Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 2/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2005
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 2/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

“Chronic Fatigue Syndrome” (CFS) (Ugonjwa wa Uchovu Wenye Kusedeka) Tulilia kwa uthamini katika familia yetu tulipopokea Amkeni! yetu juu ya CFS. (Agosti 22, 1992 Kiingereza) Tengenezo la Yehova linajali sana katika kujaribu kuelewesha wale ambao hawajapata ugonjwa huo mbaya wenye kuhofisha! Asanteni sana, pia, kwa shukrani zilizotolewa kwa wale wanaotutunza, wanaotuhangaikia sana.

K. C., Australia

Nilionekana kama vile yule mwanamke kwenye jalada. Makala hizo zilinipatia nguvu ya kwenda kwa daktari na kung’amua kwamba kwelikweli mimi nilikuwa mgonjwa. Nilikuwa nimedhani kwamba ni mshuko wa moyo. Lakini namshukuru Yehova, uchungu ambao nimepata umetoweka.

M. A., Uhispania

Hatimaye, gazeti juu ya CFS! Nimejaribu kuwaeleza wengine jinsi nilivyohisi lakini kwa matokeo yenye kukatiza tamaa au mara nyingi yenye kuaibisha! Makala hizo ni mfano wa jinsi vichapo vyenu hushughulikia mahitaji muhimu ya watu mmoja mmoja.

F. C., Italia

Bado siwezi kuamini kwamba hatimaye nimepata majibu kwa maswali yangu kuhusu afya yangu. Nimekuwa na CFS kwa miaka 14 bila kujua ni ugonjwa gani. Nimeenda kwa madaktari wengi waliosema kwamba nina mshuko wa moyo au tatizo la kihisiamoyo. Nimepeleka nakala za gazeti hilo kwa madaktari 25 kati yao.

J. A. G., Brazili

Tayari nilikuwa na maarifa ya kutosha kuhusu CFS. Yale niliyohitaji zaidi ni yale mliyoandaa katika fungu kwenye ukurasa 14 lililosema juu ya yale ambayo Yehova Mungu hufikiri. Asanteni sana! Mimi hulia kila wakati ninaposoma fungu hilo, mara ambazo sasa zinakaribia 50!

S. D., United States

Ingawa nilikuwa nikilia na kutetemeka kwa hisiamoyo, nilifaulu kusoma makala hiyo. Nilikuwa nikiugua CFS. Ilichukua muda mrefu kugundua ugonjwa wangu. Lakini uchungu wa kimwili ambao nimepata haujawa mwingi kama ule niliohisi kwa sababu ndugu zangu Wakristo hawakuelewa. Inaonekana kwamba Yehova sikuzote hujua wakati wa kutuandalia habari.

K. J., United States

Binti yangu ameugua CFS kwa miaka michache, hivyo nilifurahi sana kupokea Amkeni! ya Agosti 22 (Kiingereza) Ilionyesha matatizo waziwazi hivi kwamba nisingeweza kuweka gazeti hilo chini hadi nilipomaliza. Kisha nikalisoma tena. Hilo litakuwa mojawapo magazeti ninayoweka katika faili yangu ya pekee kwa marejezo ya haraka. Gazeti hilo lilinigusa moyo sana hivi kwamba ilikuwa lazima niwashukuru.

M. E., Uingereza

Wazazi Walevi Asanteni kwa makala “Vijana Wanauliza . . . Mzazi Mlevi—Niiwezeje Hali?” (Agosti 8, 1992 Kiingereza) Baba yangu mzoevu wa kileo anayepata nafuu. Alikuwa mwenye kutenda kijeuri sana, kimwili na kiakili pia. Nilianza kunywa nikiwa mwenye umri mchanga na nilikaribia sana kuwa mzoevu wa kileo mimi mwenyewe wakati ambapo mama yangu alianza kujifunza na Mashahidi wa Yehova. Nina furaha kusema kwamba mnamo Agosti 1991, nilibatizwa! Sasa ninatoa maombi ya kuwa painia, mweneza-evanjeli [wa wakati wote]. Ninathamini jinsi makala hiyo ilivyoelewa hisi za vijana kuelekea wazazi wazoevu wa kileo. Huenda tukawapenda, lakini hilo halimaanishi tunakubali wanayofanya.

L. W., United States

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki