Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 10/8 kur. 3-4
  • Hisiamoyo Zisizofaa— Je! Unaweza Kuzishinda?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hisiamoyo Zisizofaa— Je! Unaweza Kuzishinda?
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Tunaweza Kudhibiti Kufikiri Kwetu
  • Hisiamoyo Zisizofaa— Zinaweza Kushindwaje?
    Amkeni!—1992
  • Wewe Unaweza Kuongozaje Maoni Yako ya Moyoni?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Jinsi Wengine Wamejifunza Kushinda Hisiamoyo Zisizofaa
    Amkeni!—1992
  • Ninawezaje Kudhibiti Hisia Zangu?
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 10/8 kur. 3-4

Hisiamoyo Zisizofaa— Je! Unaweza Kuzishinda?

“BILA shaka siwezi! Hisiamoyo zisizofaa ni zenye nguvu mno. Sina la kufanya ila kuzivumilia hadi zinapokwisha.”

Hivyo ndivyo wengi wanavyoitikia wazo la kushinda hisiamoyo kama vile mahangaiko, hofu, hasira, mafadhaiko, hatia, kujisikitikia, na mshuko wa moyo. Lakini hisiamoyo hizo zaweza kushindwa. Badala ya kukubali kushindwa zinapoanza, unaweza kujifunza kupunguza nguvu zazo, labda hata kuziondolea mbali.

Bila shaka, kuna tofauti kubwa kati ya hisiamoyo zisizofaa zilizo za kawaida ambazo huonwa na kila mtu na mshuko mbaya wa moyo. Huenda hizo za pili zikahitaji matibabu ya kistadi. Zile za kwanza hazihitaji matibabu, na hizo ndizo hisiamoyo tunazoweza kujifunza kukabiliana nazo.

Kwa kweli, si hisiamoyo zote zisizofaa zinazodhuru. Kwa mfano, unapofanya kosa zito, huenda ukaonyesha toba kulingana na kosa hilo. Ikiwa hiyo inakusukuma kulisahihisha na kuepuka kulirudia wakati ujao, basi hisiamoyo hiyo imekuwa na matokeo mazuri ya muda mrefu. Au huenda ukawa na hangaiko la kawaida kuhusu tatizo fulani na usukumwe kulitatua kwa idili na kutafuta utatuzi unaofaa. Hilo pia ni itikio lifaalo.

Hata hivyo, namna gani ikiwa baada ya kufanya yote yale uwezayo ili kusahihisha kosa, bado unapata hisi za hatia au kutofaa kitu, labda zikiendelea kwa muda mrefu baadaye? Au namna gani ikiwa baada ya kutatua tatizo kwa kadiri uwezavyo, hisi zako za kuona wasiwasi zinabaki na hata kuongezeka? Basi huenda maitikio yako ya hisiamoyo yakakufanya uhuzunike. Hivyo basi, unaweza kushindaje maitikio hayo ya hisiamoyo? Huenda ufunguo ukapatikana katika kudhibiti kufikiri kwetu.

Tunaweza Kudhibiti Kufikiri Kwetu

Wengi wanaofanya kazi inayohusu afya ya akili husema kwamba hisi zetu huletwa na mawazo yetu. Kwa mfano, Dakt. Wayne W. Dyer asema hivi: “Huwezi kuwa na hisi (hisiamoyo) bila kufikiria jambo kwanza.” Dakt. David D. Burns aongeza hivi: “Kila hisi mbaya unayopata ni tokeo la kufikiri kwako kwa njia isiyofaa.”

Kwa kupendeza, Biblia vilevile huambatanisha mengi ya yale tunayohisi na uteuzi wetu wa mawazo, hivyo hiyo hukazia uhitaji wa kudhibiti kufikiri kwetu. Angalia mistari ifuatayo:

“Siku zote za mtu ateswaye ni mbaya; bali ukunjufu wa moyo ni karamu ya daima.”—Mithali 15:15.

“Msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu [kugeuza akili zenu, New World Translation], mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.”—Warumi 12:2.

“Tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.”—2 Wakorintho 10:5.

“Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani . . . ; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.”—Waefeso 4:22–24.

“Mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.”—Wafilipi 4:8.

“Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.”—Wakolosai 3:2.

Kwa kuwa hisi zako ni tokeo hasa la kufikiri kwako, ufunguo wa kushinda hisiamoyo zisizofaa ni kudhibiti mawazo yanayozitegemeza. Kwa jitihada na wakati wa kutosha, unaweza kujifunza kudhibiti zaidi mawazo yako. Basi tokeo ni kwamba unaweza kufanya vivyo hivyo kwa hisi zako.

Ni kweli, ni rahisi kusema kwamba tunaweza kushinda hisiamoyo zetu zisizofaa. Lakini kufanya hivyo hasa ni jambo jingine. Hivyo basi, tunaweza kukabilianaje na hisiamoyo hizo ambazo huenda zikatuletea magumu mengi?

[Blabu katika ukurasa wa 4]

Si hisiamoyo zote zisizofaa zinazodhuru

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki