Mashahidi.” (Septemba 8, 1991) Nina mvulana mdogo ambaye alizaliwa na haidrosefalas na spina bifida. Alifanyiwa upasuaji mara nne kabla ya kuwa na mwaka mmoja. Ingawa hali yake imeendelea kuwa nzuri, bado anahitaji uangalizi wa kitiba. Kwa sababu ya msimamo wetu wa damu [tukiwa Mashahidi wa Yehova], nawa bila uhakika kama madaktari watashirikiana nasi. Twatumaini kwamba mpango wa kuwa na ndugu Wakristo waliozoezwa kutusaidia kushughulika na madaktari utafika upesi hapa Argentina
A. M., Argentina
Halmashauri za Kupatanisha na Hospitali zinasitawishwa katika Argentina—MHARIRI.
Ulaya ya Mashariki Tangu mabadiliko ya karibuni ya Ulaya ya Mashariki yalipoanza, nimekuwa na hamu ya kujua juu ya Mashahidi wa Yehova wanaoishi katika sehemu hiyo ya dunia. Habari chache zingepatikana katika vichapo vyetu. Mnaweza kuwazia uradhi wangu wakati nilipopata toleo la Januari 8, 1991 Kiingereza, makala “Mashahidi wa Yehova katika Ulaya ya Mashariki.” Natumaini mtaendelea kutujulisha kuhusu maendeleo ya kazi ya kuhubiri katika sehemu hiyo ya dunia.
E. S. L., Brazili
Dawa za Kulevya Niliposoma makala “Dawa za Kulevya? Salimiana kwa Mkono na Shetani! (Novemba 8, 1990, Kiingereza), nilisukumwa kutoa machozi. Ripoti hiyo ilikuwa yenye kuhuzunisha lakini, kwa wakati uleule, yenye kutia nguvu. Makala hiyo iliweka wazi kwamba hakuna faida yoyote kumbadilisha Yehova na chochote ambacho ulimwengu huu unaweza kutoa.
M.C.P., Brazili
Usumbuo Shuleni Makala “Vijana Wanauliza . . . “Naweza kumfanyaje Ili Aniache?” (Mei 22, 1991 Kiingereza) lilikuwa na habari nzuri ajabu. Nilipokuwa shuleni, wanadarasa wenzi walikuwa wananishawishi kila mara tuwe marafiki. Walipoona kwamba sikukubaliana nao, wakaacha kunichokoza. Hivi sasa siko shuleni na ninafanya kazi. Yapata mwezi mmoja uliopita, mtu mkubwa kwa umri (miaka 37) alinijia kazini na kuniambia nilikuwa mrembo na alitaka kunijua mimi. Nina umri wa miaka 18. Nilishindwa kuzungumza kwa muda. Lakini nilimwambia nilikuwa ninajifunza niwe mmoja wa Mashahidi wa Yehova na nikamwangushia vichapo. Pia alikubali upingaji wangu kwa aliyotaka.
M. L., United States
Kufua Nguo Ninawaandikia kuonyesha uthamini wangu kwa makala “Hivi Ndivyo Tunavyofua Nguo Zetu . . . ” (Desemba 8, 1991) Nikiwa painia wa pekee [mhubiri wa wakati wote] anayetumikia katika sehemu za mashambani, inanilazimu kufua nguo zangu kwa mikono. Baada ya kusoma makala yenu, sioni sababu yoyote ya kuwaonea wivu wenye kutumia mashine za kufulia nguo.
M. M., Jamhuri ya Dominican