Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 3/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 3/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Vichezeo Nimemaliza tu kusoma ile makala nzuri “Wazazi—Chagueni Vichezeo vya Mtoto Wenu kwa Hekima.” (Septemba 8, 1994) Nikiwa mzazi, nilithamini sana habari hiyo. Hata hivyo, ningependa kuongezea dokezo la tahadhari. Tafadhali onyeni wasomaji juu ya uwezekano wa kwamba watoto wadogo waweza kufa maji katika ndoo ambamo mna hata kiwango kidogo cha maji.

E. V., Marekani

Kikumbusha hicho chathaminiwa.—Mhariri.

Mwana wangu nami tulikuwa katikati ya mazungumzo kuhusu tamaa yake ya kutaka ninunue kichezeo ambacho nilihisi hakikumfaa. Akiwa mchanga, aliona ikiwa vigumu kwake kukubali kusababu kwangu. Tulipokuwa tukizungumza, tuliangalia kifurushi cha posta, ambacho kilikuwa na Amkeni! la karibuni zaidi. Tulishangaa kuona kichwa “Je, Wajua Mtoto Wako Anacheza na Nini?” Alifurahishwa na makala hizo na akaanza kuelewa kusababu kwangu.

W. F., Marekani

Asanteni kwa makala hizo. Nina umri wa karibu miaka 13 na hufurahia utendaji wa nje ya nyumba, usanii na ufundi, na kuimba kwa piano. Nilipokuwa mchanga kidogo, nilijiundia vichezeo vyangu mwenyewe. Napenda kufanya mambo haya zaidi ya michezo ya video kwa sababu hunipa hisi ya utimilizo. Natumaini makala hizi zilisaidia watoto wengine watambue jinsi vitu hivi viwezavyo kufurahisha.

C. S., Marekani

Kiboko Asanteni kwa kuchapisha habari “Kiboko Aenda Kuokoa!” (Oktoba 8, 1994) Nilichochewa sana niliposoma kuhusu jinsi kiboko alivyomwokoa impala. Hadi wakati huu, kiboko kwa maoni yangu alikuwa mwili mkubwa mno ndani ya maji anayefungua kinywa kikubwa mno ili kuonyesha meno makubwa mno. Singalisema kwamba niliwapenda wanyama hao, lakini makala hii imebadili maoni yangu.

Y. H., Japani

Hadithi ya Mwanajeshi wa Israeli Nimemaliza tu kusoma makala “Nilizoezwa Kuua, Sasa Natolea Watu Uhai.” (Septemba 8, 1994) Mara nyingi nimechochewa kuwaandikia ili kuonyesha uthamini wangu, lakini kamwe sijapata kuchochewa kufanya hivyo kama wakati huu. Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza kuhusu itikio la Kiyahudi kwa habari njema za Ufalme wa Yehova. Sasa mmethibitisha hadithi yenye kuchangamsha moyo isivyo kawaida ya Rami Oved. Ni shangwe iliyoje kusoma juu ya ushindi wa Neno la Mungu kwa kila kipengee!

J. S., Marekani

Hadithi hiyo iligusa moyo wangu, kwa kadiri familia yangu pia ni ya nasaba ya Kiyahudi. Hali huwa ngumu kwa watu wengi wanapochagua kweli za Biblia badala ya familia zao, lakini hasa yaelekea hali ni ngumu kwa Wayahudi, kwa kuwa familia zao hukuchukulia kuwa mfu kwa maoni yao. Ingawa hivyo, familia za wazazi wangu walikuwa wororo wakati walipogundua kuwa wazazi wangu hawangeacha kweli kwa ajili ya kupendeza yeyote!

F. K., Marekani

Upasuaji wa Macho Nilisoma makala “Keratotomia ya Nusu-Kipenyo—Ni Nini?” kwa upendezi mkubwa. (Septemba 22, 1994) Kwa kuwa nitapitia upasuaji huu katika miezi michache inayokuja, nilithamini sana habari hiyo yenye kurekebisha. Ilikuwa yenye kufahamika kuliko ile niliyopewa na daktari wangu wa magonjwa ya macho.

G. C., Italia

Watoto Wanaoteseka Mfululizo wenu “Kuna Tumaini Gani kwa Watoto?” (Mei 8, 1994) ulikuwa na uhalisi uliotayarishwa vizuri sana. Kusoma maono yenye kuogofya na magonjwa hatari, na vilevile hali zenye kuogofya ambazo watoto wengi huteseka kwazo, kumenifanya nihuzunike moyoni mwangu. Lakini nilifurahia kusoma kuhusu tumaini la kweli kwa watoto ambalo litatimizwa wakati Ufalme wa Mungu utatawala wanadamu.

D. G., Papua New Guinea

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki