Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 11/8 uku. 31
  • Ndege “Aliyetoweka” Apatikana Tena

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ndege “Aliyetoweka” Apatikana Tena
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Wanaweza Kuokolewa Wasitoweke?
    Amkeni!—2012
  • Kuwatazama Ndege—Je, Kwavutia Kila Mtu?
    Amkeni!—1998
  • Spishi Zilizo Hatarini mwa Kutoweka—Mweneo wa Hilo Tatizo
    Amkeni!—1996
  • Wakati Ndege Wanapogonga Majengo
    Amkeni!—2009
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 11/8 uku. 31

Ndege “Aliyetoweka” Apatikana Tena

JE, NI nani aliye karibu saizi ya kuku wa kufugwa, ana mdomo mwekundu kama wa kasuku na pambo la manyoya zambarau-samawi, haruki, na alifikiriwa kuwa alitoweka tangu karibu 1900 hadi 1948? Dokezo jingine: Hupatikana tu katika New Zealand na ana jina la Kimaori. Ni takahe, au Notornis mantelli hochstetteri.

Ndege hawa waepaji hutumia wakati mwingi mwakani katika nchi ya milima ya Murchison na milima-milima ya Kepler ya Fiordland kusini-magharibi mwa Kisiwa Kusini cha New Zealand. Hata hivyo, wachache wameshikwa mateka, kama vile huyu mmoja aliyepigwa picha hapa katika mbuga ndogo ya umma ya Te Anau. The Illustrated Encyclopedia of Birds yataarifu kwamba ndege mkubwa huyu (karibu sentimeta 63 kwa urefu) “kwa sababu ya ushindani na unyafuzi kutoka kwa wanyama walioingizwa amepungua sana.” Kujapokuwa kushika mateka na udhibiti wa wanyafuzi, bado ni spishi iliyohatarishwa.

Chanzo hicho hicho chasema kwamba “hujilisha kwa vichwa vya mbegu na visingi vyororo vya nyasi.” Lakini analazimika kushindania chakula chake “kwa paa aliyeingizwa na kwa ujumla yeye hafui dafu katika shindano hilo.” Acheni tutumaini kwamba ndege huyu asiye na kifani hatayoyomea atoke katika orodha ya New Zealand ya wanyama haba.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki