Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 1/8 uku. 21
  • Nyotamkia Yagonga Sumbula!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nyotamkia Yagonga Sumbula!
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Kilicho Nyuma ya Sayari?
    Amkeni!—1999
  • Vimondo Hutoka Wapi?
    Amkeni!—1993
  • Sayari Ndogo, Nyotamkia, na Dunia—Je, Ziko Katika Mwendo wa Kugongana?
    Amkeni!—1999
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 1/8 uku. 21

Nyotamkia Yagonga Sumbula!

KWA juma moja katika Julai 1994, karibu vipande 20 vya nyotamkia iitwayo Shoemaker-Levy 9 vilivyogonga Sumbula vilionekana na watazamaji wa nyota ulimwenguni pote. Watazamaji wa nyotamkia walishangaa, kwa kuwa wonyesho huo ulikuja kuwa, kama mwastronomia mmoja alivyotaja, “wonyesho bora zaidi wa anga katika karne hii.” Kwa nini tukio hilo lilipita sana matazamio?

Kwanza, vipande vile vya nyotamkia, vikienda kwa mwendo wa kilometa 200,000 kwa saa, vilitokeza milipuko mikubwa sana ambayo ni matarajio makubwa zaidi tu yaliyokuwa yameitabiri. Kuingia kwa vipande hivyo katika angahewa la Sumbula kulitokeza mimweko ya nuru ambayo ilionekana kwa sekunde kadhaa tu. Kisha, gesi moto sana zilirushwa angani, zikifanyiza matufe-moto makubwa ambayo kwayo milipuko mikubwa zaidi ilitokeza halijoto ambayo ni kali kuliko uso wa jua! Kwa dakika 10 hadi 20 zilizofuata, wingu kubwa liliinuka hadi kimo cha kilometa 3,200.

Isitoshe, kile ambacho mara ya kwanza kilifikiriwa kuwa hali mbaya za kuzuia kuona vizuri kikawa bora kabisa. Kwa sababu upande wenye giza wa Sumbula ndio uliogongwa, mimweko mikali na mawingu yalionekana kwa urahisi zaidi. Katika visa fulani sehemu ya juu ya mawingu hayo iliweza kuonekana ikiinuka juu ya anga ya Sumbula, na mnamo dakika kumi baada ya kugongwa, mzunguko wa Sumbula ulileta sehemu zilizogongwa zikaelekeana na dunia moja kwa moja. Dakika nyingine kumi zilitokeza sehemu zilizogongwa katika jua. Kufikia wakati huo mawingu hayo yalikuwa yametawanyika, na madoa makubwa meusi ndiyo yaliyokuwa yamebaki. Madoa hayo—lile kubwa likizidi ukubwa wa dunia mara mbili—hayakuwa yametabiriwa na waastronomia, na bado yakawa ndizo sehemu ziwezazo kuonekana vizuri zaidi.

Chombo cha angani cha Galileo kiliandaa picha za moja kwa moja za kugongana huko. Katika mzunguko wa dunia, Darubini-Upeo ya Anga ya Hubble iliona kugongana huko katika lukoka za nuru ionekanayo na nuru ya kiuka-urujuani. Vichungulio vingine pia vilipima matokeo ya kugongana huko kwa vipimo mbalimbali vya lukoka ambazo zilichaguliwa kihususa kutoa habari zifaazo. Katika Ncha ya Kusini, jua halikupanda kamwe, jambo lililofanya darubini-upeo ya South Pole Infrared Explorer kuona tukio hilo muda wote.

Watazamaji wa anga wameona tukio lililo nadra sana. Tukio jingine la nyotamkia litatokea lini? Nyotamkia Hale-Bopp, ambayo tayari inaonekana kwa macho matupu, huenda ikawa ndiyo nyotamkia nyangavu zaidi tutakayoona katika karne hii. Itapitia kwa umbali wa kilometa milioni 198 kutoka duniani. Watazamaji wa nyotamkia katika Kizio cha Kaskazini wataona Hale-Bopp katika mwezi wa Aprili 1997. Yote haya yatukumbusha kwamba twaishi katika ulimwengu wenye nguvu na wenye kubadilika-badilika ulioumbwa na Yehova, “Baba wa mianga.”—Yakobo 1:17; Zaburi 115:16.

[Picha katika ukurasa wa 21]

Madoa meusi yaonyesha mahali ambapo vipande vya nyotamkia viligonga Sumbula

[Hisani]

Hubble Space Telescope Comet Team na NASA

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki