Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 3/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • La kwa Mapadri wa Kike
  • “Kifo Katika Mtoto-Meza”
  • Wanyama Wapungua
  • UKIMWI Wasambazwa na Waendesha Malori
  • Marupurupu-Amani ya Wapi?
  • Upendezi wa Dini Wanyong’onyea
  • Baraka Zauzwa
  • Kubainisha Madereva Wakatili
  • Kombe la Dunia na Mungu
  • Maisha Yenye Vizuizi kwa Watu Wafupi
  • Uchovu—Mtego Usiotambuliwa na Madereva wa Lori
    Amkeni!—1997
  • Kuagizwa Rasmi kwa Wanawake Kwaghadhibisha Makasisi wa Anglikana
    Amkeni!—1995
  • Aksidenti za Magari Je, U Salama?
    Amkeni!—2002
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 3/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

La kwa Mapadri wa Kike

Ingawa uchunguzi wa Gallup uliofanywa ulifunua kwamba zaidi ya theluthi mbili za washiriki wa Kanisa Katoliki waliohojiwa walifikiri kwamba wanawake wanapaswa kuruhusiwa kuwa mapadri, Papa John Paul 2 kwa uthabiti amewaambia Wakatoliki wafutilie mbali wazo hilo. Katika barua kwa maaskofu, Papa alitaarifu hivi: “Natangaza kwamba kanisa halina mamlaka yoyote ya kutwesha Upadri kwa wanawake na kwamba uamuzi huu utashikiliwa na washiriki wote wa kanisa.” Barua ya kipapa iliyokuwa na kichwa “Kuhifadhi Uteuzi wa Upadri kwa Wanaume Tu” iliambatanishwa na taarifa rasmi iliyoongezea hivi: “Kwa sababu si jambo linalohitaji kubishaniwa, sikuzote hilo huhitaji imani kamili ya waumini, na kufundisha kinyume ni sawa na kuongoza dhamiri makosani.” Miezi miwili iliyotangulia, wanawake 32 waliwekwa kuwa mapadri katika Kanisa la Uingereza, wanawake wa kwanza katika historia ya kanisa hilo. Mara baada ya hilo, karibu washiriki 700 wa makasisi wa Anglikana walitangaza kusudio lao la kubadili dini na kuingia katika Ukatoliki wa Kiroma, hata ingawa ni 35 tu waliong’atuka. Maofisa fulani wa Vatikani wanaamini kwamba barua ya papa kwa upande ilikusudiwa kuwaambia mapadri Waanglikana wanaoondoka kwamba wangewakaribisha kwenye Kanisa Katoliki la Kiroma.

“Kifo Katika Mtoto-Meza”

“Katika majiji makubwa, ushawishi wa kuwa na silaha katika nyumba unaongezeka,” lasema Veja chini ya kichwa kikuu “Kifo Katika Mtoto-Meza.” Lakini mlenga shabaha kabambe wa Brazili adai kwamba: “Hakuna mtu hawezi kupatwa na aksidenti za bunduki, na njia pekee ya kuziepuka ni kutonunua bunduki.” Kwa sababu wahalifu huenda wakawa wanafahamu vizuri bunduki na kutumia athari za kushtusha, “uwezekano wa matokeo mazuri kwa anayejikinga katika mkabiliano ni mdogo sana.” Ofisa wa polisi aandika hivi: “Ukiwa bila silaha, mtu atajaribu kushinda mkabiliano kwa kutumia akili na si kwa kutumia nguvu.”

Wanyama Wapungua

Wakati mmoja Zimbabwe ilijivunia idadi kubwa ya kifaru mweusi duniani. Lakini idadi imepungua kutoka wapatao karibu 3,000 katika 1980 hadi 300 kwa sasa, laripoti gazeti The Star la Johannesburg. Wawindaji haramu waendelea kuwawinda wanyama hao kwa ajili ya pembe zao zenye thamani. Katika miaka ya karibuni serikali ilianzisha usimamizi mkali uliowapa maofisa wa idara ya mbuga mamlaka ya kuua wawindaji haramu. Tatizo ni kwamba serikali haiwezi kutoa fedha za kutosha kwa Idara ya Mbuga za Kitaifa na Wanyama wa Pori ili kulinda zamu kwa matokeo katika maeneo ya kifaru. The Star laripoti kwamba kwa sababu ya uwindaji, “Idadi ya ndovu katika Zimbabwe [imepungua] kutoka 80 000 hadi karibu 60 000 katika mwongo uliopita.”

UKIMWI Wasambazwa na Waendesha Malori

Waendesha malori katika India wafikiriwa kuwa kikundi kilicho na uwezekano mkubwa zaidi wa kupitisha virusi ya UKIMWI (HIV). Kwa kutumia vipindi virefu vya wakati wakiwa mbali na familia zao, maelfu ya madereva hupitia katika makao ya makahaba katika Bombay, ambapo makadirio yaonyesha kwamba kuanzia asilimia 50 hadi 60 ya makahaba 80,000 wafanyao kazi hapo huenda wawe na HIV. Kutoka Bombay waendesha malori hao hupitia nchi nzima. Baadhi ya vijiji karibu na njia kuu huandaa safu za vibanda ambapo wasichana wa kijiji hujipa fedha kwa kufanya ngono na madereva wa malori. Maeneo hayahaya pia hupitiwa-pitiwa na vijana walio matajiri kutoka majiji yaliyo karibu, na kama inavyotaarifiwa katika The Times of India, hili “husitawisha mfumo tata na usiofuatilika wa virusi hiyo.” Na kuongezea tatizo hilo, madereva wengi wa malori kishirikina huamini kwamba ngono ni muhimu ili kuweka miili yao ikiwa na ubaridi wanapoendesha lori kwa saa nyingi katika halijoto la juu.

Marupurupu-Amani ya Wapi?

“Ni nini kiliyapata yale matazamio ya ‘marupurupu-amani’?” likauliza gazeti la Kifaransa Valeurs Actuelles. Ule mkakamao wa Vita Baridi ukiwa unapungua na mapunguo sawia katika matumizi ya kijeshi ya serikali nyingi, matumaini yalitokezwa kwamba angalau sehemu kubwa ya rasilimali za kifedha zilizotumiwa katika silaha zingeelekezwa kwenye programu za msaada wa kibinadamu ili kusaidia kukinzana na umaskini na maradhi. Likirejezea Human Development Report ya UM ya karibuni, gazeti hilo laandika kwamba mapunguzo katika matumizi ya kijeshi kwa muda wa miaka saba iliyopita yatoshana na “akiba” iliyorundamana ya karibu dola bilioni 935, hata hivyo hakujakuwa na maongezeko yanayoambatana na hiyo kwa ajili ya programu za msaada wa kibinadamu. Ripoti hiyo pia ilionelea kwamba nchi nyingi bado huendelea kutumia fedha mara tatu au nne zaidi kwa silaha kuliko zitumiavyo kwenye programu zao za elimu na afya zikiunganishwa.

Upendezi wa Dini Wanyong’onyea

Wajapani wamekuwa na ubaridi zaidi kuelekea dini, ukatangaza uchunguzi uliofanywa na gazeti Yomiuri Shimbun. Kulingana na uchunguzi walo “Uchunguzi wa Ufahamu wa Kitaifa kwa Dini,” unaofanywa kila miaka mitano tangu 1979, uwiano wa wale wanaoamini katika dini fulani hususa karibuni umefikia rekodi ya chini ya 1 katika 4. Kwa nini kuwe na upendezi mnyong’onyevu hivyo katika dini? Kwa kustaajabisha, asilimia 47 ya wale waliohojiwa walilalamika kwamba dini zina “bidii sana kuhusu kupata fedha.” Wengine walishtaki dini juu ya “mahubiri ya ukali,” “ujihusishaji mwingi mno katika siasa,” na “kukosa kuwa na viongozi wa kidini wanaostahili staha.” Hata hivyo, “asilimia 44 walifikiri Mungu au Buddha ‘yuko.’”

Baraka Zauzwa

Kwa kukabili upungufu mkubwa wa fedha, mapadri wengi wa Kanisa Orthodoksi la Kirusi wamegeukia kuuza baraka, ingawa si mapadri wote hukubali kufanywa kwa biashara hiyo kwa njia ya wazi. The Moscow Times lanukuu padri mmoja wa Orthodoksi ya Kirusi akisema hivi: “Makanisa mengi yana uhitaji mkubwa wa fedha kwa ajili ya urekebishaji.” Hivyo mapadri hulipisha ili kubariki maduka, makao, vilabu vya pombe, na majumba ya kamari. Gari huja katika msururu wa kupata baraka. Ikitegemea muundo wa gari hilo, padri anayefanya kazi katika soko la magari yaliyotumika, hulipisha kuanzia rubles 30,000 hadi 50,000 (dola 15 hadi 25) kwa ajili ya baraka, ambazo hutia ndani sala, kuvukiza uvumba, na unyunyiziaji wa “maji matakatifu.”

Kubainisha Madereva Wakatili

Dereva aenda kasi kukupita na kwa ukorofi akata mbele yako, au amwesha mataa yake ili umwondokee njia na afanya ishara ya kukirihisha apitapo. Ukiitikia kwa njia isiyofaa, itakugharimu uhai wako, wasema wataalamu. Wao wapendekeza yafuatayo, kulingana na Chapa ya Afrika Kusini ya Reader’s Digest: Dumisha mtazamo mtulivu na wa kutoshindana. Kazia macho kwa uendeshaji wako na epuka mwonano wa macho kwa macho na huyo dereva mwingine. Angalia vioo vyako vya kando kila sekunde tatu hadi kumi. Mtambue dereva matata kabla hajafika, na mpe nafasi atakayo. Punguza mwendo ili kumruhusu dereva kukukata mbele, au washa kiashiria-barabara chako na uelekee kwenye safu iliyo na mwanya. “Jinsi utakavyoitikia dereva mkatili afuataye,” yakata kauli makala hiyo, “huenda ukawa ufunguo wa usalama wako, na hata kuokoka kwako.”

Kombe la Dunia na Mungu

“Katika mng’ang’ano wa kushinda [soka] Kombe la Dunia kwa mara ya nne [Brazili], aina zote za maonyesho ya kidini yalidhihirika,” laripoti Jornal da Tarde. “Taratibu za kidini zafuatwa kabla, wakati wa, na baada ya michezo.” Akadai Bebeto wa Brazili: “Nina uhakika kwamba [Mungu] atakuwa pamoja na Mbrazili katika Kombe hili la Dunia.” Baada ya mchezo, akiona kwamba wachezaji walihusianisha ushindi huo na Mungu, kardinali Dom Lucas Moreira Neves aliandika hivi: “Kwa wengi, ushindaji wa Kombe la Dunia huenda ukawa na mafaa ya kibinafsi, kifamilia, au viwango vya kijamii . . . : uibukaji wa ujistahi na ujitumaini; uliwazo katikati ya maumivu mengi; na hata catharsis [utakaso] kwa nchi ya ukiwa.” Ingawa hivyo, kwa kupendeza, nyota wa soka Mauro Silva alitaarifu hivi: “Tofauti na baadhi ya wachezaji wengine wa timu ya Brazili, siamini Mungu alitusaidia kushinda Kombe la Dunia. Mungu hana upendeleo, na hahusiki hata kidogo na soka.”

Maisha Yenye Vizuizi kwa Watu Wafupi

Watu mmoja-mmoja katika Ujerumani walio na urefu wa chini ya meta 1.5 wanaweza kuwa wanachama wa Shirika la Watu Wafupi, laripoti Süddeutsche Zeitung. Sabine Popp, mmoja wa wanachama hao, hapendi kuitwa mbilikimo au Liliputi. “Sisi ni watu halisi, si watu wa kihekaya tu,” akasema. Maisha ya kila siku yanaweza kuwa maisha yenye vizuizi, kwa sababu vitu kama vile vibonyezo vya lifti, swichi za taa, mashine za tiketi za viingilio na vishiko vya milango mara nyingi huwekwa juu mno hivi kwamba havifikiliki. Zaidi ya yote, matatizo ambayo watu wafupi hukabili si ya kimwili tu. Harald Berndt, mwenyekiti wa shirika hilo, alalama kwamba umma kwa ujumla haitambui uwezo wao. “Watu wafupi waweza kufanya kazi nzuri kijapo kimo chao,” yeye aeleza.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki