Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 5/8 kur. 12-13
  • Kujikinga—Mkristo Aweza Kufikia Hatua Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kujikinga—Mkristo Aweza Kufikia Hatua Gani?
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jeuri kwa Jeuri?
  • Wakati wa Kupigana?
  • Je, Ni Sawa Kutumia Nguvu Ili Kujilinda?
    Amkeni!—2008
  • ‘Tafuteni Amani na Mwifuate Sana’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Je, Nijifunze Mbinu za Kujikinga?
    Amkeni!—1995
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 5/8 kur. 12-13

Maoni ya Biblia

Kujikinga—Mkristo Aweza Kufikia Hatua Gani?

“Kwa nini uishi kwa woga? Jifunze njia za kujikinga mwenyewe na kumhepa mshambulizi. Njia zilizo rahisi na ustadi zimeelezwa kwa undani. Video hii yenye mafundisho ingeweza kufanyiza tofauti kati ya kuwa mfu au mwokokakaji.”—Tangazo la video ya kujikinga.

HAKUNA yeyote anayehitaji kuelezea uuzaji mkubwa wa video kama hiyo leo. Katika jiji la Philadelphia, Pennsylvania, U. S. A., vikundi vya vijana huimba “kimbia, kimbia, kimbia” wakizunguka-zunguka mitaani wakitafuta watu wa kuwanyang’anya. “Woga wa uhalifu unakumba jiji lote” la Rio de Janeiro, likaripoti gazeti Time. Katika Hong Kong wanyang’anyi na wauaji wenye silaha wanapatikana katika maeneo ambayo jeuri ya uhalifu umekuwa haujulikani—hadi sasa.

Ripoti kama hizo zasikika ulimwenguni pote. Kwa matokeo gani? “Wananchi hufikiria hatari za kulipiza ufyatuaji risasi,” lasema Newsweek. Wakristo hawakingwi na hizi siku “zenye hatari,” lakini je! kulipiza ufyatuaji risasi kutafanyiza “tofauti kati ya kuwa mfu au mwokokaji”?—2 Timotheo 3:1.

Jeuri kwa Jeuri?

Watu fulani huamini kwamba, ‘Nikibeba bunduki nitakuwa salama. Nitampata yeye kabla hajanipata mimi. Angalau nitamwogopesha!’ Hata hivyo, si rahisi hivyo.

George Napper, wakili wa usalama wa Atlanta, Georgia, U. S. A., anasema: “Kuwa na bunduki mkononi kwamaanisha kuwa tayari kuishi pamoja na matokeo ya kuua binadamu mwingine.” Je! Mkristo atakuwa tayari kuishi na sifa kama hiyo, ambayo huenda hata ikatia ndani umwagaji damu?—Linganisha Hesabu 35:11, 12.

Pia, Neno la Mungu huamuru, ‘Fueni panga zenu ziwe majembe’ na, ‘Tafuta amani na uifuate sana.’ (Mika 4:3; 1 Petro 3:11) Wakristo wanawezaje kutafuta ulinzi wakiwa na silaha na wakati uleule waishi kwa kupatana na matakwa ya Mungu? Katika hali yoyote ile, itakuwa rahisi kwa mshambulizi kushambulia kimbele kuliko mshambuliwa.

Yesu alikataa ukinzani wa silaha. Ni kweli, aliwaambia wanafunzi wake wabebe panga mbili kwenye shamba la Gethsemane, mahali ambapo angeshikiwa. Lakini kwa nini alifanya hivi? Kuwa na silaha, na hata hivyo kutozitumia, kulionyesha kwamba wafuasi wa Yesu hawangepaswa kutumia silaha. Ni wazi kwamba kwa kuwa na silaha, Petro aliitumia bila kufikiri. Yesu alimkemea sana kwa tendo hili la harara kwa maneno haya: “Wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga.”—Mathayo 26:36, 47-56; Luka 22:36-38, 49-51.

‘Hiyo ni kweli kabisa kuhusu kuwa na silaha zenye risasi,’ huenda mtu fulani akasema. ‘Lakini vipi juu ya kujifunza stadi fulani za kujikinga, kama vile judo, karate, na kendo?’ Jiulize mwenyewe, je! lengo la maagizo hayo si kupiga na kuumiza wengine? Na je! zoezi hilo si sawa na kujiandaa na silaha zinazoweza kuua? (1 Timotheo 3:3) Hata vipindi vya mazoezi vimetokeza maumizo mabaya na mapigo yenye kuua.

Warumi 12:17-19 hutoa ushauri wenye hekima kuhusu hili: “Msimlipe mtu ovu kwa ovu . . . Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana [Yehova, NW].” Neno la Kigiriki analotumia Paulo kwa “ovu” (ka·kosʹ) laweza kumaanisha pia “uangamivu, uharibifu.” Hivyo, Wakristo wanapaswa kujiepusha na aina zote za kuangamiza au kuumiza mtu mwingine kwa kulipa kisasi.

Badala ya kuonyesha hasira yake mwenyewe bila kufikiri, Mkristo humtumaini Mungu kabisa, ambaye husema juu ya watu wake: “Yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho [langu].” Kupatana na hili, Mungu aahidi ‘kuwaangamiza waovu’ kwa wakati wake.—Zekaria 2:8, UV; Zaburi 145:20, NW.

Wakati wa Kupigana?

‘Sitawacha pesa zangu ziende bila kupigana!’ wengine huthubutu kusema. Dick Mellard, msimamizi wa Taasisi ya Kitaifa ya Kuzuia Uhalifu, atahadharisha: “Ni asili ya kibinadamu kukinza, lakini asili ya kibinadamu yaweza kukufanya uuawe katika hali mbaya.” Wanyang’anyi wengi wana silaha hatari na ni wenye hangaiko na wasiwasi. Pesa zilizopotea zaweza kupatikana tena, lakini vipi juu ya uhai uliopotezwa? Je! kujasiria kunastahili kweli?

George Napper anatoa shauri hili: “Labda njia bora zaidi ya kujilinda ni kujasiria kupoteza mali yako badala ya uhai wako. Lengo la wanyang’anyi wengi na wavamizi ni kuiba, si kuua.” Katika hali ambapo mtu ameendewa au pesa zake zinaitishwa, kanuni ya maana ni: “Haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi.”—2 Timotheo 2:24.a

Hiyo si sera ya kutokinza kabisa katika hali yoyote. Katika Kutoka 22:2, 3, kuna maelezo ya hali ambayo mwizi anapigwa na kufa anapoingia katika nyumba ya mtu wakati wa mchana. Aina hiyo ya kujikinga ilionekana sawa na kuua kimakusudi, kwa kuwa mwizi angetambuliwa na kuletwa kwenye hukumu. Lakini wakati wa usiku, ingekuwa vigumu kwa mwenye nyumba kumwona mdukizi na kujua makusudio yake. Kwa hivyo, mtu aliyeua mdukizi katika giza alionwa kuwa asiye na hatia.

Hivyo, Biblia haizuii mwelekeo wa haraka wa kujikinga. Hata hivyo, kwa kutokuunga mkono sera ya kutokinza hata kidogo katika hali yoyote, Biblia inaonyesha kwamba kuna wakati wa kujikinga. Wakristo wanaweza kuondoshea kando mashambulio yanayowapata wao, familia zao, au wengine wenye uhitaji halisi wa kukingwa.b Lakini wao hawatakuwa wa kwanza kufanya shambulio, wala hawatalipa kisasi kuokoa mali zao. Hawatabeba silaha wakitarajia shambulio; badala yake, wanajitahidi ‘kukaaa katika amani.’—2 Wakorintho 13:11.

[Maelezo ya Chini]

a Ingawa muktadha uonyeshapo kwamba Paulo alikuwa akisema juu ya ugomvi wa maneno, neno la awali linalotumiwa kuwa “ugomvi” (maʹkhe·sthai) kwa kawaida linashirikishwa na kupigana kwa silaha na mkono-kwa-mkono.

b Mwanamke anayetishwa kulalwa kinguvu anapaswa kupiga yowe na kutumia njia yoyote ile akinze ngono.—Kumbukumbu la Torati 22:23-27.

[Picha katika ukurasa wa 12]

Kusalitiwa kwa Kristo, by Albrecht Durer, 1508

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki