Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 9/8 kur. 11-13
  • Je! Umepata Kujiuliza?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Umepata Kujiuliza?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Umepata Kujiuliza? Majibu ya Biblia
  • Yesu Kristo Mwana Mpendwa wa Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Ule “Utatu Uliobarikiwa”—je! Umo Katika Biblia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Mungu ni Nani?
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
  • Utatu—Je! Hufundishwa Katika Biblia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 9/8 kur. 11-13

Je! Umepata Kujiuliza?

NI NINI kimojapo vikwazo vitenganishavyo Waislamu na Wayahudi na dini za Jumuiya ya Wakristo? Ni fundisho la “Utatu Ulio Mtakatifu Sana.” Kanuni hiyo ya kikanisa hutaarifu nini? Utatu ulifasiliwa katika Imani ya Athanasio kuwa ibada ya “Mungu mmoja katika Utatu . . . Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu, na Roho Mtakatifu ni Mungu; na bado wao si miungu watatu, bali Mungu mmoja.”[1] Kila mmoja husemwa kuwa wa milele, kuwa mweza-yote, bila mkubwa wala mdogo kuliko mwingine; kila mmoja akisemwa kuwa Mungu, lakini wote pamoja wakiwa Mungu mmoja tu. Wanatheolojia hueleza hilo kuwa fumbo.

Je, Biblia husema lolote juu ya Utatu?a Maswali yanayofuata yangeweza kukuongoza ukate mashauri ya kupendeza. Majibu ya Kibiblia yapatikana ukurasa 12.

1. Ikiwa Mungu ni Utatu na amekuwa hivyo sikuzote, je, Wayahudi walipata fundisho hilo katika Maandiko ya Kiebrania (“Agano la Kale”)?

2. Maandiko ya Kiebrania husema nini juu ya Mungu?—Kumbukumbu la Torati 6:4; Zaburi 145; Zekaria 14:9.

3. Je, Maandiko ya Kiebrania hurejezea roho takatifu?—Waamuzi 15:14; Zekaria 4:6.

4. Katika Maandiko ya Kiebrania, je, roho takatifu hurejezewa kuwa mtu au kuwa kani ya utendaji ya Mungu?—Waamuzi 14:6; Isaya 44:3.

5. Je, Maandiko ya Kiebrania hurejezea Mesiya aliyeahidiwa, au Mtiwa-Mafuta?—Danieli 9:25, 26.

6. Je, andiko lolote katika Maandiko ya Kiebrania humfanya Mesiya sawa na Mungu?—Zaburi 2:2, 4-8; Isaya 45:18; 61:1.

7. Je, andiko lolote la Kiebrania hutoa msingi thabiti wa kuamini kwamba Yehova ni nafsi tatu katika Mungu mmoja?—Isaya 44:6; 46:9, 10.

8. Nani alituma Yesu duniani? Basi nani mkubwa zaidi?—Yohana 5:19, 23, 30; 8:42; 14:28; 17:3.

9. Yesu alipata kusema wakati wowote yeye ni Mungu?—Yohana 7:28, 29; 14:6.

10. Wengi walimwona Yesu, lakini je, kuna binadamu yeyote ambaye amepata kumwona Mungu?—Yohana 1:18; 6:46.

11. Je, Yesu alisema kwamba yeye ni “Mwana wa Mungu” au kwamba yeye ni ‘Mungu Mwana’?—Yohana 10:36; 1 Yohana 4:15; 5:5, 13.

12. Je, Yesu alipata kusema wakati wowote kwamba yeye ni sawa na Baba?—Yohana 14:28; 20:17.

13. Je, maneno “Mimi na baba tu umoja” yathibitisha Utatu?—Yohana 10:30; 17:21; Mathayo 24:36.

14. Wanafunzi wa mapema walimwonaje Yesu?—Yohana 1:29, 34, 41, 49; 6:69; 1 Wakorintho 11:3.

15. Mungu alimwonaje Yesu?—Marko 9:7; Luka 2:9-11.

16. Je, Maandiko ya Kigiriki (“Agano Jipya”) hupinga Maandiko ya Kiebrania kwamba roho takatifu si kani ya utendaji ya Mungu?—Mathayo 3:11; Luka 1:41; Yohana 14:26; Matendo 1:8; 4:31; 10:38.

17. Wakati wa ubatizo wa Yesu, Baba, Mwana, na roho takatifu walikuwa wapi? Je, walikuwa watatu katika mmoja?—Mathayo 3:16, 17.

18. Yesu aliyefufuliwa ana cheo gani katika mbingu?—Matendo 7:55, 56; Warumi 8:34; Wakolosai 3:1; Waebrania 12:2.

19. Nani alimpa Yesu cheo hicho kilichokwezwa?—Wafilipi 2:9-11.

20. Je, hiyo yamfanya Yesu kuwa Mungu au wa pili pekee kwa Mungu katika ulimwengu wote mzima?—1 Wakorintho 11:3; Wafilipi 2:9-11.

21. Ni nani aliye Mwenye Enzi Kuu kupita wote katika Ulimwengu Wote Mzima?—Kumbukumbu la Torati 3:24; Matendo 4:24-27; 1 Wakorintho 15:28.

Je! Umepata Kujiuliza? Majibu ya Biblia

“Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”—Mathayo 3:16, 17; linganisha NW.

Yanayofuata ni baadhi ya maandiko yajibuyo maswali yaliyoulizwa ukurasa 11:

1. The Encyclopedia of Religion chakiri hivi: “Wanatheolojia leo hukubaliana kwamba Biblia ya Kiebrania haina fundisho la Utatu.”[1] New Catholic Encyclopedia pia yasema: “Fundisho la Utatu Mtakatifu halifundishwi katika A[gano la] K[ale].”[2]

2. “Sikiza, ewe Isiraeli: Jehova Mwenyiezi Mngu wetu, Jehova ni mmoja.” (Kumbukumbu la Torati 6:4, The Old Testament in Swahili [Mombasa]) “Jehova atakuwa ni mfaume juu ya dunia nzima: siku hiyo Jehova atakuwa ni mmoja na jina lakwe moja.”—Zekaria 14:9, OTSW [Mombasa].

3. “Roho ya BWANA ikamjia [Samsoni] kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake.” (Waamuzi 15:14) “Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.”—Zekaria 4:6.

4. “Roho ya BWANA ikamjilia [Samsoni] kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake.” (Waamuzi 14:6) “Nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa.”—Isaya 44:3.

5. “Ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na . . . majuma sitini na mawili . . . Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu.”—Danieli 9:25, 26.

6. “BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.”—Isaya 45:18.

7. “Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi.”—Isaya 46:9.

8. “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.” (Yohana 5:30) “Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba; kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.”—Yohana 14:28.

9. “Sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.”—Yohana 7:28, 29.

10. “Hakuna mtu aliyeona Mungu wakati wo wote; Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemufunua.” (Yohana 1:18, Zaire Swahili Bible) “Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba.”—Yohana 6:46.

11. “Je! yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?”—Yohana 10:36.

12. “Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba; kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.”—Yohana 14:28.

13. “Habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.” (Mathayo 24:36) “[Wafuasi wa Yesu] wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao [wafuasi wa Yesu] nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.”—Yohana 17:21.

14. “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29) “Tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu.”—Yohana 6:69.

15. “Sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.”—Marko 9:7.

16. “Mtapokea nguvu wakati roho takatifu iwasilipo juu yenu.” (Matendo 1:8, NW) “Mungu [alimtia Yesu] mafuta kwa roho takatifu na nguvu.”—Matendo 10:38, NW.

17. Ona kielezi, kushoto, na maandishi juu na katika ukurasa 12.

18. “Tumkaziapo macho Wakili Mkuu na Mkamilishaji wa imani yetu, Yesu. Kwa ajili ya shangwe iliyowekwa mbele yake alivumilia mti wa mateso, akidharau aibu, na ameketi kwenye mkono wa kuume wa kiti cha ufalme cha Mungu.”—Waebrania 12:2, NW.

19. “Kwa sababu hiihii pia Mungu alimkweza kwenye cheo cha juu zaidi na kumpa kwa fadhili Jina lililo juu ya kila jina jingine.”—Wafilipi 2:9, NW.

20. “Kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.”—1 Wakorintho 11:3.

21. “Ewe Jehova Mwenyiezi Mngu, . . . kuna mngu gani katika mbingu na katika nti awezae kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa vitendo vyako?” (Kumbukumbu la Torati 3:24, OTSW [Mombasa]) “Vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake [Yesu], ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.”—1 Wakorintho 15:28.

[Maelezo ya Chini]

a Ili kupata uelewevu mrefu wa habari hii, tafadhali angalia kitabu Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko, kurasa 261-2 na 373-93, na broshua Je! Uamini Utatu?, vyote viwili vikiwa vimechapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

[Picha katika ukurasa wa 13]

Je, Mungu alimimina roho takatifu juu yake mwenyewe?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki