Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 9/22 uku. 20
  • Serikali ya Ulimwengu—Je! Umoja wa Mataifa Ndilo Jibu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Serikali ya Ulimwengu—Je! Umoja wa Mataifa Ndilo Jibu?
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Umoja wa Mataifa—Njia Bora Zaidi?
    Amkeni!—1992
  • Fumbo Lenye Kutia Hofu Lafumbuliwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
  • Je, Ulimwengu Usio na Vita Wawezekana?
    Amkeni!—1996
  • Ziara ya Papa kwa UM—Ilitimiza Nini?
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 9/22 uku. 20

Serikali ya Ulimwengu—Je! Umoja wa Mataifa Ndilo Jibu?

KATIKA miaka ya karibuni shirika la Umoja wa Mataifa limetumainiwa tena na kuvutia katika ulimwengu. Kwa mamilioni ya watu ule ufupisho “UM” huleta mawazo ya shujaa: wanajeshi wenye kofia buluu wakikimbilia sehemu zenye matatizo ulimwenguni kwa ujasiri ili kuleta amani, wafanyakazi wa kutoa msaada wakileta chakula kwa wakimbizi katika Afrika, na wanaume na wanawake waliojiweka wakfu wakifanya kazi bila choyo kusimamisha utaratibu wa ulimwengu mpya.

Kulingana na uchunguzi wa miezi tisa uliofanywa na The Washington Post, kama ulivyoripotiwa katika International Herald Tribune, ukweli wa ule ushujaa ni “ubwana mkubwa sana usiodhibitiwa unaoweza kutumiwa vibaya na mapungufu yanayodhoofisha uwezo walo wa kutenda.” Uchunguzi huo, unaotegemea maelfu ya kurasa za hati na mahoji ya maofisa wa sasa na wa zamani wa UM, ulifunua hali hii inayofuata.

Msaada kwa Afrika: Shirika la UM lilimwaga mabilioni ya dola zilizohitajiwa sana zikiwa msaada katika Afrika, bara ambalo limeharibiwa kabisa na vita, njaa kubwa, umaskini, na maradhi. Uhai mwingi umeokolewa.

Lakini, maelfu ya uhai na mamilioni ya dola zimepotea pia kwa sababu ya usimamizi mbaya, uzembe, na, nyakati nyingine ufisadi. Shirika la UM limeingiza msaada katika Somalia yenye njaa kubwa, ambako watu wengi wamekuwa wakifa kila siku. Lakini Aryeh Neier, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Haki za Kibinadamu, anukuliwa akisema hivi katika Tribune: “Umoja wa Mataifa na mashirika yayo mengi yamekuwa yenye uzembe sana na kutoweza kutekeleza mambo hivi kwamba ni kama hayajashiriki daraka lolote kabisa katika kuondoa huzuni ya Somalia.”

Ripoti hiyo pia ilishtaki kwamba baadhi ya maofisa wa UM wamehuhishwa katika kugeuza kando msaada wa chakula, kutumia vibaya msaada wa kibinadamu, kutumia kwa njia ya kupunja vifaa, magendo, na kutumia vibaya ubadilishaji wa fedha. Wachunguzi wa UM walipata uthibitisho wa kupunja huko katika nchi za Kiafrika zisizopungua saba.

Udumishaji wa Amani: Kudumisha amani ndio mradi mkubwa wa UM, ingawa katika miaka ambayo imepita tangu lianzishwe katika 1945, kumekuwa na mapigano makubwa zaidi ya mia moja, na watu zaidi ya milioni 20 wameuawa katika vita. Hata hivyo, tangu 1987, shirika la UM limeanzisha utendaji 13 wa kudumisha amani, mwingi kufikia kadiri ambayo limepata kufanya katika historia yalo yote kabla ya wakati huo.

Ingawa wengine waweza kubisha kwamba ni afadhali kuwa na gharama ya utendaji huo mbalimbali kuliko matokeo mabaya ya vita, wengi wanalalamika kwamba mambo yamekuwa mabaya sana. Kwa kielelezo, utendaji wa kudumisha amani huendelea kwa miongo ya miaka, ukitumia mamia ya mamilioni ya dola wakati mijadala ya kupata amani inakwama. Tume ya kudumisha amani ya UM katika Kambodia hutoa zaidi ya dola milioni 1 kwa ajili ya TV na vidio kwa ajili ya majeshi na dola nyinginezo 600,000 kwa ajili ya maandikisho ya magazeti.

Marekebisho: Kuna maombi mengi ya kutaka marekebisho ndani ya shirika la UM, lakini maoni yatofautiana juu ya ni nini kinachohitaji kurekebishwa. Nchi zinazoendelea zinataka ziwe na ushiriki mkubwa zaidi katika kufanya maamuzi na zingependa zieneze programu za kiuchumi na kijamii. Nchi zenye maendeleo kiviwanda zinataka kupunguza programu hizo na kumaliza ufisadi, usimamizi mbaya na matumizi mabaya.

Ofisa mmoja wa juu wa UM alisema hivi: “Ili urekebishe kabisa ni lazima ufanye jambo ambalo haliwezekani kufanywa katika mfumo wa urasimu: Ni lazima usafishe mahali hapo kabisa. Ili ufanye jambo la maana, ni lazima uondoe kasoro za miaka 45, na hizo ni kasoro nyingi.”

Ingawa Wakristo wanaona uhitaji wa kuwa na usimamizi mmoja wa mambo ya kibinadamu, hawaamini kwamba Umoja wa Mataifa ndilo jibu. Badala ya hivyo, wanatazamia Ufalme wa Mungu, ile serikali ambayo Yesu aliwaambia wafuasi wake wasali juu yayo.—Mathayo 6:9, 10.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki