Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 11/15 uku. 28
  • Muono-Ndani Juu ya Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Muono-Ndani Juu ya Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Ni Mlango wa Maisha Yaliyotangulia?
  • Wakatoliki na Utoaji-Mimba
  • Kutoa Mimba—Si Suluhisho Lisilo na Madhara
    Amkeni!—2009
  • Je! Dini Hizi Zina Majibu?
    Amkeni!—1993
  • Je, Utoaji-Mimba—Ndio Suluhisho?
    Amkeni!—1995
  • Matokeo Yenye Msiba ya Utoaji-Mimba
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 11/15 uku. 28

Muono-Ndani Juu ya Habari

Je! Ni Mlango wa Maisha Yaliyotangulia?

Miezi fulani iliyopita, wasichana watatu wa shule ya msingi na vidato vya kwanza vya shule ya sekondari walipatikana wamezirai katika barabara moja katika Tokushima, Japani, likiwa ni tokeo la kujaribu kujiua. Ni nini kilichochochea kitendo chao? Gazeti Asahi Shimbun liliripoti hivi: “Waliamini kwamba wao walikuwa ni maumbo yaliyozaliwa upya ya mabinti-wafalme wa kale na wakajisadikisha kwamba wangeweza kupata muono mfupi wa maisha yao yaliyotangulia ikiwa wangefikia hatua fulani ya kukaribia kifo.” Lililochochea kisa hiki, lasema gazeti hilo, ni “lile elekeo miongoni mwa watoto la kuingilia ulimwengu wa mafumbo, [ambalo] limekuwa likienea sana muda wa miaka michache iliyopita.” Wasichana hao walikuwa wasomaji wenye bidii wa vitabu vya komiki zenye kukazia kuzaliwa upya kwa umbo jingine.

Hata hivyo, kuikubali dhana ya kuzaliwa upya kwa umbo jingine ni jambo bure tu sawasawa na kujitahidi kufuatia sarabi (mazigazi) jangwani. Biblia yafunua kwamba wakati wa kifo ‘mtu huurudia udongo wake, siku hiyo mawazo yake yapotea.’ (Zaburi 146:4) Ukweli huu juu ya kifo umefunikwa na lile fundisho la udanganyifu kwamba nafsi hubaki hai mtu afapo. Badala ya kufundisha kwamba wanadamu wana nafsi isiyokufa, Biblia husema kwamba nafsi hufa. (Ezekieli 18:4, NW) Lakini kwa wale walio katika kumbukumbu la Mungu kuna tumaini bora la ufufuo. (Yohana 5:28, 29) Pia Biblia yafunua wazi aliye mchochezi wa mafundisho ya nafsi isiyokufa na kuzaliwa upya kwa umbo jingine; yeye ndiye Shetani Ibilisi, “baba wa uwongo.”—Yohana 8:44, HNWW; linganisha Mwanzo 3:4.

Wakatoliki na Utoaji-Mimba

Karibu mwongo mmoja umepita tangu maoni ya umma katika Italia yalipoombwa juu ya utoaji-mimba yakaonyesha kushindwa kwa Kanisa Katoliki. Hata hivyo, katika hati rasmi iliyotolewa majuzi na maaskofu Waitalia, baraza la viongozi Wakatoliki linaonyesha wazi tena kwamba “kukataa kuzoea utoaji mimba au hata kufanya ushirikiano nalo ni wajibu mzito wa kiadili, ambao wategemea msingi wa sheria iliyoandikwa katika moyo wa kila mtu na kuhakikishwa upya na kanisa katika sheria yalo, ambayo huwaadhibu kwa kuwaondosha katika ushirika Wakristo wenye kuzoea utoaji-mimba au kushirikiana nao.”

Waitalia wafikiria nini juu ya utoaji-mimba? Uchunguzi mmoja wa hivi majuzi wenye kuhusisha watu 2,040 ulifunua kwamba kinyume cha maamrisho ya kanisa, Waitalia hukubalia utoaji mimba katika hali nne. (1) Ikiwa mimba yahatarisha uhai wa mama, asilimia 83 wapendelea utoaji-mimba. (2) Kukiwapo na hatari ya kuumbika vibaya kwa kijusi, asilimia 76.3 wapendelea kuikomesha mimba. (3) Afya ya mwanamke iwapo hatarini, asilimia 71.1 wapendelea utoaji-mimba. (4) Ikiwa mimba ni tokeo la kulalwa kinguvu, asilimia 55.2 waafiki kwamba utoaji-mimba wapasa kuruhusiwa. Zaidi ya Mwitalia mmoja kati ya wanne apendelea utoaji mimba “katika hali zote ambamo mwanamke ataka iwe hivyo,” laripoti La Repubblica. Visa vya utoaji mimba wa kisheria na usio wa kisheria vikadiriwavyo kuwa 300,000 hufanywa kila mwaka katika Italia.

Yaonekana wazi kwamba katika mambo hayo ya uhusiano wa kindani, baraza la viongozi Wakatoliki halijaweza kuwapa waumini wao maagizo ya kutosha ya Kimaandiko ili kuwavuta wawe na utii. Hata hivyo, Wakristo wa kweli wamefundishwa mambo ambayo Maandiko husema juu ya habari hii muhimu. Kwa kustahi matakwa bora ya kiadili ya Biblia, wao hawafanyi utoaji-mimba katika yoyote ya zile hali nne zilizoelezwa juu.—Kutoka 21:22-25; ona pia Zaburi 139:14-17; Yeremia 1:5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki