Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 10/8 uku. 15
  • Mashahidi wa Yehova Watetewa Katika Vita ya Kutunza Watoto

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mashahidi wa Yehova Watetewa Katika Vita ya Kutunza Watoto
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Kuna Mahakama ya Kimataifa Ulaya?
    Amkeni!—1996
  • Kupigania Uhuru wa Kuabudu
    Ufalme wa Mungu Unatawala!
  • Mashahidi wa Yehova Watetewa Katika Ugiriki
    Amkeni!—1997
  • Kulinda Kisheria Habari Njema
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 10/8 uku. 15

Mashahidi wa Yehova Watetewa Katika Vita ya Kutunza Watoto

TANGU katikati ya mwongo uliopita, Ingrid Hoffmann amekuwa akishindana aweze kuwatunza watoto wake wawili. Yeye akiwa mwanamke Mwaustria, alizaliwa na kulelewa akiwa Mkatoliki wa Roma. Yeye alioa Mkatoliki mwenzake, na kuzaa mwana katika 1980 na binti katika 1982. Lakini katika 1983 mume na mke hao wakatalikana; wazazi wote wawili walitaka wawatunze watoto hao. Baba huyo alidai kwamba dini ya mama huyo—yeye alikuwa amekuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova—ingewadhuru watoto, ikiwanyima malezi ya kawaida, yenye mafaa. Yeye alitaja mambo kama vile kukataa kwa Mashahidi kusherehekea sikukuu fulani zilizo mashuhuri nchini mwake na kukataa kwao kutiwa damu mishipani.—Matendo 15:28, 29.

Hoja hizo za kijuu-juu zilikosa kusadikisha. Mahakama zote mbili, ile ya chini na ya rufani zilikataa madai ya baba huyo na zikampa mama huyo haki ya kutunza watoto. Hata hivyo, katika Septemba 1986, Mahakama Kuu ya Austria ilibadili ule uamuzi wa mahakama za chini. Ilidai kwamba maamuzi hayo yalikuwa yamekiuka Sheria ya Elimu ya Kidini ya Austria, sheria inayotaka watoto waliozaliwa na Wakatoliki waelimishwe kuwa Wakatoliki. Mahakama hiyo iliamua pia kwamba haingekuwa kwa masilahi bora ya watoto kuwaruhusu walelewe kuwa Mashahidi wa Yehova!

Ingrid Hoffmann alipata msaada wapi dhidi ya ubaguzi huo wa kidini wa waziwazi? Katika Februari 1987 kesi yake ilipelekwa mbele ya Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ulaya. Mnamo Aprili 13, 1992, tume hiyo, inayofanyizwa na mahakimu wanaowakilisha mataifa mbalimbali yaliyo washirika wa nchi za Jumuiya ya Ulaya, ilipeleka kesi hiyo mbele ya Mahakama ya Haki za Kibinadamu ya Ulaya ili isikizwe kikamili.

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi mnamo Juni 23, 1993. Hiyo ilisema hivi: “Kwa hiyo Mahakama ya Ulaya inakubali kwamba kumekuwa na tofauti katika namna ya kutendewa na kwamba tofauti hiyo ilikuwa kwa msingi wa kidini; mkataa huu unaungwa mkono na maneno na hali ya kusababu ya Mahakama Kuu [ya Austria] juu ya matokeo halisi ya dini ya mshtaki. Tofauti hiyo katika namna ya kutendewa ni yenye ubaguzi.” [Italiki ni zetu.] Iliendelea kusema kwamba Mahakama Kuu “iliamua mambo kwa njia tofauti na ile ya mahakama za chini, ambazo uamuzi wazo hata uliungwa mkono na maoni ya wataalamu wa kisaikolojia. Kujapokuwa hoja zozote zinazoweza kutolewa zilizo kinyume cha hayo, hali ya kutofautisha inayotegemea hasa tofauti ya kidini pekee haikubaliki.”

Kwa kura ya watano dhidi ya wanne, hao mahakimu waliamua kwa kumpendelea Ingrid Hoffmann na dhidi ya Austria, wakisema hasa kwamba Austria ilikuwa imemwonea kwa msingi wa dini yake na ilikuwa imevunja haki yake ya kulea familia yake. Isitoshe, kwa kura ya wanane dhidi ya mmoja, hao mahakimu walimpa ridhaa ya kifedha.

Ushindi huo wenye kutokeza wa uhuru wa kidini ulikuja mwezi mmoja tu baada ya ushindi mwingine katika mahakama iyo hiyo—kesi ya Kokkinakis v. Greece, iliyoamua kwamba Ugiriki ilikuwa imevunja haki ya kibinadamu ya kuweza kufundisha Neno la Mungu nyumba kwa nyumba. Wapendao uhuru ulimwenguni pote hushangilia wakati majaribio hayo ya kuzuia uhuru wa kidini yanaposhindwa huku haki za kibinafsi za kumwabudu Mungu na kulea familia kulingana na kanuni za Biblia zikilindwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki