Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 11/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoa Mimba—Si Suluhisho Lisilo na Madhara
    Amkeni!—2009
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Je! Dini Hizi Zina Majibu?
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 11/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Utoaji-Mimba Mfululizo wenu “Utoaji-Mimba—Kutunga na Kutungua Uhai” (Mei 22, 1993) ulinitoa machozi machoni pangu na kunitia uchungu moyoni mwangu. Kama ningalisoma habari hiyo miaka minane iliyopita, nisingalitoa mimba yangu. Ilinichukua karibu miaka saba kutubu dhambi hiyo kwa mume wangu, ambaye angalikuwa baba yacho. Natumaini kwamba mtu yeyote anayefikiria kutoa mimba atasoma makala hizo na kutambua kwamba uhai ni zawadi yenye thamani kutoka kwa Mungu.

G. D., United States

Nina umri wa miaka 16, na tulijifunza juu ya utoaji-mimba shuleni. Lakini, kwa njia fulani sikuwa nimetambua ule uchungu unaompata mtoto. Nilipokuwa nikisoma gazeti hilo, nilikasirika sana, na machozi ambayo nisingeweza kuzuia yakanitiririka. Watu wanaweza kuuonaje kijuujuu tu uhai wenye thamani ambao Yehova hutoa kwa fadhili?

N. K., Japani

Nilipeleka gazeti hilo shuleni, na nilishangaa sana kwamba wanafunzi walilipenda! Liligusa sana mioyo ya wanadarasa wenzangu kufikia hatua ya kwamba mmoja wao akashindwa na kuanza kulia. Siku chache tu kabla ya siku hiyo, alikuwa ametoa mimba.

L. S., United States

Helikopta Makala yenu “Mfanyakazi Mwenye Bidii wa Angani” (Machi 8, 1993) ilinipendeza sana. Nikiwa mkaguzi wa usalama angani wa Usimamizi wa Serikali wa Angani na mfunzi wa rubani na mwendo wa helikopta, naweza kuona kwamba makala hiyo ni sahihi kabisa kwa njia ya kutokeza sana. Nathamini hasa njia sahili iliyotolewa.

J. R., United States

Kupunguza Uzito Nilisoma makala “Ikiwa Mimi Nilipunguza Uzito, Yeyote Aweza!” (Januari 22, 1993), na ingawa ninafurahi sana kwamba mwandikaji anashinda vita yake dhidi ya uzito wake, nahofu kwamba makala hiyo itatia watu wengi moyo kufikiri kwamba watu wenye uzito kupita kiasi wanahitaji tu kujidhibiti na kula kwa uangalifu. Tatizo langu ni kubwa zaidi kuweza kusuluhishwa na ulaji wa “kalori 1,200 hadi 1,500 kila siku.” Ni sharti nile, ni dawa. Ni hivi majuzi tu nilipokuja kutambua kwamba nikiwa mtoto aliye mtu mzima, wa mzoelevu wa kileo, nimekuwa nikijaribu kujaza hamu ya kutaka kupendwa na kujistahi. Basi, ulaji wenye uangalifu sana si suluhisho rahisi kwa suala hilo gumu.

R. S., United States

Twathamini maelezo yako manyoofu. Hata hivyo, kwa msingi makala hiyo ilielekezwa kwa watu wenye mazoea ya ulaji usiofaa, si kwa wale wanaopambana na matatizo mazito ya ulaji. Hawa wenye matatizo mazito waweza kuhitaji msaada wa kitiba ili washinde matatizo yao. Habari zenye msaada juu ya matatizo ya ulaji yalichapishwa katika toleo letu la Februari 22, 1992, Kiingereza.—Mhariri.

Makala hiyo ilikuwa kama historia ya mazoea yangu mabaya ya ulaji. Madokezo hayo yalikuwa yenye mafaa sana, na ninayatumia sasa hivi. Asanteni sana kwa ajili ya makala hiyo!

S. P., Brazili

Makala hiyo ilinifundisha jinsi ya kusawazisha mazoea yangu ya ulaji kwa njia yenye afya. Hilo ndilo jambo nililohitaji. Asanteni sana!

S. G., United States

Farasi Niliguswa moyo na makala “Farasi Walikuwa Maisha Yangu.” (Mei 22, 1993) Kabla ya kuwa Mkristo, nilitoa karibu wakati wangu wote wa ziada katika kupanda na kutunza farasi. Hata hivyo, baada ya kujifunza Biblia, niliacha mapendezi hayo yangu yenye Kugharimu sana na kuanza kazi ya utumishi wa wakati wote. Hata hivyo bado nawapenda farasi. Makala hiyo ilinisaidia nijue kwamba wengine wamepata hisia izo hizo.

G. V., Ujerumani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki