Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 5/22 uku. 21
  • Je! Biblia Husema Yasiyopatana na Hali?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Biblia Husema Yasiyopatana na Hali?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Hata Hivyo, Mambo ya Hakika Ni Nini?
  • Sayansi: Je! Imethibitisha Biblia Kuwa Yenye Makosa?
    Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu?
  • Je, Kitabu Hiki Chaafikiana Na Sayansi?
    Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
  • Chanzo Kisicho na Kifani cha Hekima Bora
    Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai?
  • Je! Wameithibitisha Biblia Kuwa Bandia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 5/22 uku. 21

Je! Biblia Husema Yasiyopatana na Hali?

WENGI hujibu ndiyo na kusema: “Haipatani na sayansi. Ni hadithi na ngano tu. Ni ya kikale. Haitumiki kuhusu hali. Waamini wanaishi katika ulimwengu wa ndoto.”

Hata Hivyo, Mambo ya Hakika Ni Nini?

•Biblia husema kwamba uhai uliumbwa na Mungu. Sayansi husema kwamba uhai ulipata asili kupitia mchanganyiko wa kemikali na nishati uliotokea kwa nasibu. The World Book Encyclopedia husema hivi: “Pasteur alionyesha kwamba uhai hauwezi kutokea wenyewe tu.”[1] Kitabu Evolution: A Theory in Crisis cha mwanabiolojia Michael Denton husema hivi: “Kati ya chembe iliyo hai na mfumo usio wa kibiolojia wenye utaratibu wa hali ya juu zaidi, . . . kuna bonde la mweneo mkubwa sana na la utenganisho kamili kwa kadiri iwezekanayo kuwaziwa.”[2] Hakuna mwanamageuzi awezaye kudokeza njia yoyote timamu kisayansi ya kwamba uhai ungeweza kutokea wenyewe tu.

• Mageuzi husema kwamba chembe hii ya asili iligeuka-geuka ikawa viumbe vyote vilivyo hai duniani. Kumbukumbu la mabaki ya kale ya viumbe (visukuku) halionyeshi kamwe kamwe mgeuko-geuko huo ambamo aina ya familia moja huwa nyingine. Mwanasayansi Francis Hitching katika kitabu chake The Neck of the Giraffe aandika hivi: “Wakati utafutapo madaraja kati ya vikundi vikubwa-vikubwa vya wanyama, huyapati kamwe.”[3] Hii hupatana na lile Biblia isemalo—kwamba familia huzaa upya “kwa jinsi yake.”—Mwanzo 1:12, 25.

• Katika visa vingi akiolojia huthibitisha kwamba masimulizi ya historia ya Biblia ni ya kweli.[4]

• Wakale walifikiri kwamba dunia ilitegemezwa katika anga na vitu vya ajabu-ajabu vya namna zote. Isaac Newton ndiye aliyeonyesha kisayansi kwamba dunia ilielea angani bila kuegemea chochote kwa sheria za mwendo na nguvu ya uvutano.[5] Biblia ilionyesha hilo karibu miaka 3,200 mapema zaidi, ikiandika kwenye Ayubu 26:7 kwamba Mungu alikuwa ‘akiutundika ulimwengu pasipo kitu.’

• The Encyclopedia Americana husema: “Wazo la dunia iliyo tufe halikukubaliwa mahali pengi mpaka wakati wa kile Kipindi cha Mwerevuko,”[6] lakini katika karne ya nane K.W.K., Biblia ilisema hivi juu ya Mungu: “Yeye huketi juu ya dunia iliyo mviringo.”—Isaya 40:22, Moffatt.

• Sheria ya Kimusa (karne ya 16 K.W.K.) ilionyesha utambuzi wa viini vya ugonjwa vyenye kuambukiza maelfu ya miaka kabla ya Pasteur kuhusianisha viini na ugonjwa.—Mambo ya Walawi, sura 13, 14.

• Miaka elfu moja kabla ya Kristo, Sulemani aliandika kwa usemi wa kitamathali juu ya kuzunguka kwa damu, lakini sayansi ya kitiba ililazimika kungoja mpaka William Harvey alipoeleza hilo katika karne ya 17 W.K.—Mhubiri 12:6.[7]

• Sulemani aliandika juu ya chungu waliokuwa na ghala za chini ya ardhi ambako waliweka akiba ya mbegu za kuwaendeleza hadi majira ya baridi yapite. (Mithali 6:6-8) Wachambuzi wa Biblia walisema hakukuwa na chungu wa jinsi hiyo. Hata hivyo, katika 1871, mchunguzi Mwingereza wa vitu vya asili alivumbua chungu hao na ghala zao.[8]

• Zaburi 139:16 ilionyesha ujuzi wa msimbo-jeni (tabia za urithi): “Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia.”

• Katika karne ya saba K.W.K.,[9] kabla wanasayansi hawajatambua uhamaji wa ndege, Biblia kwenye Yeremia 8:7 ilifunua hivi: “Koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao.”

• Katika karne ya kwanza W.K., Biblia ilitabiri kwamba katika “siku za mwisho,” watu wangekuwa wakiharibu mazingira ya dunia, na kwa sababu ya hilo, Mungu ‘angewaangamiza wale wanaoangamiza dunia.’—2 Timotheo 3:1; Ufunuo 11:18, HNWW.

• Eti Biblia haitumiki kuhusu hali? Hiyo ndiyo yenye hekima itumikayo zaidi ya zote kwa ajili ya nyakati hizi zenye hatari, lakini ni lazima watu watumie hiari yao kuifuata ndipo waweze kunufaika. ‘Fueni panga zenu ziwe majembe na mikuki yenu iwe miundu.’ ‘Tendeeni wengine vile mtakavyo wawatendee nyinyi.’ Penda jirani yako kama ujipendavyo mwenyewe. Wale wafuatao miongozo hiyo hawaanzishi vita vyovyote, hawatendi uhalifu wowote. Wakati watu duniani watakapokuwa watiifu kwa utawala wa Ufalme wa Mungu ukiwa mikononi mwa Kristo Yesu, hapo ndipo tumaini la mwamini wa Biblia litakapothibitika kuwa, si ndoto isiyowezekana, bali uhalisi wenye kutumika.—Mika 4:2-4; Mathayo 7:12; Ufunuo 21:3-5.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 21]

Kwa hisani ya Shrine of the Book, Israel Museum, Jerusalem

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki