Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 10/8 uku. 31
  • Kiboko Aenda Kuokoa!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kiboko Aenda Kuokoa!
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Mtazame Kiboko Mwenye Nguvu Ajabu!
    Amkeni!—2003
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi Ambapo Wanyama Wako Huru
    Amkeni!—2003
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1999
Amkeni!—1994
g94 10/8 uku. 31

Kiboko Aenda Kuokoa!

KIBOKO, ambaye ana uzito wa kufikia tani nne, ndiye mamalia hai aliye wa pili kwa ukubwa katika nchi kavu. Taya zake zenye nguvu zaweza kuvunja mtumbwi kwa umo moja tu. Hivyo, kikundi cha wanaume kule Mbuga ya Kitaifa ya Hwange, Zimbabwe, walishangaa sana walipoona kiboko akijiendesha kwa njia waliyoona wazi si kawaida yake kamwe—hata ilikuwa ya ajabu kabisa.

Wanaume hao, wakiwa karibu na bwawa la maji, waliona impala wawili wakitimuliwa mbio na mbwa-mwitu tisa. Kwa kukosa njia ya kuponyokea, impala hao walijitupa ndani ya maji. Wale mbwa waliruka-ruka ovyo kwenye ukingo wa maji, wakiwazua ni wapi impala hao wangeelekea kuibuka.

Hatimaye, impala mmoja mchovu alianza kuogelea kwenda ufukwe wa mbali, asing’amue kwamba mbwa hao walikuwa huko wakingoja. Hata hivyo impala huyo alipokaribia nchi kavu, wale wanaume waliona kiboko aliyekuwa hapo karibu akiogelea kumwelekea impala. Alipomfikia, laripoti gazeti African Wildlife, kiboko “alimgeuza aelekee alikotoka na kumdokoa amlazimishe kuogelea upande mwingine huo.” Impala alitii. Kiboko akafuata, pindi kwa pindi akimdokoa-dokoa impala alipoonyesha ishara za kuzubaa.

Impala alipokuwa akifikia ukingo wa maji, wale wanaume walimtazama kiboko huyo akimsukuma impala kwa uanana lakini kwa imara ili apande ufukweni. Impala huyo alipiga hatua chache za kupepesuka, kisha akaacha na kusimama akitetema. Muda si muda, impala alianza kutembea kuondoka kwenye maji. Kiboko alimfuata mpaka wote wawili wakaacha kuonekana.

Ilitendeka nini kwa impala yule mwingine? Wanaume hao waripoti kwamba wale mbwa-mwitu “walikuwa wamekaza sana fikira kutazama uokozi huo hata impala huyo mwingine akawa ameponyoka bila kuonekana.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki