Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 9/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Hali ya Hewa Imebadilika?
    Amkeni!—2003
  • Je! Katuni Zenye Jeuri za Televisheni Hudhuru?
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Joto Hupunguza Ambukizo
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 9/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kihoro Asante sana sana kwa ile makala “Maoni ya Biblia: Msaada kwa Kihoro Chako.” (Machi 8, 1994) Hivi majuzi mume wangu, mzee katika kutaniko la Kikristo, aliuawa katika aksidenti. Maneno hayawezi kuonyesha majonzi ambayo watoto wetu watatu na mimi tumeona kwa kufiwa. Ni baraka iliyoje kusoma makala hiyo na kuona kwamba hisia tunazozipata ni za kawaida!

N. S., Marekani

Ni miaka mitatu iliyopita kwamba mama yangu, kisha baba yangu miezi mitatu iliyopita, alilala usingizi katika kifo. Hata ingawa tumaini la ufufuo ni hakika, mtengano uliosababishwa na kifo ungali wenye maumivu. Makala yenu imenichochea kukaza fikira zaidi ya wakati mwingineo juu ya tumaini la Ufalme na kuendelea kumtumikia Mungu kwa uaminifu.

K. S., Japani

Nilifiwa na baba yangu mwezi mmoja uliopita. Kihoro changu nikiwa binti hakielezeki. Makala yenu ilikuwa ya wakati ufaao sana na imenisaidia nisikate tamaa, nijapohisi maumivu.

A. P. L., Brazili

Katuni Nataka kuwashukuru kwa ile makala “Je! Katuni Zenye Jeuri za Televisheni Hudhuru?” (Desemba 8, 1993) Nina miaka minane na nilikuwa nikizitazama katuni hizi. Lakini niliposoma gazeti lenu, niling’amua kwamba katuni hizo si njema, na sasa sizitazami tena.

L. T., Italia

Muhula Mpya Nimemaliza hivi sasa kusoma Amkeni! la Machi 8, 1994 juu ya “Ule Muhula Mpya—Je! Utakuja?” Katika miaka ya mwisho ya 1960 na ya mapema 1970 nilihusika katika vikundi vya utafakari, ujiboreshaji, na ukadiriaji wa tabia-akili ziamuliwazo na matukio ya utotoni. Nilikuwa nikitafuta utoshelevu nisiupate. Halafu mke wangu akaonana na Mashahidi wa Yehova, nami nikaketi katika funzo moja. Lo, nikaipata kweli! Nilibatizwa na sasa nina pendeleo la kutumikia nikiwa mishonari hapa Ghana. Asanteni kwa gazeti hili. Kuna wengine wengi wanaotafuta utoshelevu vilevile.

D. D., Ghana

Ingawa ile harakati ya Muhula Mpya ni habari pana, mlizungumzia pande zayo mbalimbali kwa njia ya kupendeza katika nafasi ndogo sana! Nathamini mlivyodondoa mambo yale yahusianayo na harakati ya Muhula Mpya ambayo si kinyume cha Maandiko kwa lazima, kama vile afya, muziki, na mahangaiko juu ya mazingira. Mfululizo huo uliandikwa kwa kujali hisia za watu, na bado haukuepa kuzisema kweli ambazo watu wahitaji kuzisikia. Dada yangu apendezwa na falsafa za Muhula Mpya, nami nitampelekea nakala ya toleo hili.

R. H., Marekani

Joto Lenye Kuongezeka Duniani Ninaandika kujibu lile sanduku “Joto Lenye Kuongezeka Duniani na Malaria,” lililotokea kuhusiana na ule mfululizo “Ulimwengu Bila Maradhi—Je! Wawezekana?” (Desemba 8, 1993) Mimi ni mwanasayansi anayefanya kazi inayohusiana na mazingira, na inazidi kuwa vigumu kushughulika kwa uhakika wowote na lile suala la joto lenye kuongezeka duniani. Ni kweli kwamba halijoto inayoongezeka ingeweza kutarajiwa iathiri jamii nyingi za wanyama. Lakini kuhusu uhalisi wa kuwako au kutokuwako kwa ongezeko la joto duniani, ni vigumu hata zaidi kuwa na uhakika. Utafiti ambao umefanywa ni wa kutiliwa shaka sana kitakwimu. Wanasayansi fulani hata waamini kwamba kwa kweli ongezeko la kaboni dayoksaidi katika anga kutapoesha uso wa dunia!

K. O., Uingereza

Nadharia ya joto lenye kuongezeka duniani ilizungumziwa kirefu katika toleo letu (la Kiingereza) la Septemba 8, 1989, na ni kweli kwamba ni ya kubishaniwa kidogo. Hivyo sehemu yetu fupi haikuwa uthibitisho wa nadharia hii bali onyo lifaalo juu ya jambo ambalo lingeweza kutokea ikiwa kweli joto linaongezeka duniani.—Mhariri.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki