Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 2/8 kur. 26-27
  • Jina Jipya kwa Sherehe Fasiki ya Zamani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jina Jipya kwa Sherehe Fasiki ya Zamani
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Shughuli za Baada ya Masomo
    Shule na Mashahidi wa Yehova
  • Sikukuu
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Wanatafuna Kuelekea Taabu
    Amkeni!—1996
  • Jinsi Chokoleti Inavyotengenezwa
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 2/8 kur. 26-27

Jina Jipya kwa Sherehe Fasiki ya Zamani

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA JAPANI

KATIKA Uingereza, Ann mwenye miaka 15 afungua kwa msisimko bahasha ambayo imefika sasa tu kutoka posta. Achomoa kadi. Upande wayo wa mbele umepambwa kwa mioyo maridadi. Ndani ina ujumbe wa mahaba, nayo imetiwa sahihi hivi: “Kutoka kwa mvutiwa.” Kwa macho ya uvutio wa kuwaziawazia na kwa kuiva uso kidogo, Ann atweta. Ni wazi amepumbazika na sifa hiyo, lakini ametatanika. ‘Nani alinipelekea kadi hii ya valentine?’ Ann ajiuliza.

Katika Japani, msichana Yuko ameanza kufanya kazi katika ofisi moja. Siku ya Valentine yakaribia. Kuhesabu-hesabu kwa Yuko kwaonyesha kwamba itagharimu yeni 20,000 (dola 200, za Marekani) kununulia kila mmoja wa wafanyakazi wenzake wa kiume visanduku vya chokoleti. Yuko atumia wakati wa chakula cha mchana akiwa na rafikize wasichana wakinunua zile waziitazo giri-choco—chokoleti za kiwajibu.

Februari 14 ni siku ambayo wanamahaba wenye hamu nyingi ulimwenguni pote hungojea kuambiwa, kwa njia moja au nyingine, “Nakupenda.” Wala Ann wala Yuko hana habari juu ya jinsi sikukuu hii ilivyoanzishwa. Huenda wakashangaa wakijua.

Asili ya ile iitwayo sasa Siku ya Valentine yaweza kufuatishwa nyuma hadi Ugiriki wa kale, ambako ibada ya Pan ilisitawi sana. Huyu mungu wa uzazi aliyekuwa nusu-mwanamume-nusu-mbuzi alikuwa na asili ya kihayawani, isiyotabirika ambayo iliingiza hofu kuu katika wanadamu. Kwa kufaa, neno la Kiingereza “panic” (babaiko) humaanisha kwa halisi “-a kuhusiana na Pan.”

Pan alipaswa kuangalia makundi ya kufugwa huku akipiga filimbi zake. Hata hivyo, alikengeushwa fikira kwa urahisi. Pan alifanya mapenzi mengi na vimungu-virembo na miungu ya kike. Mchongo mmoja waonyesha Pan akimtongoza Afrodito, yule mungu wa kike wa mapenzi. Eros, yule mungu wa kiume wa mapenzi, aruka hewani akielea juu yao kwa kupigapiga mabawa yake—kwa kufanana sana na ile Cupid ipatikanayo leo katika mavalentine.a

Katika Roma wengi waliabudu mungu kama huyo jina lake Faunus. Yeye pia alionyeshwa akiwa kama nusu-mwanamume na nusu-mbuzi. Ibada ya Faunus ilikuwa maarufu kwenye Lupercalia, msherehekeo wa kifasiki uliofuatwa kila mwaka katika Februari 15. Katika msherehekeo huu wanaume waliovalia mavazi yasiyofunika mwili vizuri walikimbia kasi kuzunguka kilima, wakipunga viboko vya ngozi ya mbuzi. Wanawake waliotaka kuzaa watoto walisimama karibu na kijia cha wakimbiaji hawa. Waroma waliamini kwamba kuchapa mwanamke kwa kiboko kungemhakikishia kuzaa.

Kulingana na The Catholic Encyclopedia, Lupercalia ulifutiliwa mbali na Papa Gelasius 1 mwishoni mwa karne ya tano W.K.b Hata hivyo, leo twaona kifanani cha ki-siku-hizi kikisitawi chini ya mtajo: “Siku ya Mtakatifu Valentine.” Kuna nadharia mbalimbali kuhusu asili ya jina hili ‘lililofanywa kuwa la Kikristo.’ Kulingana na hadithi moja, yule maliki Mroma wa karne ya tatu Claudius 2 alikataza wanaume vijana kuoa. Valentine, padri, aliwaoza wenzi vijana kwa siri. Watu fulani husema kwamba yeye alifishwa katika Februari 14, karibu 269 W.K. Vyovyote vile, mtajo “wa kiutakatifu” hauwezi kuficha ile asili chukivu ya mwadhimisho huu. Siku ya Valentine ina mizizi katika desturi za kipagani na kwa hiyo haiadhimishwi na Wakristo wa kweli. (2 Wakorintho 6:14-18) Maonyesho ya muda wote wa mwaka ya upendo wa kweli ni yenye kuthawabisha kuliko mipwito ya muda tu ya sikukuu ya kusisimuka mawazo tu.

[Maelezo ya Chini]

a Herodotus adokeza kwamba ibada ya Pan iliathiriwa na Wamisri, ambao ilikuwa kawaida miongoni mwao kuabudu mbuzi. Kile kifungu cha maneno “roho waovu wenye umbo la mbuzi” (“majini,” UV) kipatikanacho katika Biblia huenda kikawa chadokeza namna hii ya ibada ya kipagani.—Mambo ya Walawi 17:7; 2 Mambo ya Nyakati 11:15, NW.

b Watu fulani husema kwamba Gelasius aliubadili tu Lupercalia kwa “Karamu ya Utakatisho.”

[Sanduku katika ukurasa wa 27]

Wakati Mapenzi Ni Shughuli Kubwa

KUKARIBIA kwa Siku ya Valentine katika Japani huchochea hisia zenye nguvu—si za mahaba tu bali za biashara kubwa. Kwa miongo mingi watengenezaji chokoleti walihimiza umma watoe tamutamu kama kionyeshi cha mapenzi katika Februari 14. Utangazaji wa mapana ulipata mafanikio kwa kuwa mauzo ya chokoleti yaliongezeka kwa uthabiti.

Tofauti na Magharibi, desturi ya Kijapani ni wanawake kuwanunulia wanaume. Lakini shughuli ya Siku ya Valentine haiishi katika Februari 14. Mwezi mmoja baadaye, katika Machi 14, ni lazima wanaume nao watende hivyo hivyo—kwa chokoleti nyeupe. Kwa nini? The Daily Yomiuri lajibu hivi: “Ishara ya zawadi nyeupe huzuia wanaume wowote wanyimivu au wajanja wasirudishe ile chokoleti waliyopokea na wakaepuka kuila.”

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 26]

Old-Fashioned Romantic Cuts/Dover

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki