Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 11/8 kur. 6-10
  • Je! Kuna Nafasi ya Kutosha Mwanadamu na Mnyama?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Kuna Nafasi ya Kutosha Mwanadamu na Mnyama?
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Idadi ya Watu Yenye Kupita Kiasi —Ndilo Tisho la Pekee?
  • Ni Nani Atakayekuwa wa Kwanza?
  • Mwelekeo Mpya Katika Hifadhi
  • Ni Nani Alindaye Wanyama wa Pori wa Afrika?
    Amkeni!—1993
  • Yule Mnyama Mwenye Hizo Pembe Zenye Bei
    Amkeni!—1995
  • Vifaru Mayatima wa Kenya
    Amkeni!—1998
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2015
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 11/8 kur. 6-10

Je! Kuna Nafasi ya Kutosha Mwanadamu na Mnyama?

NI KWA nini wanyama wa pori wanapungua katika sehemu nyingi za Afrika? (Ona sanduku, ukurasa ufuatao.) Watu fulani hulaumu ukuzi wa haraka wa idadi ya watu wa kontinenti hii.

Ni kweli kwamba sehemu fulani za Afrika, hasa mijini, zina idadi kubwa ya watu kupita kiasi. Maeneo ya mashambani vilevile yamekaushwa na mifugo ya wakulima wengi. Kwa kielelezo, fikiria maeneo yenye watu wengi sana ya Venda, Gazankulu, na Kangwane, yanayopiga mpaka na Mbuga ya Kitaifa ya Kruger. Makazi hayo ya weusi yalifanyizwa yakiwa sehemu ya sera ya zamani ya ubaguzi wa rangi ya Afrika Kusini na yana msongamano wa watu kutoka watu 70 hadi watu wanaopita 100 kwa kila kilometa moja ya mraba. Kusafiri kupitia maeneo hayo kwenda kufurahia likizo katika Mbuga ya Kitaifa ya Kruger kwaweza kukasirisha sana. “Jumuiya zinazoishi mpakani . . . ni maskini, wengi wakiwa hawana kazi na wenye njaa,” laeleza gazeti la habari la Afrika Kusini Sowetan. “Wanyama,” lasema gazeti jingine la hapo, The Natal Witness, “huishi katika fahari yenye utele katika upande wao wa ua.”

Kulingana na ripoti za karibuni, wenye mamlaka wa Mbuga ya Kruger wanakusudia kufanya mambo zaidi ili kusaidia watu wanaoishi kwenye mipaka ya mbuga hiyo. Lakini ni jambo gani lingetokea ikiwa nyua zote zingebomolewa na kusiwe na kizuizi kwa wawindaji, wachungaji, na walowezi? Wahifadhi wahofia kwamba hatimaye wengi wa wanyama wa pori wangeangamizwa, kama ilivyotokea katika nchi nyinginezo.

Hifadhi za wanyama zinazosimamiwa vizuri huwa na fungu kubwa katika kuhifadhi wanyama wa pori, hasa katika maeneo yenye wakazi wengi sana. Hifadhi zaweza pia kuleta fedha zinazohitajika sana kutoka kwa watalii wa kigeni. (Ona sanduku, ukurasa 5.) “Maeneo hayo,” amalizia mwandishi Mwafrika Musa Zondi, katika makala iliyorejezewa juu katika gazeti Sowetan, “pia huandaa fursa za kazi kwa maelfu ya watu—hasa wale wanaoishi kando ya hifadhi hizo. Zaidi ya hayo, hiyo ni urithi wetu. Hatuwezi kuwaachia watoto wetu zawadi bora kuliko sehemu hizo.”

Idadi ya Watu Yenye Kupita Kiasi —Ndilo Tisho la Pekee?

Ongezeko kubwa la idadi ya watu si tisho la pekee kwa wanyama wa pori wa Afrika. Kwa kielelezo, ebu fikiria nchi nne zilizo kubwa zinazoshiriki mipaka: Namibia, Botswana, Angola, na Zambia. Nchi hizo zikiwa pamoja zina eneo kubwa kuliko India, na hali zina jumla ya msongamano wa watu 6 tu kwa kila kilometa moja ya mraba. Idadi hiyo si kubwa kwa kulinganisha na msongamano wa watu katika nchi kama Ujerumani, ikiwa na watu 222 kwa kila kilometa ya mraba; Uingereza, ikiwa na watu 236 kwa kila kilometa ya mraba; na India, ikiwa na watu 275 kwa kila kilometa ya mraba! Kwa kweli, msongamano wa watu katika kontinenti nzima ya Afrika, watu 22 kwa kila kilometa ya mraba, ni chini sana ya wastani ya ulimwengu wa watu 40.

“Idadi ya watu katika Afrika inaongezeka kwa kasi sana,” akiri Mzambia Richard Bell katika kitabu Conservation in Africa, “lakini jumla kuu ya msongamano wa watu bado ni chini kwa kulinganishwa isipokuwa tu katika sehemu fulani-fulani zenye watu wengi.”

Maradhi, ukame wenye madhara makubwa, vitendo vya kimataifa vya uwindaji haramu, vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kupuuzwa kwa wakulima wa hali ya chini wa sehemu za mashambani zote huchangia kupungua kwa wanyama wa pori wa Afrika.

Yale mapambano ya mataifa yenye nguvu zaidi kati ya ile iliyokuwa Muungano wa Sovieti na Magharibi yalitokeza mizozano kotekote katika Afrika, huku pande zote mbili zikimwaga kwa wingi silaha za hali ya juu katika kontinenti hiyo. Mara nyingi, baadhi ya silaha za hali ya juu zimetumiwa kuua wanyama wa pori ili kulisha majeshi yenye njaa na kupata silaha nyingi zaidi kutokana na mauzo ya pembe za ndovu, pembe za vifaru, na sehemu nyinginezo za miili ya wanyama na vitu vinavyotokana nao. Uharibifu wa kasi wa wanyama wa pori haukukoma baada ya Vita Baridi. Silaha hizo bado zabaki katika Afrika. Kuhusu moja ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Afrika, katika Angola, jarida Africa South laripoti hivi: “Uwindaji haramu, uliokuwa tayari umeenea sana wakati wa vita, umeongezeka zaidi tangu vita vikome kwa sababu hakujawa na udhibiti juu ya wapiganaji walioondolewa jeshini.” Na tangu wakati huo vita hiyo imeanza tena.

Wawindaji haramu wengi huhatarisha maisha zao kwa sababu ya kiasi kikubwa cha fedha zinazohusika. “Pembe moja tu ya [kifaru] yaweza kutokeza dola 25,000 [za U.S.],” laripoti gazeti moja la habari la Kiafrika, The Star. Mhifadhi, Dakt. Esmond Martin, alizuru nchi moja ya Esia katika 1988 na kupata kwamba bei ya pembe ya kifaru ilikuwa imeongezeka kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka dola 1,532 za U.S. hadi dola 4,660 za U.S. kwa kilo moja.

Ni Nani Atakayekuwa wa Kwanza?

Hatua kali tayari zimechukuliwa ili kuvuta uangalifu kwa tisho liletwalo na mahitaji ya pembe za ndovu na vifaru. Katika Julai 1989, mamilioni ya watazamaji wa televisheni kotekote ulimwenguni walitazama rundo kubwa la tani 12 za pembe za ndovu, zilizokadiriwa kuwa na thamani ya kati ya dola milioni tatu na milioni sita, likiwashwa moto na rais wa Kenya, Daniel arap Moi. Mkurugenzi wa Wanyama wa Pori wa Kenya, Dakt. Richard Leakey, aliulizwa jinsi angetetea potezo hilo la wazi. “Hatungeweza kusadikisha watu wanaoishi katika Amerika, Kanada, au Japani wakome kununua pembe kama tulikuwa tungali tukiziuza,” yeye alijibu hivyo. Kwa kweli hatua kama hizo zilishtua watu wengi na kuwafanya washirikiane na marufuku ya kimataifa juu ya biashara ya pembe za ndovu. Mahitaji ya vitu vinavyotokana na pembe yakapungua sana.

Kwa habari ya vifaru, hali ni tofauti. Ingawa rais wa Kenya aliteketeza pembe za vifaru zenye thamani ya mamilioni ya dola katika 1990, mahitaji yaendelea. (Ona sanduku “Sababu Inayofanya Pembe ya Kifaru Ipendwe Sana,” ukurasa 9.) Ili kulinda idadi ya vifaru inayozidi kupungua, nchi fulani zimeamua kukata kwa msumeno pembe za viumbe hivyo. Nyakati nyingine inakuwa ni mbio za kufa na kupona za kuona ni nani atakayekuwa wa kwanza, yule mhifadhi mwenye kishale chenye kumaliza nguvu za mnyama huyo au yule mwindaji haramu mwenye silaha hatari yenye kuua.

Mwelekeo Mpya Katika Hifadhi

Wawindaji na wahifadhi kutoka nchi za Magharibi wamethamini kwa muda mrefu uwezo wa wakazi wa mashambani kufuatia nyayo za wanyama. Kwa kweli Waafrika wengi wana ujuzi wenye kutokeza sana wa wanyama wa pori. “Mwingi wa ujuzi huo,” aeleza Lloyd Timberlake katika kitabu chake Africa in Crisis, “hupitishwa kwa masimulizi ya mdomo, na unaelekea kutoweka kwa sababu Waafrika wanahama kutoka mashambani kwenda majijini . . . Basi ulimwengu umo katika hatari ya kupoteza jambo lile . . . mwanthropolojia Leslie Brownrigg ameiita ‘karne nyingi za utafiti wa watu wengi.’”

Katika wakati uliopita, serikali za kikoloni zilianzisha mbuga za kitaifa kwa kupuuza wakulima waliotegemea wanyama wa pori kwa ajili ya chakula kwa karne nyingi. Sasa baadhi ya serikali za Kiafrika zataka kusaidia wakulima hao wa mashambani waliopuuzwa kwa muda mrefu. “Katika mataifa kadhaa ya kusini mwa Afrika,” yaripoti Taasisi ya Worldwatch, “taifa limeacha kuwa na udhibiti wote juu ya wanyama wa pori. Watu wa jumuiya za mashambani wanaoishi katika sehemu 10 kati ya zile 31 za Maeneo ya Usimamizi wa Hifadhi wa Wanyama wa Pori ya Zambia wamepewa haki ya kushughulikia wanyama wa pori; kama matokeo, uwindaji haramu umepungua sana na idadi za wanyama wa pori zaonekana kuwa zaongezeka.” Kuna ripoti nyinginezo za mafanikio katika sehemu ambazo wakulima wa hali ya chini wamejihusisha na hifadhi yao wenyewe, kama vile miongoni mwa vifaru-weusi na ndovu-jangwa wa Kaokoland katika Namibia, katika hifadhi za wanyama wa pori za Kangwane katika Afrika Kusini, na katika nchi nyinginezo za Afrika.

Ujapokuwa mwendo huo mzuri, wahifadhi wa wanyama wa pori bado huhangaika juu ya wakati ujao. Mwelekeo huo ni suluhisho la muda mfupi tu. Baada ya muda mrefu, ukuzi wa haraka wa idadi ya ainabinadamu bado wabaki kuwa tisho. “Kufikia karne inayofuata,” laeleza U.S.News & World Report, “idadi ya wanadamu yatazamiwa kuongezeka kwa karibu bilioni 5, sanasana katika nchi zinazoendelea ambazo pia ndizo himaya za wanyama wa pori katika [dunia].”

Huku idadi ya watu ipanukapo na kuingia ndani ya maeneo ya pori, hitilafiano hutokea kati ya mwanadamu na mnyama. “Aina nyingi za wanyama wakubwa wa Afrika hazipatani na maendeleo mengi ya sehemu za mashambani, kwa kielelezo ndovu, kiboko, kifaru, nyati, simba na mamba, na vilevile baadhi ya paa wakubwa, jamii ya nyani na nguruwe,” chaeleza kitabu Conservation in Africa.

Kwa sababu inaonekana kwamba mwanadamu hana suluhisho la kule kuokoka kwenye kudumu kwa wanyama wa pori wa Afrika, ni nani aliye na suluhisho?

[Sanduku/Ramani katika ukurasa wa 7]

“Nyati wamepungua kutoka 55,000 hadi chini ya 4,000, kuro kutoka 45,000 hadi chini ya 5,000, pundamilia kutoka 2,720 hadi chini ya 1,000, na kiboko wamepungua kutoka 1,770 hadi karibu 260.”—Mlinganisho wa uchunguzi uliofanywa angani katika 1979 na 1990 katika Marromeu Delta ya Msumbiji na kuripotiwa katika jarida African Wildlife, la Machi/Aprili 1992.

“Katika 1981 karibu pundamilia 45,000 walihama kupitia mbuga na misitu [za kaskazani mwa Botswana]. Lakini kufikia 1991 ni wapatao 7,000 tu waliomaliza safari hiyo.”—Kutoka katika gazeti Getaway likichanganua vidio ya wanyama wa pori inayoitwa Patterns in the Grass, mnamo Novemba 1992.

“Wakati wa ziara yetu [kwenda Togo, Afrika Magharibi] tulipata idadi ya ndovu wa misitu yenye kushangaza na isiyotarajiwa katika Hifadhi ya Asili ya Fosse aux Lions . . . Hesabu iliyofanywa kutoka angani katika Machi 1991 ilitokeza wanyama 130. . . . [Lakini kwa muda unaopungua mwaka mmoja,] idadi ya ndovu katika Fosse aux Lions ilikuwa imeshuka hadi 25.” —Liliripotiwa katika jarida African Wildlife, Machi/Aprili 1992.

[Ramani]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Hifadhi za wanyama wa pori za Afrika hutimiza fungu kubwa katika huhifadhi aina nyingi za wanyama

AFRIKA

MOROKO

SAHARA YA MAGHARIBI

MAURITANIA

ALGERIA

MALI

TUNISIA

LIBYA

NIGER

NIGERIA

MISRI

CHAD

SUDAN

JIBUTI

ETHIOPIA

JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

KAMEROON

KONGO

Kabinda (Angola)

GABON

ZAIRE

UGANDA

KENYA

SOMALIA

TANZANIA

ANGOLA

ZAMBIA

MALAWI

NAMIBIA

ZIMBABWE

MSUMBIJI

BOTSWANA

MADAGASKA

AFRIKA KUSINI

SENEGAL

GAMBIA

GUINEA-BISSAU

GUINEA

BURKINA FASO

BENIN

SIERRA LEONE

LIBERIA

CÔTE D’IVOIRE

GHANA

TOGO

GUINEA YA IKWETA

RWANDA

BURUNDI

SWAZILAND

LESOTHO

Fosse aux Lions

Hifadhi ya Asili

Hifadhi ya Wanyama Masai Mara

Mbuga ya Kitaifa ya Serengeti

Marromeu Delta

Mbuga ya Kitaifa ya Kruger

Bahari Mediterania

Bahari Nyekundu

Bahari ya Hindi

Maeneo Yanayotajw Katika Makala

Mbuga Kubwa za Kitaifa

[Sanduku katika ukurasa wa 9]

Sababu Inayofanya Pembe ya Kifaru Ipendwe Sana

“CHAPA ya Miguu Mitatu ya Maji ya Pembe ya Kifaru Yanayozuia Homa.” Hilo ndilo jina la dawa ipendwayo zaidi inayouzwa katika Malaysia, kulingana na waandikaji wa kitabu Rhino, Daryl na Sharna Balfour. Kibandiko cha hiyo isemwayo kuwa dawa ina ujumbe huu: “Dawa hii imetayarishwa kwa uangalifu kutoka kwa dawa bora zaidi zilizoteuliwa za Pembe za Kifaru Zinazozuia Homa, na chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Wastadi. Dawa hii ya ajabu huponya kimuujiza katika kutuliza mara hiyo wale wanaougua: Malaria, Joto Jingi, Homa inayoathiri Moyo na [Miguu na Mikono], Dhidi ya Kizunguzungu Kinacholetwa na Badiliko la Hewa, Kuruka Akili, Maumivu ya Meno, n.k.”—Italiki ni zetu.

Itikadi kama hizo zimeenea sana katika nchi za Esia. Pembe ya kifaru ikiwa katika hali ya umaji-maji au hali ya unga-unga hupatikana kwa urahisi katika majiji mengi ya Esia. Akitumaini kupinga kupendwa kwayo, akina Balfour wadai hivi: “Kumeza dawa ya pembe ya kifaru kuna thamani ya kitiba kama kule kutafuna makucha yako.”

Katika Yemeni, pembe ya kifaru huthaminiwa kwa sababu nyingine—kuwa kifaa kinachofanyiza kishikio cha jambia (kijisu chenye kupinda). Zaidi ya tani 22 ziliingizwa nchini humo katika kipindi cha mwongo wa miaka ya 1970, na ni vigumu kupata kitu kiwezacho kutumiwa cha badala. “Wayemeni,” waeleza akina Balfours, “wamepata kwamba hakuna kitu kizuri kuliko pembe ya kifaru katika hali ya kudumu na umaridadi. . . . Kwa kadiri [vishikio vya jambia] vinavyozeeka ndivyo vinavyoonekana maridadi zaidi, vikibadilika kuwa na rangi yenye ukungu inayofanana na rangi ya kimanjano.”

[Grafu/Picha katika ukurasa wa 8]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

2,720

1,000

1979 Idadi ya pundamilia 1990

55,000

3,696

1979 Idadi ya nyati 1990

1,770

260

1979 Idadi ya viboko 1990

45,000

4,480

1979 Idadi ya kuro 1990

Mielekeo Iliyolinganishwa ya idadi za wanyama wa pori za 1979 na 1990 katika Marromeu Delta

[Hisani]

Chini kushoto: Safari-Zoo of Ramat-Gan, Tel Aviv

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki