Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 8/22 kur. 3-4
  • Kurudi Shuleni kwa Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kurudi Shuleni kwa Nini?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Kuna Tatizo Hilo?
  • Je! Ufuatilie Masomo Zaidi au La?
    Amkeni!—1994
  • Elimu Yenye Kusudi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Wazazi, Mnataka Watoto Wenu Wawe na Maisha ya Aina Gani Wakati Ujao?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Je, Biblia Inapinga Elimu?
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 8/22 kur. 3-4

Kurudi Shuleni kwa Nini?

HALI ya Robert ya kutafuta kazi ilikuwa ono lenye kumfadhaisha sana iliyomchukua muda wa miaka mitatu mirefu. Hatimaye, akiwa na umri wa miaka 21, aliandikwa kazi akiwa mshauri katika kambi moja ya tafrija ya kipindi cha kiangazi. Ingawa kwa kiasi fulani sasa amepata faraja kidogo, Robert alikuwa amechoshwa na hali ngumu ya kutafuta kazi. “Wazazi wetu hawaelewi kabisa,” yeye asema. “Ni vigumu zaidi kupata kazi siku hizi.”

Kama ilivyo na Robert, vijana wengi waliohitimu kutoka shule huanza kazi kila mwaka. Wao huwa na matumaini. Wao huwa na mipango. Lakini idadi inayoongezeka wanapata kwamba hawawezi kupata aina ya kazi waliotazamia.

Kwa hiyo, wengi wanaongeza elimu yao.a “Ikiwa miaka ya Sabini ilitoa ishara zilizotokeza mwelekeo usiofaa dhidi ya manufaa za elimu,” lasema gazeti Fortune, “miaka ya Themanini ilitokeza ishara za mwelekeo tofauti: Pata digrii ama sivyo uone cha mtemakuni.”

Kwa Nini Kuna Tatizo Hilo?

Kwa nini elimu ya ziada mara nyingi huhitajika? Kwanza, hesabu kubwa ya kazi leo huhitaji ustadi wa hali ya juu. “Karani wa benki ambaye alikuwa tu anapokea fedha za kuwekwa akiba ameondolewa kazi na mashine za fedha,” asema mwakilishi wa Wizara ya Wafanyakazi ya Marekani. “Sasa ni lazima [karani huyo] awe na uwezo wa kuniambia aina tatu za akiba za hisa na anieleze ni kwa nini nahitaji aina hii kuliko aina ile.” William D. Ford, ambaye ni msimamizi wa Elimu ya Bunge na Halmashauri ya Wafanya kazi, asema: “Zile kazi rahisi hazipo tena.”

Pili, watu fulani wahisi kwamba shule haziwapi wanafunzi elimu ya kutosha. Wao wasema kwamba ule mkazo unaotiliwa masuala kama matumizi ya dawa za kulevya, UKIMWI, na kudhibiti uzazi wapita ufundishaji wa kusoma, kuandika, na hesabu. Dakt. Robert Appleton, ambaye amekuwa mwalimu kwa miaka 27, aomboleza kwamba mfumo wa shule waonekana kuwa umekuwa “mahali pa utendaji wa kijamii” unaolemewa na mzigo wa “kushughulikia matatizo ambayo zamani hayakuonwa kuwa yanahusu mambo ya shule.”

Kwa sababu ya baadhi ya shule kukosa kufundisha watoto stadi zinazohitajika, wahitimu wengi wa shule za sekondari hawawezi kujitegemeza kifedha. “Hawajafundishwa kufanya kazi,” asema Joseph W. Schroeder, meneja wa ofisi ya Utumishi wa Kazi wa Florida. “Waajiri-kazi wanaposhughulika na vijana, tatizo ambalo wengi wao huniambia kila wakati ni kwamba [vijana] hao hawawezi kusoma wala kuandika vizuri. Wao hawawezi kujaza fomu ya kutaka kazi.”

Sababu ya tatu inayoweza kufanya elimu ya ziada ihitajike ni kwamba katika nchi nyingi kuna wahitimu wengi kupita kiasi wa vyuo. “Wahitimu wa vyuo ni wengi kuliko kazi zinazohitaji stadi zao,” lasema The New York Times. “Kwa sababu ya kuwapo kwa wingi huo wa kupita kiasi,” ripoti hiyo yaongezea, “waajiri-kazi hawapendelei kujasiria kuajiri wahitimu wa shule za sekondari.”

Ili wafaulu kupata aina ya kazi inayohitajika ili wajitegemeze wenyewe ifaavyo, wengi wanarudi shuleni. Katika Marekani, asilimia 59 huendelea na elimu baada ya shule ya sekondari. Hilo ni ongezeko kubwa kupita ile asilimia 50 ambayo ilikuwa imedumu kwa miongo mingi.

Miendo kama hiyo yaonwa katika nchi nyinginezo vilevile. Kwa kielelezo, tangu miaka ya 1960, Uingereza imekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi wanaopokea elimu baada ya kumaliza masomo kwa kiwango kinachotakikana na sheria. Katika mwaka mmoja wa karibuni, asilimia 85 ya wale waliomaliza shule ya sekondari katika Australia walitoa maombi ya kwenda vyuo vikuu na vyuo mbalimbali. Karibu asilimia 95 ya wanafunzi wa Japani hufanya mtihani ili kuendelea na elimu kwa miaka mitatu, ambako watatayarishwa kwa ajili ya kazi au kwa ajili ya kwenda chuo.

Hata hivyo, elimu ya ziada haitokezi nyakati zote mafaa yanayotakikana. Faida zayo na hasara ni zipi?

[Maelezo ya Chini]

a Majina ya viwango vya masomo hutofautiana nchi hadi nchi. Katika makala hizi “shule ya sekondari” yawakilisha masomo yote ambayo ni ya lazima kisheria. “Chuo,” “chuo kikuu,” na “shule za kiufundi,” zarejezea aina mbalimbali za elimu ya ziada ambayo haishurutishwi na sheria lakini yanayofuatiliwa tu kwa hiari.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki