Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 5/8 kur. 3-4
  • Wakati Utoto Uletapo Kumbukumbu Baya Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wakati Utoto Uletapo Kumbukumbu Baya Sana
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kulea Watoto tangu Uchanga
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
  • Jitihada za Kuwaokoa Watoto
    Amkeni!—1994
  • Sababu Inayofanya Watoto Wawe Wapiganaji Bora
    Amkeni!—1997
  • Zoeza Mtoto Wako Tangu Utoto Mchanga Sana
    Siri ya Furaha ya Familia
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 5/8 kur. 3-4

Wakati Utoto Uletapo Kumbukumbu Baya Sana

NA MLETA-HABARI ZA AMKENI! KATIKA UHISPANIA

Leo—siku iliyo kama nyingineyo ya miaka ya 1990—watoto 200 elfu watapigana katika vita vya kiharamia,[1] watoto 100 milioni wa umri wa kwenda shule hawataenda shuleni,[2] watoto 150 milioni wataenda kulala njaa,[3] watoto 30 milioni watalala barabarani,[4] na watoto 40 elfu watakufa.[5]

IKIWA tarakimu zilizo juu zaonekana kuwa za kuogopesha, nyuso zinazowakilishwa na tarakimu hizo zinavunja moyo kabisa. Hapa chini zipo hadithi fupi za watoto watano ambao shida zao kubwa zatusaidia kuelewa idadi hizo zilivyo za kusikitisha.

Askari-jeshi mtoto. Mohammad ana miaka 13 tu, lakini tayari amekolea akiwa askari-jeshi katika Asia ya kusini-magharibi, mzee-wa-kazi aliyepigana mapigano saba. Alikuwa akichunga mbuzi kabla hajaenda vitani—akiwa na miaka kumi. Sasa, Mohammad hubeba bunduki nyepesi ya mashambulizi aina ya AK-47, ambayo yeye hasiti kuitumia. Katika kipigano kimoja aliua askari-jeshi wawili maadui akiwa karibu. Alipoulizwa alivyohisi juu ya kuua, alijibu hivi: “Nilifurahi kwa sababu niliwaua.” Watoto huwa askari-jeshi wazuri zaidi, ofisa wake aeleza, “kwa sababu hawaogopi.”[6]

Mfanyakazi mtoto. Woodcaby wa miaka minne huishi katika nyumba ambayo ni shimo lililojengwa kwa saruji na makaa-mawe yaliyounguzwa katika kisiwa kimoja cha Karibea. Yeye huamka saa 12 asubuhi kufanya kazi zake za nyumbani: kupika, kuteka maji, na kusafisha nyumba ya bwana-mkubwa wake. Hapati mshahara na labda hataenda shuleni kamwe. Woodcaby asema kwamba asikitika kutokuwa pamoja na wazazi wake, lakini hajui waliko. Siku yake humalizika saa 3:30 usiku, na mambo yakimwendea vema, haendi kulala njaa.[7]

Mtoto mwenye njaa. Katika kijiji cha Comosawha cha Afrika, msichana wa miaka 11 hushinda mchana kutwa kila siku akinyong’onyea kwa uchovu wa kupekua akitafuta magugu ya kung’oa. Vile vitufe vya gugu-kitunguu—karibu vyote vile viwezavyo kukua katika udongo uliokaushwa na joto—hutumika kumwendeleza yeye na familia yao wakiwa hai. Vitufe hivyo huchemshwa au kutwangwa kisha kukaangwa. Mchanganyiko hatari wa ukavu na vita ya wenyewe kwa wenyewe umefanya wanakijiji wakaribie kufa njaa.[8]

Mtoto wa barabarani. Edison ni mmoja tu wa maelfu ya watoto wa barabarani katika jiji moja kubwa la Amerika Kusini. Yeye hupata fedha kwa kung’arisha viatu, naye hulala kando ya barabara karibu na kituo cha mabasi, pamoja na watoto wengine ambao hukunjamana kwa kusogeleana wakati wa baridi nyakati za usiku. Nyakati fulani yeye hujisaidia kwa kufanya uhalifu mdogomdogo ili kuongezea mapato yake akiwa mvulana-mng’arisha-viatu. Amepigwa mara mbili na polisi, na ametumia miezi mitatu katika jela. Edison husisitiza kwamba sasa “ni kama” ameacha kutumia dawa za kulevya na kunusanusa gundi. Ana ndoto ya kuwa mekanika, ya kujifunza kazi yenye mapato.[9]

Kifo cha mtoto. Ni asubuhi yenye baridi na unyevunyevu juu ya mlima Dugen katika Mashariki ya Kati. Kitoto kichanga, kilichofungwafungwa kwa nguo ya maziko, kimewekwa katika kaburi lisilo la kina kirefu. Mtoto mchanga huyo alikufa kwa ugonjwa wa kuhara—kisababishi cha kawaida cha kufa kwa vitoto vichanga. Mama ni mkimbizi na maziwa yake yalikauka katika ile safari ngumu ya kuchosha ya kwenda kutafuta usalama. Kwa kukata tamaa alilisha mtoto wake sukari na maji, lakini maji hayo yalikuwa yameambukizwa, basi mtoto mchanga huyo akafa. Yeye, kama watoto wengine 25,000 waliozikwa siku hiyohiyo, hakufaulu kutimiza mwaka mmoja.[10]

Visa hivyo vyenye misiba vikizidishwa mara elfu nyingi, vyaonyesha jinsi maisha yalivyo kwa wengi wa watoto wa ulimwengu. Utoto, ambao ni wakati wa kujifunza na kukomaa katika hifadhi ya familia yenye upendo, umekuwa wakati mbaya sana kwa watoto hao ambao wengi wao hawawezi kamwe kutazamia kuuponyoka.

Peter Adamson, mhariri wa ripoti iitwayo The State of the World’s Children (Hali ya Watoto wa Ulimwengu), alitangaza hivi katika 1990: “Kifo na mateso kwa kadiri hiyo si mambo ya lazima tena; kwa hiyo hayakubaliki tena. Ni lazima wajibu wa kujali maadili utimizwe kwa kuondoa hali hizo.”[11]

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Picha: Godo-Foto

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki