Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 11/22 kur. 3-4
  • Sababu Ifanyayo Watoto Fulani Wawe Wagumu Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sababu Ifanyayo Watoto Fulani Wawe Wagumu Sana
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Shule Yatokeza Tatizo Hasa
  • Ono la Kibinafsi la Mama na Ronnie
  • Kulea Mtoto Aliye Mgumu
    Amkeni!—1994
  • “Kaa Tuli na Ukaze Fikira!”
    Amkeni!—1997
  • Kulikabili Hilo Tatizo
    Amkeni!—1997
  • Funguo za Elimu Nzuri
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 11/22 kur. 3-4

Sababu Ifanyayo Watoto Fulani Wawe Wagumu Sana

“Athari za jeni, kemia ya ubongo, na ukuzi wa neva za ubongo huchangia sana kwa jinsi tulivyo tukiwa watoto na tuwavyo tukiwa watu wazima.”—STANLEY TURECKI, M.D.

KILA mtoto hukua kwa jinsi ya pekee, njia tofauti. Watoto huonyesha vitabia vingi na hali zionekanazo kuwa za kuzaliwa nazo—vitabia ambavyo wazazi wana udhibiti mdogo ama hawana juu yavyo. Ni kweli kwamba watoto watukutu, wasiotulia na wasumbufu siku zote wamekuwako. Wazazi walio bora zaidi wanaweza kuwa na mtoto aliye mgumu kulea.

Lakini kwa nini watoto fulani ni wagumu zaidi hivyo na wenye kusumbua kwa kulea? Ile idadi ya watoto wanaokuwa na matatizo makubwa ya kitabia inazidi kuongezeka. Kuna mwafikiano wa ujumla kati ya wanakliniki na watafiti kwamba asilimia 5 hadi 10 ya watoto wote huonyesha dalili zaidi za kutotulia na kwamba uwezo wa watoto hawa wa kutokaza fikira, kumakinika, kufuata kanuni, na kudhibiti hisia hutokeza magumu mengi kwao na kwa familia zao, walimu wao, na marika zao.

Dakt. Bennett Shaywitz, profesa wa afya ya watoto na neva za ubongo katika Shule ya Kitiba ya Chuo Kikuu cha Yale, atoa uangalifu kwa kinachoelekea kuwa tatizo kuu: “michafuko iliyorithiwa katika kemikali fulani ndani ya mifumo ya ubongo ya kupitishia niuroni,” inayotendesha utendi wa seli za ubongo na kurahisisha jinsi ubongo unavyotendesha tabia. Lolote lifanyalo mtoto kuwa mgumu kulea, wazazi wanapaswa kutanguliza kuwa na ustadi wa kushughulikia tabia za vijana wao, wakiandaa kitia moyo na kuwaunga mkono badala ya kuwalaumu na kuwakana.

Katika nyakati za Biblia, wazazi ndio waliokuwa na daraka la kuelimisha na kuzoeza watoto wao. Walijua kwamba nidhamu na maagizo katika sheria za Mungu yangemfanya mtoto wao awe mwenye hekima. (Kumbukumbu la Torati 6:6, 7; 2 Timotheo 3:15) Hivyo basi, ni daraka la wazazi walilopewa na Mungu ili kujitahidi wawezavyo, zijapokuwa ratiba zenye shughuli nyingi, ili kutimiza mahitaji ya mtoto, hasa kuitikia kwa njia chanya kwa tabia hasi. Kwa kuwa mengi ya matatizo ya kitabia yaonekanayo katika zoezi la tiba ya watoto leo huhusu watoto ambao ni watendaji kupita kiasi, wasisimukaji, wasio na makini, mazungumzo ya ADD na ADHD kuwa visababishi kwa watoto wagumu kulea yaweza kusaidia.a

Katika miaka ya 1950, kasoro hizi ziliitwa “utendaji-kasoro mdogo wa ubongo.” Mtajo huo uliacha kutumiwa, kulingana na Dakt. Jan Mathisen tabibu wa watoto anayeshughulikia neva, machunguo yalipoonyesha kwamba “ADD haiharibu ubongo kamwe.” Dakt. Mathisen asema: “Yaonekana ADD ni kasoro katika sehemu fulani za ubongo. Bado hatuna uhakika kwa matatizo yahusikayo katika kemikali za neva, lakini tunahisi kwamba kuna uhusika na kemikali katika ubongo iitwayo dopamini.” Yeye aamini tatizo hilo hutia ndani utendaji wa dopamini. “Huenda si kemikali moja, bali mahusiano miongoni mwa kemikali kadhaa,” akaongezea.

Ingawa bado kuna maswali mengi ambayo hayajajibiwa kuhusu kisababishi cha ADD, watafiti kwa ujumla hukubaliana na Dakt. Mathisen kwamba hali mbaya sana ya utendaji wa makini, ya usisimkaji, na utendaji wa miendo hutokana na niuroni. Majuzi uchunguzi uliofanywa na Dakt. Alan Zametkin na watafiti katika Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Kiakili, katika Marekani, walipata kwa mara ya kwanza kuwa ADD huletwa na kasoro fulani hususa ya metaboli katika ubongo, ingawa ilikubaliwa kwamba “utafiti mwingi zaidi ulihitaji kufanywa ili kufikia majibu yaliyo yakini zaidi.”

Shule Yatokeza Tatizo Hasa

Kwa kawaida shule ni ngumu sana kwa watoto walio na tatizo la daima la kutokaza fikira, wakengeufu, wasisimukaji, au watendaji kupita kiasi, kwani mahitaji ya kumakinika na ya kukaa kimya huongezeka mno katika mpangilio wa darasani. Kwa sababu watoto kama hao hupata kuwa vigumu sana kukaza fikira kwa chochote kile kwa muda mrefu, ni jingine jipi wawezalo kufanya isipokuwa kutenda kupita kiasi kama wehu? Kwa wengine, ukosefu wao wa kukaza fikira ni mwingi hivi kwamba hawawezi kuendeleza usomaji wa kawaida hata nyumbani ama shuleni. Kupata kwao nidhamu kwa kuwa ama tisho kwa darasa ama kichekwa cha darasa ni kawaida, kwani wana ugumu wa kudhibiti tabia zao na kuchanganua matokeo ya matendo yao.

Hatimaye, wao hukuza mtazamo mbaya kujihusu, labda kujibandika wenyewe “mbaya” na “zuzu” na kutenda kwa kupatana nayo. Kupata gredi zenye kufeli kujapokuwa kujaribu kisulubu, watoto hawa waweza kupatwa na kushindwa kutojistahi daima.

Kwa kushangaa, wazazi wanakuwa wenye kuhangaika sana na waliofumaniwa na tabia ya mtoto wao yenye kusumbua. Nyakati nyingine kutopatana kwa ndoa hutokea, kila mzazi akimlaumu yule mwingine kwa hali hiyo. Wazazi wengi hutumia wakati mwingi kwa hasira wakipigiana zomari juu ya ubaya na kusahau uzuri. Hivyo basi, itikio lao hasi kwa vitendo vya vitabia hasi husababisha miingiliano mingi hasi. Hivyo familia, na zaidi wengine walio na mahusiano na mtoto huyo, wanakuwa daima katika kifungo cha mng’ang’ano wa mamlaka ambayo ni tokeo la kutofahamu na kutoiweza tabia ya mtoto mgumu sana—mtoto aliye, ama asiye na, Kasoro ya Upungufu wa Makini.

Ono la Kibinafsi la Mama na Ronnie

“Tangu wakati Ronnie alipokuja ulimwenguni, hakupata kamwe kuwa na furaha bali daima aliudhika-udhika na kulia. Akiwa na mzio, alikuwa na harara za ngozi, maambukizo ya masikio, na alihara daima.

“Ingawa stadi za mapema za miendo ya Ronnie zilikua vizuri, alikuwa na haraka sana kukaa kitako, kusimama, kisha kutembea—au niseme kukimbia? Nilifanya haraka kufanya kazi yangu yote ya nyumba wakati wa lepe lake la usingizi kwa sababu ‘tufani’ wangu mdogo alipoamka, ningekuwa na shughuli ya kujaribu kumlinda asijidhuru mwenyewe na nyumba akiwa katika pilikapilika kufanya chochote kilichomvutia, na vingi vyavyo vilimvutia!

“Alikuwa na umakini wa muda mfupi sana. Hakuna chochote kilichomweka kwa muda mrefu sana. Alichukia kukaa tuli. Bila shaka, hili lilikuwa tatizo tulipompeleka mahali popote alipohitajika kukaa tuli—hasa mikutano ya kutaniko. Ilikuwa bure kumgota ili akae kwa utulivu. Hangeweza kamwe. Watu wengi walio na nia njema walilalamika ama walitupa mashauri, lakini hakuna yaliyofanya kazi.

“Ronnie alikuwa mwerevu, hivyo alipokuwa apata umri wa miaka mitatu, tulianza programu ya kipindi kifupi ya kusoma naye kila siku. Alipokuwa na miaka mitano, angeweza kusoma vizuri sana. Kisha akaenda shuleni. Baada ya karibu mwezi, nilipata ombi la kwenda shuleni ili kuzungumza na mwalimu. Mwalimu huyo wa kike aliniambia kwamba kwanza alipomuona Ronnie, alifikiri alifanana na malaika, lakini baada ya kuwa naye katika darasa kwa mwezi, sasa alifikiri alitoka pale mahali pengine! Alinifahamisha kwamba yeye daima aliruka, kuchuna watoto wale wengine, ama kuwavuruta. Hangenyamaza wala kukaa kitako, na alisumbua darasa zima. Alikosa kujidhibiti. Aliona pia mtazamo wa uasi ulikuwa ukikua. Ilipendekezwa kwamba awekwe katika darasa la elimu ya kipekee na kwamba tumpeleke kwa daktari ili aandikiwe dawa ya kutumia ili atulie. Tulivunjika moyo!

“Dawa halikuwa chaguo lililofaa kwa Ronnie, lakini tabibu wa watoto alitupa madokezo fulani yenye kutumika. Lilikuwa oni lake kwamba Ronnie alikuwa mwerevu na aliyechoka kwa kukosa shughuli za kupendeza; hivyo basi, alidokeza kwamba tumfanye Ronnie awe na shughuli, kwamba tumwonyeshe upendo zaidi na zaidi, na kwamba tumsubiri na tuwe chanya. Alifikiri Ronnie angekuwa na matatizo machache akuapo na kwa kubadili lishe.

“Tuling’amua kwamba mwana wetu alihitaji kushughulikiwa kwa umakini, kwamba alihitaji kusaidiwa kujifunza kuelekeza nguvu zake kwa njia inayofaa. Hili lingechukua muda mwingi; hivyo basi, tulibadili ratiba zetu za siku, tukitumia saa nyingi na yeye juu ya kazi ya shule, kwa saburi tukimfunza na kumweleza mambo. Tuliacha kutumia maneno hasi ama kumlaumu kwa kutokuwa na fahamu na utukutu wake. Nia yetu ilikuwa kujenga hali yake ya kutojistahi. Tulizungumza badala ya kuamrisha na kudai. Ikiwa kulikuwa na maamuzi yoyote yaliyomhusu, tulimwomba maoni yake.

“Mambo mengine yanayokuja kiasili kwa watoto wengine hayakuja kwa urahisi kwa Ronnie. Mathalani, alilazimika kujifunza jinsi ya kuwa na subira, jinsi ya kuwa mtulivu, jinsi ya kukaa tuli, na jinsi ya kudhibiti utendaji wake wa kimwili usio na kiasi. Lakini ulidhibitika. Mara alipofahamu kwamba alihitaji afanye jitihada za kudhamiria ili kutulia na kufikiri kuhusu alilokuwa akifanya, ama atakalofanya, alianza kujiweza na kusawazika. Kufikia umri wa miaka 13, tabia yake ilikuwa sawa. Kwa furaha, kila jambo lilienda shwari kuanzia hapo na kuendelea, hata wakati wa miaka ya uasi ya utineja.

“Mapato kwa kumpa Ronnie upendo mwingi, na kiasi sawia cha wakati na saburi, yamekuwa na matokeo yenye kupendeza!”

[Maelezo ya Chini]

a ADD yarejezea kwa Kasoro ya Upungufu wa Makini na ADHD yarejezea kwa Kasoro ya Upungufu Kutokana na Utendaji wa Kupita Kiasi kotekote katika makala hizi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki