Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 9/8 kur. 5-6
  • Vatikani 2—Baraka au Laana?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Vatikani 2—Baraka au Laana?
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • ‘Kweli Katika Dini Nyinginezo’
  • Vatikani 2—Ni Laana?
  • Vatikani 2—Ni Baraka?
  • Kanisa—Mabadiliko na Mvurugo
    Amkeni!—1993
  • Kwa Nini Ule “Wasiwasi Mwingi”?
    Amkeni!—1991
  • Jaribio la Kutimua Vatikani Kutoka UM
    Amkeni!—2000
  • Kwa Nini Ile Migawanyiko?
    Amkeni!—1991
Amkeni!—1993
g93 9/8 kur. 5-6

Vatikani 2—Baraka au Laana?

ILIKUWA 1962 katika Vatikani. Papa alifungua dirisha katika makao yake ya Vatikani, mbele ya askofu mwenye kushangaa. Papa John wa 23 alitoa kielezi cha jambo alilotarajia kutoka kwa Baraza la Pili la Vatikani (1962-65): kuingiza hewa safi katika Kanisa Katoliki, ili kuwe na aggiornamento, kufanya mambo yawe ya kisasa.

Ni mabadiliko gani ambayo hilo baraza lilileta katika kanisa? Hilo bado ni swali lifaalo, kwa kuwa Vatikani 2 na matokeo yayo yanabishaniwa sana hata leo.

‘Kweli Katika Dini Nyinginezo’

Papa John wa 23 alitaka mabadiliko—hilo lilikuwa dhahiri sana. Wanatheolojia ambao mawazo yao mapya yalikuwa yamekataliwa miaka michache iliyopita walikaribishwa kwenye Baraza la Vatikani kuwa wastadi. Wakuu wa Orthodoksi na Protestanti walialikwa pia wawe watazamaji.

Mtazamo huo mpya ulisababisha mabadiliko makubwa sana kuhusiana na mambo ya uhuru wa dini na dhamiri. Kwa karne nyingi kanisa lilikuwa limeshutumu kabisa mawazo hayo; Gregory wa 16, papa wa karne ya 19, hata aliyafafanua kuwa “upumbavu.” Hata hivyo, katika 1964, likikubaliwa na watu wengi, baraza lilikubali agizo la kwamba kila mtu alikuwa na haki ya kuchagua dini yake mwenyewe. Hilo lilipita uhuru kamili na ulio sahili, kama vile gazeti Notre Histoire lilieleza: “Kuanzia wakati huo kuendelea, ilikubaliwa kwamba kweli fulani ilipatikana katika dini nyinginezo.”

Baada ya Vatikani 2 kanisa liliendelea na sera yalo ya uhuru zaidi kuelekea dini nyingine. Akionyesha jambo hili, Papa John Paul wa 2 alimtembelea Mfalme Hassan wa 2 wa Moroko, kiongozi wa kiroho wa waislamu. Pia alitembelea kanisa la Protestanti na sinagogi moja katika Roma. Wakatoliki wengi wanakumbuka ule mkutano wa 1986 katika Assisi, Italia, ambapo Papa John Paul wa 2 alikaribisha viongozi wa dini kuu za ulimwengu waombe pamoja naye kwa ajili ya amani.

Vatikani 2—Ni Laana?

Kwa wengine, “mabadiliko yenye kuburudisha” yaliyotumainiwa na Papa John wa 23 yalikuwa mabadiliko makubwa kwelikweli.” Ili kuunga mkono maoni yao, walitaja hotuba iliyojulikana sana ambayo Papa Paul wa 6, aliyekuwa mwandamizi wa John wa 23, alitangaza kwamba “moshi wa Shetani” ulikuwa umepenya kanisani. Kitabu La Réception de Vatican II kilieleza kwamba, kwa kutangaza kwake, Paul wa 6 “alionekana kufungamanisha matukio yaliyotokezwa na baraza hilo na mwendo ulio kinyume cha mapendezi ya kanisa.”

Waenda-kanisani wengi wanashiriki maoni hayo. Uchunguzi wa karibuni ulionyesha kwamba karibu nusu ya Wakatoliki katika Ufaransa wanafikiri kwamba “kanisa limepita kiasi katika kufanya mageuzo.” Wachambuzi wa Vatikani 2 wanashtaki kanisa kwa kukosa kubaki jaminifu kwa desturi zalo lakini linajichafua lenyewe na umambo-leo. Wanasema kwamba kanisa limeunga mkono mabadiliko ambayo yametikisa jamii ya Magharibi na yamesababisha shida katika kanisa.

Vatikani 2—Ni Baraka?

Kwa wengine si baraza ambalo linapaswa kutiliwa shaka. Wanasema kwamba dalili za kwanza za udhaifu katika kanisa zilionekana dhahiri kabla ya Vatikani 2. Gazeti la kila siku la Ufaransa La Croix lilikiri hivi: “Upungufu wa tamaa ya kufanya kazi ya ukasisii na ile isiyo ya ukasisi katika nchi za Magharibi unapaswa kuonwa kuhusiana na shida ya ujumla katika jamii na matokeo yayo kwa jumuiya za Kikristo: Wakristo wengi sana wamejiruhusu wawe na maoni ya ki-siku-hizi na mawazo ya kidesturi.”

Bado wengine wanahisi kwamba mabadiliko yaliyopendekezwa na Vatikani ya 2 yalikuwa muhimu. Mwandikaji mwingine wa La Croix alisema: “Mtu . . . anaweza kushangaa kanisa lingekuwaje ikiwa lingebaki kama lilivyokuwa.” Mwishowe, wasemaji mbalimbali Wakatoliki hueleza kwamba kanisa ni tengenezo lenye binadamu wasiokamilika, na kwamba limepata shida wakati uliopita na litatatua hii pia. Gilles, aliyetajwa kwenye makala iliyotangulia, alisema hivi: “Tulipotaja matatizo ya kanisa, tuliambiwa kuwa kanisa lilikuwa katikati ya shida kama ya tineja na kwamba lingeipita bila athari yoyote.”

Iwe Vatikani 2 ilichangia mabadiliko mazuri au mabaya, imekuwa na athari kubwa sana kwa Wakatoliki, kama tutakavyoona kwenye makala ifuatayo.

[Picha katika ukurasa wa 6]

Baraza la Pili la Vatikani lilisababisha mabadiliko na mvurugo

[Hisani]

UPI/Bettman Newsphotos

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki