Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 5/22 uku. 12
  • Je! Dini Hizi Zina Majibu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Dini Hizi Zina Majibu?
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoa Mimba—Si Suluhisho Lisilo na Madhara
    Amkeni!—2009
  • Je, Utoaji-Mimba—Ndio Suluhisho?
    Amkeni!—1995
  • Muono-Ndani Juu ya Habari
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Matokeo Yenye Msiba ya Utoaji-Mimba
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 5/22 uku. 12

Je! Dini Hizi Zina Majibu?

KATIKA tataniko kubwa la suala la utoaji-mimba, wengi hutafuta mwelekezo wa viongozi wao wa kidini. Hao viongozi huitikiaje?

Kanisa Katoliki huchukua msimamo thabiti dhidi ya utoaji-mimba, likifundisha kwamba uhai huanza wakati wa utungaji wa mimba. Makasisi wengine wamehusika kisiasa na wanamwomba papa awaondoshe Wakatoliki ambao ni wanasiasa wanaopiga kura kwa kupendelea utoaji-mimba. Hata hivyo, Wakatoliki wengi wanapendelea utoaji-mimba na hudai wapewe uhuru wa kufanya hivyo.

Kanisa Presbyterian Church (U.S.A.) laripoti kwamba asilimia 46 ya mapasta “hawaamini kwamba Biblia inafundisha kwamba utoaji-mimba ni mbaya.” Msimamo rasmi wa kanisa ni kupendelea utoaji-mimba.

Mkutano wa 16 wa Makasisi wa United Church of Christ uliazimia kwamba ‘unaunga mkono haki za wanaume na wanawake wawe na huduma za kutosha za kupanga uzazi na pia wakapendekeza chaguo moja liwe njia salama ya utoaji-mimba ulio halali.’

Sera ya kanisa Evangelical Lutheran Church yasema kwamba utoaji-mimba “wapaswa kufanywa ikiwa tu hakuna jambo jingine la kufanya”; lakini lilikataa kuita utoaji-mimba “dhambi” wala kusema kwamba “uhai huanza wakati wa kutunga mimba.”

Kanisa Southern Baptist Convention linapinga sana utoaji-mimba. Lakini kanisa American Baptist Church lasema: “Tumegawanyika kwa habari ya taarifa rasmi ya kanisa kwa hali inayohusu utoaji-mimba. Kwa sababu hiyo, tunatambua uhuru wa kila mtu wa kutetea sera ya umma juu ya utoaji-mimba inayoonyesha itikadi zake.”

Dini ya Kiyahudi imegawanyika, wale wa Orthodoksi wakichukua kwa sehemu kubwa msimamo unaopinga utoaji-mimba, huku Wayahudi wa Reform na Conservative hasa wakipendelea utoaji-mimba.

Uislamu huruhusu utoaji-mimba kwa sababu yoyote ile kwa siku 40 za kwanza za uhai lakini baada ya hapo ni ikiwa tu uhai wa mama unahatarishwa. Kile kitabu Hadith chasema kwamba kijusi hicho “kinabaki siku 40 kikiwa kwa namna ya mbegu, kisha kinakuwa namna ya mgandamano wa damu kwa siku [40] kama hizo tena, kisha kinakuwa namna ya mnofu kwa pindi nyingine kama hiyo, kisha . . . malaika anatumwa kwacho anayepuliza pumzi ndani yacho.”

Dini ya Shinto haina msimamo rasmi na huacha utoaji-mimba kuwa chaguo la mtu binafsi.

Wahindu, Wabuddha, na Wasikhi hufundisha staha ya ujumla kwa uhai. Lakini hawajiingizi katika ubishi wa suala la utoaji-mimba, kwa sababu wanaamini katika kuzaliwa upya katika mwili mwingine; utoaji-mimba humpeleka tu mtoto asiyezaliwa katika uhai mwingine.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki