Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 4/22 uku. 3
  • Je, Ulimwengu Usio na Vita Wawezekana?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Ulimwengu Usio na Vita Wawezekana?
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Kuna Wakati Ujao Gani kwa Vita?
    Amkeni!—1999
  • Umoja wa Mataifa—Njia Bora Zaidi?
    Amkeni!—1992
  • Mipango ya Mwanadamu kwa Ajili ya Usalama wa Kimataifa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Serikali ya Ulimwengu—Je! Umoja wa Mataifa Ndilo Jibu?
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 4/22 uku. 3

Je, Ulimwengu Usio na Vita Wawezekana?

WAZIA kutoona tena kamwe au kupatwa tena na uhalisi wenye kutisha wa vita na matokeo yayo. Wazia kutosikia tena kamwe sauti ya mpigo wa bunduki au mabomu, kutoona tena vikundi vya wakimbizi wanaokaribia kufa kwa njaa wakitoroka, kutojiuliza tena kamwe ikiwa wewe au mpendwa wako atakufa katika vita yenye ukatili na isiyo na maana. Itakuwa vizuri ajabu kuishi katika ulimwengu usio na vita!

‘Si taraja linalowezekana,’ huenda ukasema. Hata hivyo, mwono wa ulimwengu wenye amani ulikuwa mwangavu miaka michache tu iliyopita. Katika 1990 na 1991, wengi walikuwa wakisema kwamba mataifa yalikuwa mwanzoni mwa enzi mpya ya usalama na ushirikiano. Akidhihirisha hali ya nyakati hizo, George Bush, aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo, katika pindi nyingi alisema juu ya “utaratibu wa ulimwengu mpya” uliokuwa ukizuka.

Kwa nini kulikuwa na matarajio hayo? Vita Baridi ilikuwa imekwisha. Kwa zaidi ya miaka 40, lile tisho la vita ya nyuklia lilikuwa limening’inia kwa njia hatari juu ya jamii ya kibinadamu kama upanga ulioning’inizwa kwa kamba nyembamba. Lakini Ukomunisti ulipokoma na Muungano wa Sovieti kuvunjika, tisho la maangamizi makubwa ya nyuklia lilielekea kutoweka. Ulimwengu ukatulia.

Kulikuwa na sababu nyingine kubwa iliyofanya watu waone wakati ujao wakiwa na uhakika, na inayofanya watu wengi bado waendelee kuuona hivyo. Kwa miongo minne uadui kati ya Mashariki na Magharibi ulikuwa umefanya Umoja wa Mataifa kiwe jamii ya majadiliano tu. Lakini mwisho wa Vita Baridi uliweka UM huru kufanya kile lilichoundwa kufanya—kujaribu kuleta amani na usalama wa kimataifa.

Katika miaka ya majuzi UM limeongeza jitihada za kukomesha vita. Likijiandaa kwa majeshi kutoka mataifa shirika, Umoja wa Mataifa lilijiingiza katika shughuli za kudumisha amani katika miaka 4 iliyotangulia 1994 kuliko katika miaka 44 iliyopita. Wafanya kazi wa kiraia na wa kijeshi wapatao 70,000 walitumikia katika opereshani 17 kotekote ulimwenguni. Kwa miaka miwili tu, matumizi ya kudumisha amani yalirudufika hadi dola bilioni 3.3 katika 1994.

Boutros Boutros-Ghali, katibu-mkuu wa UM, aliandika majuzi hivi: “Kuna ishara kwamba mfumo wa usalama wa jumla ulioanzishwa katika San Fransisco yapata miaka 50 iliyopita [wakati wa kuanzishwa kwa UM] hatimaye waanza kutenda kama ilivyonuiwa tangu mwanzoni . . . Twafanya maendeleo kuelekea kupata mfumo wa kimataifa uwezao kutenda.” Licha ya maendeleo haya, mwono wa utaratibu wa ulimwengu mpya hufifia haraka. Ni nini kimetukia kutia giza matumaini ya ulimwengu usio na vita? Je, kuna sababu yoyote ya sisi kuamini kwamba tutapata kuona amani ya duniani kote? Makala zifuatazo zitazungumzia maswali haya.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Ndege za kivita: picha ya USAF

Bunduki za kulipua ndege: picha ya U.S. National Archives

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki