Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 3/22 uku. 12
  • Vimondo Hutoka Wapi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Vimondo Hutoka Wapi?
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Kilicho Nyuma ya Sayari?
    Amkeni!—1999
  • Nyotamkia Yagonga Sumbula!
    Amkeni!—1997
  • Sayari Ndogo, Nyotamkia, na Dunia—Je, Ziko Katika Mwendo wa Kugongana?
    Amkeni!—1999
  • Miamba Inayoruka
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 3/22 uku. 12

Vimondo Hutoka Wapi?

“AA, TAZAMA! Kingine kile!” “Wapi? Wapi?” Je! umepata kusema maneno kama hayo ulipotazama kwenye anga la usiku kuona vimondo (nyota ipitayo kasi angani)? Labda mara ya kwanza ulikiona ghafula kikifanyiza mstari wa nuru juu angani, ilionekana kana kwamba nyota moja ilikuwa ghafula imejitupa kwa kasi angani. Bila shaka, jina kimondo halifai. Huenda “vikajitupa,” lakini hivyo si nyota hata kidogo.

Wanajimu huviita vimondo. Na ingawa nyota ya ukubwa wa kadiri ingeweza kuwa na ukubwa wa sayari yetu yote mara milioni moja, sayari yetu ndiyo yenye ukubwa mara mamilioni ya vimondo hivyo. Vimondo ni nini, navyo hutoka wapi?

Vinafanana sana na kometi. Kometi ya Halley, mfano mashuhuri, ilipita dunia kwa kasi katika 1986 kwenye safari yayo ya umbo la yai kuzunguka jua inayochukua miaka 76. Kwa sababu kometi kwa wazi hufanyizwa sanasana na barafu na vumbi, nyakati nyingine huitwa mipira michafu ya theluji. Kometi inapokaribia jua, sehemu yayo ya juu hupata joto, ikiachilia vumbi na gesi. Kani-eneo la mnururisho wa jua husukuma nyuma sehemu iliyo ngumu katika mkia wenye kunururisha wa vumbi. Hivyo kometi huacha nyuma alama ya vumbi ya takataka—vitu ambavyo vikiwa vingali angani, huitwa metoroidi (mavi ya nyota). Mavumbi mengi ya kometi huwa madogo sana kuweza kuwa vimondo vinavyoonekana. Hesabu ndogo ya vipande vya mavumbi vina ukubwa kama wa chembe ya mchanga, na vichache vina ukubwa wa changarawe ndogo.

Katika visa vichache, njia inayopitia kometi hupitana na ile ya dunia. Hiyo inamaanisha kwamba dunia hukutana na alama ya mavumbi yaleyale kila wakati inapopitia njia ya kometi hiyo. Hilo linapotukia, vimondo vidogo huingia kwenye anga-hewa kwa kasi sana—kufikia kilomita 71 kwa sekunde. Vinapoanguka, vile vikubwa zaidi hupata joto na kuchomeka, vikifanyiza alama nyeupe-moto angani zinazoitwa vimondo.

Dunia inapovuka njia ya kometi, vimondo huonekana kana kwamba vinajitupa katika pande zote kutoka mahali pamoja angani, panapoitwa kinururishi. Kutoka kwa vinururishi hivyo, mvua ya vimondo huanguka katika nyakati barabara za mwaka. Wonyesho mmoja mashuhuri ni mvua ya Perseidisi, iitwayo hivyo kwa sababu kinururishi chayo kinapatikana katika kundi la nyota la Perseusi. perseidisi inapofikia kilele chayo karibu Agosti 12 au 13 kila mwaka, ni wonyesho wenye kutazamisha. Zaidi ya vimondo 60 vyaweza kuanguka kila saa.

Karibu Oktoba 21 unaweza kuona mvua ya Orionidi, ambayo, kama ile mvua ya Akwaridi ya mapema, husemwa kuwa husababishwa na vimondo kutoka kwa Kometi ya Halley. Kulingana na jarida Astronomy, wanasayansi wanakadiria kwamba kometi ya Halley “yaweza kufanya mizunguko 100,000 kabla visehemu vyake vyote kwisha.” Ikiwa wazo lao ni sahihi, kometi ya Halley itarudi kwa ukawaida wakati wa miaka 7,600,000 ijayo! Na hata baada ya hiyo kwisha, hakuna shaka kwamba alama yake ya mavumbi itaendelea kuandalia wakazi wa dunia na vimondo kwa kipindi kirefu baadaye. Vimondo vingi tuonavyo sasa kwa wazi hutoka kwa kometi ambazo kwa muda mrefu zimekuwa hazitendi.

Wanasayansi wanakadiria kwamba ulimwenguni pote, kuna vimondo milioni 200 hivi vinavyoonekana katika anga-hewa letu kila siku. Na kwa habari ya mvua ya vimondo yenye kutokeza zaidi, sikuzote kuna mwaka ujao—na mamilioni ya miaka itakayokuja!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki