Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 7/22 kur. 15-18
  • Matetemeko ya Dunia—ya California Lile Kubwa Litatokea Lini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matetemeko ya Dunia—ya California Lile Kubwa Litatokea Lini?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • San Francisco
  • Tetemeko la Landers
  • Los Angeles
  • Je! Tetemeko Kubwa la Pili Litatukia?
  • Miatuko ya Dunia Iliyofichika
    Amkeni!—1996
  • Matetemeko Makubwa Zaidi Yanatazamiwa
    Amkeni!—2010
  • Tetemeko la Ardhi
    Amkeni!—2002
  • Msiba wa Ghafula wa Japani—Jinsi Watu Walivyoukabili
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 7/22 kur. 15-18

Matetemeko ya Dunia—ya California Lile Kubwa Litatokea Lini?

ARDHI iliyumbayumba. Mifereji ya gesi ikavunjika. Majengo yakaporomoka. Mioto ikawaka. Je! hilo lilikuwa tetemeko la dunia la hivi karibuni la Los Angeles? La. Lilikuwa tetemeko lililokumba San Francisco mnamo Aprili 18, 1906. Tetemeko hilo, na moto wa siku tatu uliofuata, liliharibu maeneo 512 yenye majengo katikati mwa mji, na kuua watu 700 hivi.[1]

Ni nini husababisha maafa hayo?

Wanasayansi hujaribu kueleza kwa kutumia nadharia ya mabamba yanayopitana kwa kuteleza. Wao husema kwamba ganda la dunia limo juu ya mabamba au tabaka 20 hivi za miamba zilizo imara, zinazosogea polepole, zikiteleza na kupitana na nyakati nyingine zikipitana moja juu ya nyingine.[2] Bamba la Pasifiki huteleza polepole kuelekea kaskazini, likipita bamba la Amerika ya Kaskazini. Eneo la kuteleza kati ya mabamba hayo mawili huitwa Ufa wa San Andreas.[3] Hilo huenea kuelekea kaskazini kwa kilometa 1046 hivi, kutoka mwanzo wa Ghuba ya California, ukitoweka katika Bahari Pasifiki karibu na San Francisco.[3a]

Mabamba hayo husogea polepole sana,[4] kwa kadiri ile ambayo kucha za vidole vya mikono hukua—sentimeta chache kwa mwaka.[5] Baada ya miaka mingi, mkazo huongezeka wakati mabamba yanapokwama yakijaribu kuteleza ili yapitane. Halafu hayo yaweza kuachana kwa mlipuko mkubwa.[6]

Ufa wa San Andreas hupita kilometa 53 kaskazini-mashariki mwa Los Angeles na kufika hadi Bahari Pasifiki karibu na San Francisco.[7] Je! ni ajabu kwamba Watu wa California wana wasiwasi juu ya lile liitwalo eti Tetemeko Kubwa?

San Francisco

Baada ya tetemeko la 1906, ncha ya kaskazini ya Ufa wa San Andreas iliendelea kuwa tulivu kwa kadiri fulani. Halafu, saa 11:04 jioni mnamo Oktoba 17, 1989,[9] Wamarekani milioni 50 hivi[10] walikuwa wakitazama televisheni ili kutazama Mchuano wa Ligi ya besiboli kutoka San Francisco. Ghafula, kamera zikaanza kuruka juu-chini. Kilometa 100 hivi kusini mwa San Francisco,[11] zile pande mbili za Ufa wa San Andreas zilikuwa zimepitana kasi, zikisababisha tetemeko lililoua watu 63, zikavunja barabara kuu, zikaponda magari, na kuacha maelfu bila makao.[12] Lakini tetemeko hilo lilikuwa dogo zaidi ya lile lililotabiriwa lenye ukubwa wa kipimo 8 la lile Tetemeko Kubwa.a[12a]

Huko nyuma katika masika ya 1985, Uchunguzi wa Kijiolojia wa Marekani ulitabiri kwamba tetemeko lenye ukubwa wa kipimo 6 lingetukia katika kipindi cha miaka mitano ya 1988 karibu na mji mdogo wa Parkfield, karibu katikati ya Los Angeles na San Francisco.[13] Kwa kuchunguza kusogea kwa ardhi kabla ya tetemeko hilo lililotazamiwa, walitumaini kujifunza jinsi ya kutabiri matetemeko ya dunia na kuweza kutoa onyo labda saa au hata masiku kabla ya tetemeko kutukia. Uchunguzi huo uligharimu dola milioni 15,[14] lakini tetemeko halikutukia. Kama vile William Ellsworth wa Uchunguzi wa Kijiolojia wa Marekani alivyosema wakati mmoja, “ufafanuzi juu ya kutukia kwa matetemeko ni sayansi isiyo halisi.”[15]

Tetemeko la Landers

Hivyo, mnamo Juni 28, 1992, hakuna mtu aliyetazamia tetemeko lenye ukubwa wa kipimo 7.5 litukie katika eneo lisilo na watu wengi karibu na Landers, katika Jangwa la Mojave la California kusini. Kuhusu tetemeko hilo, gazeti Time lilisema: “Katika sekunde chache zenye kuogofya, liligeuza barabara kwingineko, likahamisha maegesho na kubadili mandhari ya eneo hilo kwa njia nyingi zisizotazamiwa, na kimuujiza zikiua mtu mmoja tu.” Kwa tetemeko la ukubwa huo, uharibifu ulikuwa mdogo.[16]

Kwa hiyo hilo pia halikuwa lile Tetemeko Kubwa. Kwa kweli, halikutukia kwenye ule Ufa wa San Andreas bali kwenye mojawapo zile nyufa ndogo zaidi zinazouzunguka.[17]

Hata hivyo, yawezekana kwamba tetemeko la Landers, kutia na lile dogo zaidi katika Ziwa la Big Bear lililo karibu, yaliamsha sehemu za karibu za Ufa wa San Andreas.[18] Wanasayansi wamesema yale mabamba yaliyokwama ambayo yako sehemu ya kusini zaidi ya San Andreas yana uwezekano wa asilimia 40 wa kufyatuka ghafula na kuachana katika kipindi cha miaka 30 ijayo. Hilo laweza kutokeza lile Tetemeko Kubwa lililoogopewa kwa muda mrefu, lenye ukubwa wa kipimo 8 likiwa na nguvu mara tano ya lile lililotukia Landers.[18a]

Los Angeles

Halafu, mnamo Januari 17 ya mwaka huu, Los Angeles ilipata tetemeko saa 10:31 usiku.[19] Kilometa 18 hivi chini ya ardhi ya Bonde la San Fernando lenye watu wengi katika Los Angeles, yafikiriwa kwamba sehemu ya mwamba iliteleza meta 5.5 katika ufa wenye kina kikubwa.[19a] Tetemeko hilo la sekunde kumi lenye ukubwa wa kipimo 6.6 liliua angalau watu 57.[19b] Kwa msiba, watu 16 walikufa katika jengo moja la makao lililoporomoka.[20] Mtu mmoja aliyeokoka alikwama kwa saa nane chini ya tani 20 za saruji za jengo la maegesho lililoanguka.[21] Kuvunjika kwa barabara kuu kulikatiza njia kuu ya jiji kuelekea kaskazini.[22] Makanisa, shule, maduka, na hospitali moja kubwa zilifungwa.[23] Kama ilivyo kawaida, familia za mapato ya chini ziliteseka zaidi, kwa sababu ya kuishi katika majengo ya zamani zaidi yaliyokuwa yamejengwa kabla ya kuanzishwa kwa kanuni za kisasa za ujenzi ili kuhimili tetemeko.[24]

Tetemeko hilo lilionyesha matatizo yawezayo kutokea kwa habari ya hata nyufa ndogo zaidi za mahali hapo zilizo chini ya jiji kubwa. Kwa habari ya watu, kwao tetemeko la dunia lolote ni lile Tetemeko Kubwa ikiwa wanaishi juu ya kiini cha tetemeko!

Uharibifu ungalikuwa mkubwa zaidi kama kusingekuwa zile kanuni imara za ujenzi za mahali hapo.[25] Kila tetemeko la dunia hutoa mafunzo ambayo yaweza kufanya mambo yawe rahisi zaidi wakati ujao. Baadhi ya barabara kuu zinazopitana moja chini ya nyingine zilizokuwa zimeimarishwa baada ya matetemeko ya hapo awali ziliokoka tetemeko hilo; nyingine hazikuokoka. Lakini mtihani halisi utakuja ikiwa tetemeko la dunia kubwa zaidi—tetemeko kubwa kwelikweli—latukia karibu na jiji kubwa. Labda tena Los Angeles?

Je! Tetemeko Kubwa la Pili Litatukia?

‘Ah, La! Lingine lisitukie! Lingine moja litakuwa limetuweza!’ Hata hivyo, wanajiolojia fulani wanafikiri kwamba lingine kubwa litatukia karibuni. Gazeti New Scientist la Januari 22, 1994, lilisema: “Miatuko ya ufa iliyo hatari chini ya Los Angeles ingeweza kusababisha ‘Tetemeko Kubwa’ lenye uharibifu kama tu lile linalotazamiwa kwenye ufa wa San Andreas, ndivyo wataalamu wanavyoonya. . . . Bonde la Los Angeles lina miatuko ya mlazo, kwa sababu ufa wa San Andreas—ambao katika mahali pengi hutoka kaskazini hadi kusini katika nchi hiyo—hupinda kuelekea magharibi katika Los Angeles, ukisababisha mkazo wa ziada sehemu hiyo. Kwa njia fulani, ni lazima lile bara linalohama la bamba la Pasifiki lipite pindo hilo na kuendelea kusonga kaskazini.”

Wanajiolojia wafikiri kwamba bamba la Pasifiki liliposogea, mfumo wa nyufa za mlazo ulifanyizwa katika bonde la Los Angeles, mojawapo ukisababisha tetemeko lililotukia huko mapema mwaka huu. Kuhusu tetemeko hilo gazeti New Scientist liliendeleza ripoti yalo ya kwanza kwa hii nyingine juma moja baadaye: “Wanasayansi wangali waamini kwamba ufa uliosababisha [tetemeko] ni ufa wa mlazo—ambapo tabaka la mwamba huteleza juu ya lingine. Wakati wa tetemeko la juma lililopita, Milima ya Santa Susana kaskazini mwa kiini cha tetemeko iliinuliwa angalau sentimeta 40 na wakati uo huo ikasogea sentimeta 15, kwenda kaskazini.”

Kerry Sieh, mwanajiolojia kutoka Caltech, aonelea kwamba zile nyufa ndogondogo za mlazo zinazopitana-pitana katika nyanda ya Los Angeles zingeweza kuwa hatari kama vile lile tetemeko ambalo lingali latazamiwa la ukubwa wa kipimo 8 la San Andreas. Kisha Sieh auliza hivi akiwaza kuhusu Los Angeles: “Je! yawezekana kwamba tungeweza kupata tetemeko kubwa kwelikweli, la ukubwa wa kipimo 8, kiini cha tetemeko kikiwa Los Angeles?” Hilo ni swali lenye kuogofya, ukifikiria mamilioni ya watu waishio humo!

Watu wa California waonekana kana kwamba huishi na matetemeko ya dunia, kama vile watu wengine huishi na vimbunga, mafuriko, au tufani.[28]

[Maelezo ya Chini]

a “Ukubwa” hurejezea kipimio cha kadiri ya badiliko. Kipimio hicho huwekwa moja kwa moja kwenye mwatuko wa mwamba ndani ya ufa. Kipimio cha Richter hupima kadiri ya mawimbi ya tetemeko na kwa hiyo hicho si kipimio cha moja kwa moja cha ukubwa wa tetemeko. Mara nyingi vipimio hivyo viwili huonyesha matokeo yaleyale kwa matetemeko mengi, ingawa kipimio cha kadiri ya badiliko huwa sahihi zaidi.

[Ramani katika ukurasa wa 16]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Miatuko ya ufa wa mlazo katika bonde la Los Angeles

Ufa wa San Andreas

Los Angeles

BAHARI PASIFIKI

[Picha katika ukurasa wa 15]

Uharibifu wa barabara kuu ulioletwa na tetemeko la Los Angeles la 1994

[Hisani]

Hans Gutknecht/Los Angeles Daily News

[Picha katika ukurasa wa 17]

Mioto ikiwaka kutoka mfereji wa gesi uliovunjwa na tetemeko la 1994

[Hisani]

Tina Gerson/Los Angeles Daily News

[Picha katika ukurasa wa 18]

Sehemu hii iliyoporomoka ya barabara kuu ya Los Angeles ilisababishwa na tetemeko la sekunde kumi la ukubwa wa kipimo 6.6

[Hisani]

Gene Blevins/Los Angeles Daily News

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki