Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 2/8 kur. 6-8
  • Wazazi Watoroshapo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wazazi Watoroshapo
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Jeuri ya Kisaikolojia”
  • Sababu Nyinginezo
  • Malezi ya Mtoto—Maoni Yaliyosawazika
    Amkeni!—1997
  • Matatizo ya Jamaa Yatatuliwa na Mashauri ya Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Malezi ya Mtoto—Dini na Sheria
    Amkeni!—1997
  • Mzazi Mmoja, Matatizo Mengi
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 2/8 kur. 6-8

Wazazi Watoroshapo

BAADA ya teseko la miaka ya kupigwa kijeuri na kutendwa vibaya kihisia-moyo na mumeye na kisha mwishowe kuachwa kwa sababu ya mwanamke mwingine, Cheryl alishitaki ili kupata talaka.a Akiwa amepewa utunzaji wa watoto wake wote na mahakama, polepole utulivu ulianza kumrudia alipoanza kuyarudisha maisha tena kwenye ukawaida—mpaka siku moja simu ilipolia. Alikuwa mume wake wa awali. Alisema: “Ikiwa wataka kuwaona watoto wako tena, lazima ukubali tuoane tena”! Wakiwa wamekatazwa kurudi kwa mama yao baada ya kuzuru baba yao kwa mwezi mmoja katika nchi yake ya kuzaliwa, watoto wa Cheryl walitoroshwa.

Kwa kushindwa na la kufanya, Cheryl aliomba Idara ya Jimbo ya Marekani lakini akapata hakuna njia ya kisheria ya kuwaokoa watoto wake katika nchi ile nyingine. Hisia za kukata tamaa kabisa alizokuwa amezipitia katika miaka ya kucharazwa zilimrudia. “Lilikuwa karibu jambo lilelile,” aeleza. “Hujui njia ya kulisimamisha.”

“Jeuri ya Kisaikolojia”

Utoroshaji wa kimzazi umetajwa kuwa “tendo lililo kuu zaidi la jeuri ya kisaikolojia” uliotendwa dhidi ya mzazi na mtoto. Carolyn Zogg, mkurugenzi mkuu wa Child Find of America, Inc., alisema kuhusu watoroshaji kama hao: “Wazazi wanaofanya hivi wanalipa kisasi, na wanafanya katika njia ziwezazo kuwa mbaya zaidi na katika upande wenye kupiga hisia kwa urahisi zaidi. Huo ni upande upendwao zaidi na [wazazi walio na haki ya kisheria ya utunzi]—kito chao, watoto wao. . . . Hawafikirii mtoto, bali wenyewe na lile lipizo—kulipiza kisasi.”

Mtoto mtoroshwa si kwamba tu hutiisha mzazi kwa hisia za kughadhabika, upotezo, kukosa tumaini, na fadhaiko bali karibu sikuzote huharibu hali nzuri ya hisia-moyo za mtoto kwa kiwango fulani. Katika visa fulani huenda mtoto akalazimika kuishi maisha ya utoro, akiepuka ufungamano wa karibu na kusikia mapotosho na mavunga kuhusu mzazi yule mwingine. Ono hilo laweza kutokeza kasoro mbalimbali, kukojoa kitandani, kukosa usingizi, tabia ya kushikamana na mzazi kupita kiasi, kuogopa madirisha na milango, na hofu ya kupita kiasi. Hata katika watoto walio wakubwa, yaweza kutokeza kihoro na hasira.

Katika Marekani, kuna zaidi ya visa 350,000 kila mwaka ambavyo katika hivyo wazazi huchukua mtoto kwa kukiuka sheria ya mahakama ya utunzaji au hukosa kurudisha mtoto kwa wakati ulioruhusiwa. Katika zaidi ya 100,000 vya visa hivi, mtoto hufichwa na washiriki wa familia wakiwa wanakusudia kumficha daima kutoka kwa mzazi yule mwingine. Wengine huondolewa katika eneo hilo au hata nchini.

Sababu Nyinginezo

Je, ni tamaa ya upatanisho au roho ya kulipa kisasi sikuzote huhamasisha wazazi wawateke nyara watoto wao? Michael Knipfing wa Child Find aeleza kwamba wazazi fulani huhofu kushindwa katika mng’ang’ano wa kukaa na watoto na mwenzi wa awali na kwamba “kutokana na hofu wao hutangulia.” Au wakati utunzaji wa mtoto unapokuwa umeamuliwa na mzazi mmoja aendelea kumkataza yule mwingine haki za kuzuru, kuvurugika hisia hutokea. Hueleza Knipfing hivi: “Ikiwa unampenda mtoto wako na unakatazwa kumwona mtoto wako, huelekea kufikiri kwamba huna la kufanya ila kumchukua mtoto na kutoweka.”

Pia yeye ataarifu kwamba ‘watu wengi hawang’amui matokeo ya kumtorosha mtoto. Hawanga’mui watapata taabu kupata kazi. Maagizo rasmi yametolewa ili kuwatia mbaroni. Wao hufikiri tatizo liko tu baina yao na mzazi yule mwingine. Hawang’amui kwamba polisi wanajihusisha. Wanahitaji wanasheria wawili badala ya mmoja kwa sababu wana shtaka la uhalifu la kushughulikiwa pamoja na lile tatizo la haki za kiraia, ambalo ni, nani atakayepata haki za utunzaji wa mtoto.’

Wazazi fulani huenda wakashuku kwamba mtoto wao anatendwa madhara na mzazi yule mwingine. Ikiwa mfumo wa kisheria hautendi kwa haraka, basi mzazi asiye na la kufanya huenda atende yajapokuwa matokeo yoyote. Hili lilidhihirika kwenye kisa cha Hilary Morgan mwenye umri wa miaka mitano. Mwanatiba wa akili wa mtoto alishauri kwamba ziara baina ya Hilary na baba yake zapasa kusimamishwa, akiita uthibitisho wa kutendwa vibaya kuwa “dhahiri na wenye usadikisho.” Hata hivyo, mahakama ziliamua kuwa kutendwa vibaya huko kuwa si hakika na ilipendekeza ziara zisizo na udhibiti. Dakt. Elizabeth Morgan, mama ya Hilary, kwa kukiuka sheria za mahakama, alimficha bintiye. Huruma nyingi ya umma hutokezwa kwa mzazi kama huyo atekaye mtoto nyara na kukimbia akapate ulinzi.

Katika kisa cha Elizabeth Morgan, alipoteza kazi yake ya upasuaji, alitumia zaidi ya miaka miwili gerezani, na akarundikisha madeni ya kitiba na ya haki za kisheria yazidiyo dola milioni 1.5. Alielezea U.S.News & World Report hivi: “Wataalamu waniambia kwamba mtoto wangu angalikuwa mwenye kichaa cha daima sasa ikiwa singalisimamisha kutendwa vibaya huko. . . . Ilinibidi kufanya kazi ambayo mahakama ilikataa kufanya: Kuokoa mtoto wangu.”

Ni wa kweli kabisa uchunguzi uliofanywa na watafiti Greif na Hegar kuhusu utekwaji nyara ufanywao na wazazi: “Haya ni matukio yaliyo tata sana kwamba, kama kilindi cha kidimbwi cha maji, huonekana tofauti kidogo ikitegemea ile pembe iliyo; kila mara mtu akodoapo macho kwenye maji kitu kipya huonekana.”—When Parents Kidnap—The Families Behind the Headlines.

Kuongezea kwenye watoto wanaotekwa nyara na mzazi au na mtu asiyejulikana, kuna mamilioni ya watoto wengine waliopotea ulimwenguni pote—waliotupwa na walio watoro. Wao ni akina nani, na ni nini huwapata?

[Maelezo ya Chini]

a Jina limebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki