Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 2/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoa Mimba—Si Suluhisho Lisilo na Madhara
    Amkeni!—2009
  • Je! Dini Hizi Zina Majibu?
    Amkeni!—1993
  • Je, Utoaji-Mimba—Ndio Suluhisho?
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 2/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Ubaguzi wa Rangi Katika mfululizo wenu “Je! Jamii Zote Zitapata Kuungana Wakati Wowote?” (Agosti 22, 1993), mnazungumzia ubaguzi wa rangi. Lakini mbona hamsemi zaidi? Je! si asili ya binadamu kutopendelea mtu aliye tofauti? Fikirieni ubaguzi uliopo kati ya mafundi wa mikono na wastadi wa kazi, kati ya wakazi wa mijini na wakazi wa mashambani, kati ya vijana na wazee-wazee. Sikuhizi kuna mwelekeo wa kutia chumvi ubaguzi wa rangi kwa sababu za kisiasa na sababu nyinginezo.

B. G., Ujerumani

Kuna aina nyinginezo za ubaguzi ambazo zimeenea, lakini mara nyingi hazijasababisha kuteseka, ukosefu wa haki na migawanyiko kama vile ubaguzi wa rangi umefanya. Kwa hiyo tuliona kuwa ni lazima tuandike juu ya suala hilo kwa wakati ufaao.—Mhariri.

Wimbo wa Ndege Nilimaliza kusoma makala “Wimbo wa Ndege—Je! Ni Sauti Nyingine Tu Iliyo Tamu?” (Juni 22, 1993) Nilisisimka sana kujua kwamba nyimbo tamu za ndege, ambazo huenda wengine waliamini kuwa ni sauti zilizo nzuri tu, kumbe zina maana fulani. Asanteni kwa kuchapisha makala zinazotuonyesha juu ya kazi za ajabu za uumbaji wa Yehova.

A. P. C., Brazili

Makala yenu ilizungumzia mwanasayansi fulani wa Uingereza aliyegundua kwamba chiru kadhaa walikuwa wameongeza sauti ya simu katika nyimbo zao. Mke wangu nami tulikuwa na ono kama hilo. Mwaka uliopita chiru kadhaa walijenga kiota chao karibu na benchi ya bustani yetu. Ili tusiwaogopeshe, tulikuwa tukipiga mbinja ya wimbo uleule ulio mfupi kila wakati tulipokuwa tukipita karibu na kiota chao. Katika masika ya wakati huu, chiru kadhaa walikuwa wakiimba ule wimbo tulioimba kwa kupiga mbinja mwaka uliopita!

K. M., Ujerumani

Utoaji-Mimba Nina umri wa miaka 14, na mfululizo wenu wa “Utoaji-Mimba—Kutunga na Kutungua Uhai” (Mei 22, 1993) ulinisaidia nielewe hata zaidi jinsi hilo lilivyo suala muhimu sana leo. Ulikazia kwamba ingawa kijusi huishi ndani ya mwanamke, utoaji-mimba hudhuru zaidi ya mwili wa mama tu. Kijusi huishi kuanzia wakati ule wa kutungwa—si kipande tu cha mnofu. Naonelea utoaji-mimba upigwe marufuku.

J. R. W., United States

Ingawa Maandiko yanashutumu waziwazi utoaji-mimba, “Amkeni!” si gazeti la kisiasa na haliungi mkono kikundi chochote kinachotaka utoaji-mimba upigwe marufuku. Badala ya hivyo, makala zetu zinakusudiwa kusaidia watu mmoja-mmoja watumie Neno la Mungu katika maisha zao.—Mhariri.

Watoto Walio na Mkazo wa Akili Ningependa kuwashukuru sana kwa mfululizo wa makala “Watoto Walio na Mkazo wa Akili—Wanaweza Kusaidiwaje?” (Julai 22, 1993) Uliniandalia ujumbe wenye mafaa wa kutusaidia sisi wazazi kuelewa jinsi tunaweza kusababisha mikazo mingi sana kwa watoto wetu kwa sababu ya kutojua habari za mikazo ya akili.

M. L. S., Italia

Ulimwengu umekuwa mahali ambapo hata watoto huugua mkazo wa akili. Nilikuwa nikishuka moyo sana kwa sababu ya majina mabaya ambayo wazazi wangu walikuwa wakiniita nilipokuwa nikifanya mambo polepole. Yaliniumiza sana. Naweza kuona kutokana na makala hizo kwamba wazazi hufanyiza utu wa watoto wao kutoka wakati wa kuzaliwa. Iwapo nitakuwa mzazi, nataka niwe mwenye hisia mwenzi na kusababu pamoja na watoto wangu.

N. K., Japani

Makala hizo zilinigusa moyo sana. Nilitendwa vibaya na mama yangu. Makala hizo zilinisaidia kuelewa sababu inayonifanya niitikie mambo fulani kwa njia fulani na sababu inayonifanya nijihisi mara nyingi kuwa asiyefaa kitu na kukosa kujitumaini. Mlinisaidia sana kumtumaini Yehova. Uchungu wa kihisia-moyo bado waumiza, lakini najua kwamba ameahidi kufuta kumbukumbu hizo mbaya kutoka moyoni na akilini. Jambo hilo lanifariji sana.

E. B., Uingereza

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki