Je, Ni Suluhisho Sahili kwa Ukimwa?
KUANDAA vichekesho visivyo na kikomo kwa mamilioni ya wateja wakimwa sasa ni biashara nono. Likizo za ugenini, vidude tata vya elektroni, hobi zenye mambo mengi, zote hutenda ili kusaidia kupitisha wakati wa wateja. Hata hivyo, ukimwa bado ni tatizo kubwa. Hata likizoni, waenda-likizo walio na ukimwa huhitaji wacheshi ili kuwachangamsha. Na wafanya-mazoezi wengi waliojitolea huhisi kukosa kitu wakosapo uandamani wa redio yao yenye kubebeka.
Hakuna shaka kwamba utumbuizo, kama vile televisheni, hufanyiza msisimko na hupoteza ukimwa, lakini kwa muda wa kiasi gani? Kwa watu fulani ni kama dawa ya kulevya yenye kuzoeleza tabia. Wakati ufuatao, mchocheo mkubwa zaidi na msisimko zaidi wahitajiwa—la sivyo hisi ya ukiwa mzito hunawiri tena. Badala ya kuwa suluhisho, utumbuizo kama huo waweza kuishia kuwa visababishi vinavyochangia ukimwa.
Televisheni yenyewe haisababishi ukimwa, lakini kutazama televisheni sana hakutaondoa ukimwa. Kwa ubaya zaidi, kadiri unavyozidi ‘kunata kwenye’ televisheni, ndivyo uwezavyo kuzidi kutenganishwa na uhalisi. Katika kisa cha watoto, hili hutokea mara nyingi mno. Katika uchunguzi mmoja ambao katika huo watoto wenye umri wa miaka minne na mitano waliulizwa kama wangependelea kuacha televisheni au baba zao, 1 kwa kila 3 yao waliamua kwamba maisha yangevumilika zaidi bila baba!
Wala kuendekeza kila tamaa si suluhisho. Vijana wengi sasa ‘walelewa katika pindi ya hali bora ya vitu vya kimwili, na kuna kila kichezeo, kila likizo, kila mtindo mpya,’ akaonelea naibu wa Chama cha Demokrasi ya Kijamii katika bunge la Ujerumani. Je, bado kuna lolote jipya wawezalo kusisimuliwa nalo? Huenda ikawa kwamba wazazi walio wazuri wanaowasheheneza watoto wao na vidude vya vichezeo vya karibuni zaidi hakika wakatayarisha njia ya kutokeza mtu mzima aliyekumbwa na ukimwa mbaya sana.
Visababishi Vikuu vya Ukimwa
Kuepuka ukimwa kabisa ni mradi usio halisi. Maisha katika ulimwengu huu hayawezi kamwe kuwa yale ya msisimko na furaha yenye kuendelea. Tarajio kama hilo lisilo halisi laweza kusababisha kutoridhika kusiko lazima. Kwa wakati uleule, kuna visababishi hususa viongezeavyo ubaya wa mambo.
Kwa kielelezo, leo familia nyingi zaidi na zaidi zinavunjika. Je, ingeweza kuwa kwamba mama na baba wamenywelea sana kwenye utumbuizo wao wenyewe hivi kwamba hawatumii wakati wa kutosha pamoja na watoto wao tena? Haishangazi, matineja hujitafutia njia zao wenyewe za kujichangamsha katika disko, majumba ya vidio, vitovu vya ununuzi, na kadhalika. Kama tokeo, katika nyumba nyingi matembezi ya familia na utendaji mwingineo wa pamoja umekuwa mambo ya zamani.
Bado wengine wamekosa uradhi na maisha yao duni hivi kwamba kwa kukosa kufahamu hujirudia pangoni, wakifanya kivyao, bila kujali wengine. Na wanapojitenga zaidi na zaidi, wao hutumbuiza lile tumaini batili la kufikia kujitambua mwenyewe. Lakini haiwi hivyo. Hata hivyo, mkaa pweke ni uvundo. Twahitaji uandamani na uwasiliano. Hivyo basi, haiepukiki kwamba wale wanaojitenga wenyewe husambaza ukimwa, kwa kutojua wakifanya maisha yao kuwa machofu na kwa wale wanaowazunguka.
Hata hivyo, tatizo hili laonekana ni kama lenye kina zaidi, kama vile Blaise Pascal, mwanafalsafa fulani Mfaransa wa karne ya 17, kwa kulenga jambo kuu alionelea hivi: “Machofu [huibuka] kutoka kwenye vilindi vya moyo ambamo yana mizizi ya asili na [hujaza] akili na sumu yayo.” Ni ukweli ulioje!
Maadamu moyo umejaa mashaka yenye kusumbua kuhusu maana halisi ya maisha, ukimwa utadumu tu. Usadikisho unaohisiwa moyoni wahitajiwa kwamba maisha ya mtu binafsi yana maana. Hata hivyo, yeyote aweza kukabilije maisha akiwa na mtazamo chanya bila kujua sababu ya kuwa hapa, bila kuwa na miradi, bila kuwa na matumaini yenye msingi mwema ya wakati ujao?
Hapa ndipo yale maswali ya msingi huzuka: Maana ya maisha ni nini? Nipo hapa kwa kusudi gani? Naelekea wapi? “Kule kung’ang’ana ili kutafuta maana ya maisha katika maisha ya mmoja ni kani ya msingi ya kuhamasisha iliyo katika mwanadamu,” akaonelea Dakt. Viktor Frankl. Hata hivyo, maana kama hiyo yaweza kupatikana wapi? Ni wapi maswali haya yawezapo kujibiwa kwa kuridhisha?
Ukimwa Uliopunguka—Jinsi Gani?
Kile kitabu cha kale zaidi ya vyote huandaa uelewevu juu ya maswali ya msingi kama hayo. Heinrich Heine, malenga Mjerumani wa karne ya 19, alisema: “Uelewevu wangu nauwia kwa kusoma kile kitabu tu.” Kitabu kipi? Biblia. Charles Dickens kwa kufanana alisema hivi: “Ndicho kitabu bora zaidi kilichokuwa au kitakachokuwa katika ulimwengu, kwa sababu chakufunza masomo yaliyo bora zaidi ambayo kwayo kiumbe chochote cha binadamu . . . huenda chaweza kuongozwa.”
Hakuna shaka kukihusu. Biblia ni kiongozi hakika kuelekea kwenye maisha yenye maana. Kutoka mwanzo hadi mwisho, huonyesha kwamba Mungu alimpa mwanadamu kazi ili afanye. Mwanadamu alipaswa kutunza dunia, ili kuirembesha, kuzoea uangalizi wenye upendo kwa uhai wa wanyama, na, zaidi ya yote, ili kumsifu Muumba, Yehova. Jukumu kwelikweli, moja ambalo halingeacha mwanya wa ukimwa! Mamilioni ya Wakristo watendaji wamevumbua kwamba kutegemeza upande wa Mungu, kuwa waliojitoa wakfu na wajitoa kikamili kwake, hakika yaongeza maana ya maisha na kusitiri ukimwa.
Ukimwa ulioenea kotekote huenda ukawa kawaida ya kisasa—lugha nyingi za kale hazionyeshi kuwa na neno lawo. Bado, Biblia, pamoja na kutuonyesha maana ya maisha, ina madokezo yenye kutumika ya kukabiliana na ukimwa. Kwa kielelezo, hutaarifu kwamba ‘ajitengaye hushindana na kila shauri jema.’ (Mithali 18:1) Kwa maneno mengine, usirudi nyuma pangoni!
Mwanadamu kimaumbile hutaka ushirika. Huhitaji kuhusiana na watu wengine, na kwa kuzaliwa ana uhitaji wa uandamani. Kukandamiza tamaa hii ya kawaida ya kuchangamana na watu wengine—kuwa mkiwa, mtazamaji tu—si hekima. Vivyohivyo, kujiwekea mipaka ili mahusiano ya kibinafsi yawe ya juujuu tu ni sawa na kupuuza hekima yote yenye kutumika.
Bila shaka, ni rahisi zaidi kupitisha wakati kwa kutazama filamu au kuwekea mipaka uwasiliano wetu kwa kuingiza data ndani ya kompyuta. Kuzoea watu wale wengine ni tatizo. Hata hivyo, unapokuwa na jambo linalostahiki kusema na kushiriki mawazo na hisia na wengine kunathawabisha na huacha mwanya mdogo wa ukimwa.—Matendo 20:35.
Sulemani, aliyekuwa mtazamaji mwangalifu wa maumbile ya binadamu, alitoa pendekezo hili lenye nguvu: “Ni afadhali zaidi kuridhika na kile kilicho mbele ya macho yako kuliko kuacha tamaa ikudhibiti.” (Mhubiri 6:9, The New English Bible) Kwa maneno mengine, jaribu kuridhika kikamili na hali zako za sasa. Kolea kwa yale uyaonayo sasa. Hilo ni afadhali zaidi kuliko kutamani matarajio ya kuyaepuka au “kuacha tamaa ikudhibiti,” kama vile Sulemani alivyosema.
Siku zilizopangwa vizuri, miradi hususa, na tamaa yenye jitihada ili kuendelea kujifunza pia itakusaidia kushinda ukimwa. Naam, hata baada ya kustaafu, bado mtu aweza kutimiza mambo mengi. Mmoja wa Mashahidi wa Yehova katika Visiwa vya Beleares, mwanamume mstaafu aliye katika miaka ya mapema ya 70, anajifunza Kijerumani kwa bidii. Mradi wake? Anataka kuzungumza kuhusu Neno la Mungu kwa wageni walio likizoni wenye ukimwa kutoka Ujerumani. Kwa hakika ukimwa si tatizo kwake!
Hatimaye, vipi kuhusu kufanya jambo na mikono yako? Kwa nini usijipe ustadi katika ufundi fulani wa mikono, katika kupaka rangi, kucheza ala fulani ya kimuziki? Kujistahi hukua kunapokuwa na hisi ya utimizo. Kwa nini usifikirie kuhusu kukunja mikono ya shati lako na kujitolea kusaidia hapo nyumbani? Kwa kawaida kunakuwa na vitu vingi sana vidogo vihitajivyo kurekebishwa katika nyumba yoyote. Badala ya kuwaza-waza kuhusu maisha yako yenye ukimwa, jitoe, fanya kazi ya maana nyumbani, uwe mwenye ustadi katika ufundi fulani. Hutaachwa bila ya kuthawabisha.—Mithali 22:29.
Zaidi ya yote, Biblia hutushauri kufanya kazi kwa nafsi yote katika mradi wowote ule ambao huenda tufanye. (Wakolosai 3:23) Bila shaka hilo lamaanisha kujihusisha, kupendezwa kikweli na yale tunayofanya. Huenda ifae kukumbuka kwamba neno la Kiingereza “interest” [upendezi] latoka kwa lile la Kilatini interesse, ambalo kihalisi humaanisha “kuwa katikati, au miongoni,” kwa maneno mengine kunywelea kwenye jukumu ulifanyalo. Hilo litafanya lipendeze.
Mashauri mazuri haya yaliyoandikwa miaka mingi iliyopita, kama yakitumiwa, yangetokeza tofauti kubwa kwa wale washukao moyo wakati wasipokuwa na la kufanya. Hivyo basi, nywea katika lile ufanyalo. Jihusishe na watu wengine. Fanya mambo kwa niaba ya wengine. Endelea kujifunza. Wasiliana na wengine kwa uhuru. Vumbua kusudi halisi la maisha. Kwa kufanya haya yote, hutaelekea kuguna hivi: ‘Maisha ni makimwa hivyo kwa nini?’
[Sanduku katika ukurasa wa 7]
Jinsi ya Kushinda Ukimwa
1. Usiruhusu uwezo wako wa kibinafsi wa kuchukua hatua ya kwanza ulemazwe na utumbuizo bandia. Uwe mteuzi kuhusu vikengeushi na utumbuizo.
2. Husiana na watu.
3. Fuliza kujifunza. Uwe na miradi ya kibinafsi.
4. Uwe mbuni. Fanya kitu fulani kwa mikono yako.
5. Uwe na kusudi katika maisha. Mfikirie Mungu.