Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 11/8 kur. 10-11
  • Maana Halisi ya 1914

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maana Halisi ya 1914
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • 1914 Yaanzisha Wakati wa Msononeko
  • Ambayo 1914 Ungemaanisha Kwako Wewe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Ufalme wa Mungu Huanza Kutawala Katikati ya Adui Zake
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
  • 1914 ni Mwaka Uliotiwa Alama—Kwa Sababu Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Uharibifu wa Ulimwengu Uliotabiriwa Utakuja Lini?
    Amani na Usalama wa Kweli—Wewe Unaweza Kuupataje?
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 11/8 kur. 10-11

Maana Halisi ya 1914

KAMA ilivyoonyeshwa kwenye ukurasa 4, “gazeti hili hujenga uhakika katika ahadi ya Muumba ya kuleta ulimwengu mpya wenye amani na usalama kabla kizazi kilichoona matukio ya 1914 hakijapitilia mbali.”

Bila shaka wengi wa wasomaji wetu hushangazwa na mtajo huo. Hata hivyo, tangu Desemba 1879—miaka 35 kabla ya 1914—Mnara wa Mlinzi (wakati huo lilijulikana kuwa Zion’s Watch Tower and Herald of Christ’s Presence) lilitoa ithibati ya Biblia iliyothibitisha 1914 ungekuwa mwaka wa maana. Hata kabla ya hili—katikati ya karne ya 19—wanafunzi wengine wa Biblia walikuwa wamedokeza kwamba 1914 ungeweza kuwa mwaka uliotiwa alama katika unabii wa Biblia.a

Unabii umefafanuliwa kuwa historia iliyoandikwa kimbele. Sehemu hii ya Biblia hupa ushuhuda wa asili yao kuwa ya kimungu. Zaidi ya kutuambia juu ya matukio ya wakati ujao, wakati mwingine Biblia hupa kipindi cha wakati ambacho kingepita kabla ya jambo fulani kutukia. Baadhi ya unabii mbali mbali hususa hurejezea siku kadhaa, nyingine kwa miaka, na nyingine kwa karne nyingi.

Danieli, aliyetabiri kuhusu wakati Mesiya angetokea kwanza, pia alifunua wakati Mesiya angerudi katika “kuwapo” kwake kwenye ule uitwao “wakati wa mwisho.” (Danieli 8:17, 19; 9:24-27) Unabii huu wa Biblia huchukua kipindi kirefu cha wakati, si kwa mamia kadhaa ya miaka tu, bali kwa zaidi ya mileani mbili—miaka 2,520! Kwenye Luka 21:24, Yesu akiita kipindi hiki “nyakati zilizowekwa za mataifa.”b

1914 Yaanzisha Wakati wa Msononeko

Utimizo wa unabii wa Biblia waonyesha kwamba tumekuwa tukiishi katika wakati wa mwisho tangu 1914. Yesu alifafanua wakati huu kuwa “mwanzo wa utungu.” (Mathayo 24:8) Kwenye Ufunuo 12:12, twasoma hivi: “Ole wa nchi na bahari! kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.” Hii hueleza kwa nini ulimwengu umekuwa katika mchafuko mkubwa tangu 1914.

Hata hivyo, wakati huu wa mwisho wapaswa kuwa, kipindi kifupi kwa kulinganisha—kikichukua kizazi kimoja. (Luka 21:31, 32) Ule uhakika wa kwamba tuko miaka 80 baada ya 1914 huonyesha kwamba karibuni tunaweza kutarajia wokovu ambao Ufalme wa Mungu utaleta. Hili lamaanisha kwamba tutaona ‘aliye dhalili zaidi sana wa wanadamu’—Yesu Kristo—akichukua udhibiti kamili wa “ufalme wa wanadamu” na alete ulimwengu mpya wenye amani na haki.—Danieli 4:17.

[Maelezo ya Chini]

a Katika 1844, kasisi Mwingereza, E. B. Elliott, alitoa uangalifu kwa 1914 kuwa wakati huenda zile “nyakati saba” za Danieli sura ya 4 zingeisha. Katika 1849, Robert Seeley, wa London, alishughulika na habari hiyo kwa njia hiyohiyo. Joseph Seiss, wa Marekani, alielekeza kwenye 1914 kuwa tarehe muhimu katika kronolojia ya Biblia katika kichapo kilichohaririwa karibu na 1870. Katika 1875, Nelson H. Barbour aliandika katika gazeti lake Herald of the Morning kwamba 1914 iliweka alama mwisho wa kipindi kile Yesu alichokiita “nyakati zilizowekwa za mataifa.”—Luka 21:24, NW.

b Kwa maelezo zaidi ya unabii wa Danieli, ona Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko, kurasa 308-10, kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

[Sanduku katika ukurasa wa 11]

Maelezo Kuhusu 1914 na Baadaye

“Huenda ikawa kwamba, baada ya, vita vya ulimwengu viwili, ubuni wa silaha za nyukilia ulitenda kama onyo la upole, uliotuhifadhi na mgongano wa tatu wa mataifa makuu, na kuanzisha kipindi kilicho kirefu zaidi cha amani ya ujumla, tangu nyakati za Kiviktoria. . . . Ni nini kilienda mrama na ubinadamu? Kwa nini matumaini ya karne hii ya kumi na tisa yakadidimizwa? Kwa nini karne ya ishirini ikawa muhula wa maafa au kama wengine wangelisema, uovu?”—A History of the Modern World—From 1917 to the 1980s, na Paul Johnson.

“Kati ya mageuzo yote yenye msukosuko ya mfumo wa Ulaya, ile Vita Kubwa na suluhisho la amani ndizo zilizoleta badiliko kubwa zaidi la utofautiano na wakati uliopita, kiuchumi na kijamii licha ya kisiasa. . . . Ule umurua wa utukufu wa mfumo huo uliotenda kwa uhuru na wenye mazao ukayoyomea katika msiba wa vita. Badala yake, Ulaya ikabidi kukabiliana na uchumi ulioharibika na uchumi uliobadilika katika ulimwengu wote. . . . Madhara yalikuwa makubwa sana hivi kwamba uchumi wa Ulaya haukupata nafuu kutoka kwa mshuko na kutoimarika kabla ya vita ya ulimwengu iliyofuata kupiga.”—The World in the Crucible 1914-1919, na Bernadotte E. Schmitt na Harold C. Vedeler.

“Katika ile Vita ya Ulimwengu ya Pili kila kifungo kati ya mwanadamu na mwanadamu kilitoweka. Vitendo vya uhalifu vilifanywa na Wajerumani chini ya utawala wa Kihitler waliojiruhusu kujitiisha, ambavyo havilingani kwa kadiri na kwa uovu na nyingine yoyote ambayo imedunisha rekodi ya binadamu. Yale machinjo ya ujumla ya taratibu za kukomesha milioni sita au saba za wanaume, wanawake, na watoto kwenye kambi za kufishia za Ujerumani yapita kwa maafa yale machinjo ya kinyama ya Genghis Khan, na yayapunguza kuwa madogo sana kwa uwiano. Kufyeka kimakusudi jumla ya idadi ya watu kulifikiriwa na kutekelezwa na Ujerumani na Urusi katika vita ya Mashariki. . . . Hatimaye tumeibuka kutoka kwa mandhari za magofu ya kimali na maangamivu ya maadili ambayo hayakupata kamwe kudunisha fikira kwa karne zilizopita.”—The Gathering Storm, Buku 1 la The Second World War, na Winston S. Churchill.

“Sasa kuna utambuzi wa haki za kibinadamu za watu wa tabaka zote, mataifa, na jamii za watu; na bado wakati huo huo tumedidimia ndani ya vilindi ambavyo labda havijapata kusikiwa vya vita ya kitabaka, utaifa, na ubaguzi wa rangi. Harara mbaya hizi huonyeshwa wazi katika matendo ya ukatili ya kuua bila kujali, yaliyopangwa kisayansi; na hali mbili hizi zisizopatana za akili na viwango vya mwenendo zaonekana leo, zikiwa bega kwa bega, si katika ulimwengu uleule mmoja tu, bali pia nyakati nyingine katika nchi ileile moja na hata katika nafsi ileile moja.”—Civilization on Trial, na Arnold Toynbee.

“Kama zimwi vile kukawia kupita saa iliyowekwa, karne ya kumi na tisa—pamoja na utaratibu wayo, kujiamini kwayo, na imani yayo katika maendeleo ya kibinadamu—ilikuwa imekaa-kaa mpaka Agosti 1914, wakati zile serikali kuu za Ulaya zilipopatwa kwa butwaa na vurugu la akili lililoongoza moja kwa moja kwenye machinjo yasiyo ya kiakili ya mamilioni ya vijana walio bora zaidi wa kizazi hicho. Miaka minne na nusu baadaye, ulimwengu ulipokuwa ukijaribu kujifuma upya baada ya ule uangamivu wenye kubana sana wa Vita Kubwa, ikawa wazi kwa watazamaji wengi wa wakati huo (lakini si wote kwa vyovyote) kwamba masalio ya mwisho yaliyobaki ya utaratibu huo wa zamani yalikuwa yamefagiliwa mbali, na kwamba wanadamu walikuwa wameingia muhula mpya uliokuwa haufikiri sana na hausamehei sana hali za kutokamilika za kibinadamu kama ule mwingine. Wale waliokuwa wametarajia amani iingize ulimwengu mzuri zaidi waliona matumaini yao yakisalitiwa katika 1919.” —Dibaji katika 1919—The Year Our World Began, na William K. Klingaman.

[Picha katika ukurasa wa 10]

Milima ya Bavaria

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki