Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 4/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Tumaini kwa Wenye Kigugumizi
  • Ile “Biashara” ya Utalii wa Kidini
  • Matatizo ya Kula Yapanda
  • Watu wa Delhi Wasiopatikana
  • Mashahidi wa Yehova Katika Kuba
  • Antaktika—Wakati Mmoja Ilikuwa Yenye Ujoto na ya Kijani
  • Kufanywa Upya kwa Keratotomia ya Nusu-Kipenyo
  • Kitulizo kwa Wenye Mzio
  • Kufumbua Ubwana Mkubwa Usio Yakini Katika Japani
  • Dawa Pipani
  • Utalii Biashara ya Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2002
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1994
  • Matatizo ya Kula—Ni Nini Kinachoweza Kusaidia?
    Amkeni!—1999
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 4/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Tumaini kwa Wenye Kigugumizi

Mama mmoja Mwaustralia aliyepatwa na aibiko la kugugumiza alipokuwa mtoto alivunjwa moyo kwa kusikia mtoto wake mwenyewe akianza kugugumiza katika umri mchanga. Kwa hiyo alijihusisha na programu iliyokuzwa kwa ushirikiano na wanatiba wa usemi katika hospitali ya Sydney na katika Chuo Kikuu cha Sydney katika New South Wales. Siri ya mafanikio kwa hakika huwa katika kutibu watoto wakiwa wachanga iwezekanavyo. Wazazi wengi hukawia kusema tatizo kwa sababu ya maoni yaliyo na kosa kwamba mtoto anapozidi kukua zoea hilo litakwisha. Kama ilivyoripotiwa katika The Sydney Morning Herald, programu hiyo “imekuwa yenye mafanikio sana na hutoa tumaini kwamba kigugumizi chaweza kutibiwa kikamili.” Laonelea kwamba inachukua wanatiba saa kumi hivi tu ili kutibu watoto wachanga, lakini mamia ya saa yalihitajiwa ili kutibu watu wazima na watoto wenye umri mkubwa zaidi, kuongezea saa zilizotumiwa na wazazi nyumbani. “Kati ya watoto 43 waliotibiwa walio kati ya miaka miwili na mitano, uchunguzi huo unaoendelea ulipata kwamba hakuna aliyerudia hali ya kugugumiza walipofuatiliwa na watafiti kwa kati ya mwaka mmoja na miaka sita baada ya utibabu,” gazeti hilo lilisema.

Ile “Biashara” ya Utalii wa Kidini

“Utalii wa kidini unaongezeka kote katika Italia na [kwingineko] ulimwenguni,” laandika La Repubblica. Wastadi wakadiria kwamba, ukifanyiwa muhtasari wa kihesabu, mwaka 1994 “utapita rekodi zote za wakati uliopita,” ukiwa na wageni kuanzia milioni 35 hadi milioni 37 kwa majengo ya kidini ya Kikatoliki katika Italia pekee. Mafanikio ya Italia, lasema gazeti hilo, ni kwa sababu ya “makanisa yayo 30,000 yenye kuorodheshwa kuwa yenye thamani ya kisanaa, madhabahu 1,500, majumba 700 ya hifadhi za kidayosisi, dazani za makao ya kitawa, na nyumba za wakuu wa makao ya kitawa.” Utalii huo wa kidini huwa ni “biashara” iliyo na faida ya kupita kiasi ya lire bilioni 4,000 [dola bilioni 2.5 za Marekani], gazeti hilo laongeza, “lakini katika nchi nyingine pia, utalii wa kidini unapata mafanikio ya kimizungu.”

Matatizo ya Kula Yapanda

Kwa nini idadi ya wale wenye matatizo ya kula ya bulimia na anorexia yanapanda? Kwa sababu ya migongano ya kihisia-moyo ambayo husababisha mahangaiko ya kina katika ulimwengu unaoonekana “wenye kutisha na usioweza kudhibitiwa,” laripoti gazeti Your Family. Visababishi vya mahangaiko yao vina sehemu nyingi, kama vile msongo wa kimzazi wa kupata mafanikio, talaka ya wazazi, na kutendwa vibaya. Kwa kuongezea, aeleza Dakt. Danie le Grange, mshiriki wa Halmashauri ya Kitaifa ya Matatizo ya Kula, wengi hujiacha wapatwe na matatizo hayo kwa kusoma kwa makini magazeti ya fashoni na kujifunza ulaji katika jitihada inayopita kiasi ya kuwa wembamba au kwa kuiga mazoea ya kula yasiyofaa kabisa. Wanawake kati ya miaka 18 na 22 ndio wapatwao sana na hali hiyo, ingawa wagonjwa wachanga zaidi kama miaka 8 wametafuta usaidizi wa kistadi. Majeruhi waweza kutibiwa ikiwa tu wanataka, asema Dakt. le Grange, akionelea kwamba “kutibika kikamili kwawezekana.” Hata hivyo, tarakimu zaonyesha kwamba asilimia 18 ya wale wanaopatwa na matatizo ya kula hufa.

Watu wa Delhi Wasiopatikana

Zaidi ya watu 10,000 wanaripotiwa kutopatikana katika Delhi, mji mkuu wa India, kila mwaka. Kati ya hawa ni thuluthi tu ya miili au ishara zao hutambuliwa wakati wowote ule. Asilimia 50 ni watoto walio chini ya miaka 18, na wanaume hushinda wanawake kwa idadi ya 2 kwa 1. Kama ilivyoripotiwa katika The Times of India, maelfu ya wasichana wachanga huishia madanguroni. Wavulana wachanga hulazimishwa na magenge ya wahalifu kuingia katika uombaji-ombaji au kufanywa wafanye kazi kwa saa nyingi kwa mishahara michache katika mikahawa midogo.

Mashahidi wa Yehova Katika Kuba

Mashahidi wa Yehova katika Kuba wamekuwa wakifurahia uhuru zaidi kutimiza huduma yao, ambao umewawezesha kushiriki na watu habari njema za Ufalme wa Mungu. Ingawaje kazi hiyo haitambuliwi kirasmi na haijahalalishwa, wameruhusiwa kutumia ofisi zao za awali na wamekutana pamoja kwa uhuru zaidi kwa ajili ya ibada—katika kiwango cha kwamba wamekuwa na makusanyiko madogo. Wameruhusiwa kuchapisha magazeti. Wakiwa wamejawa na shangwe na idili kwa matukio haya ya hivi majuzi, Mashahidi hao wanaendelea na kazi yao ya kuhubiri, wakijitahidi kuwasilisha ujumbe wa Biblia wa tumaini.

Antaktika—Wakati Mmoja Ilikuwa Yenye Ujoto na ya Kijani

Kikundi cha wanasayansi Waaustralia na Waamerika kilipata masalio ya “majani, mbao na chavuo pamoja na vijanimaji na mayai ya wadudu . . . kilometa 500 tu kutoka Ncha ya Kusini, ikionyesha hali-anga nyuzi 20-25 Selsiasi joto zaidi ya leo,” laripoti gazeti The Australian. Uvumbuzi wa mayai ya mbawakawa yalithibitisha kuwa hali-anga ilikuwa yenye ujoto kutosha kutegemeza wadudu. Kwa kuongezea, maji lazima yawe hayakuyeyuka, na vipindi vya ukuzi vilikuwa virefu vya kutosha kuwezesha mimea kutoa maua na kutokeza mbegu. Wakati wa kipindi hichohicho, ripoti hiyo iliongeza, kulikuwa na mimea iliyokua katika Tasmania (jimbo la kisiwa la Australia kusini mwa bara) ambayo leo haikui zaidi kusini kuliko New South Wales ya kati, chini kidogo ya kilometa 1,600 kaskazini mwa Tasmania—ikitoa ushuhuda usio wa moja kwa moja kwamba hali-anga yenye ujoto wakati mmoja ilikuwapo katika eneo hilo.

Kufanywa Upya kwa Keratotomia ya Nusu-Kipenyo

Keratotomia ya nusu-kipenyo, ustadi unaopendwa sana wa kurekebisha myopia (kutoona mbali vizuri) hufanywa kwa watu zaidi ya robo milioni katika Marekani kila mwaka. Upasuaji wa pili wa kusawazisha ule wa kwanza wahitajiwa katika zaidi ya asilimia 30 ya visa vya upasuaji. Sasa, chunguo la miaka kumi linalotegemezwa na Taasisi ya Kitaifa ya Macho limeazimia “kwamba mbinu hiyo ni salama kwa kadiri na yenye matokeo lakini yaweza kuongoza kwenye mshuko uliokasishwa wa uwezo wa kuona vitu vilivyo karibu,” laripoti The New York Times. Chunguo hilo la kina kwenye tukio baada ya upasuaji limeonyesha athari ya baadaye iliyokuwa haijulikani sana: mabadiliko ya haraka katika macho ambayo hutokeza kutoona mbali kuendelee na kuwa kutoona vizuri. Mshuko wa uonaji ulionekana katika asilimia 43 ya wale waliopasuliwa. Ingawa mwingine waweza kuwa sababu ya kuzeeka kwa kawaida, mingine “ilionekana kuwa sababu ya utaratibu wa keratotomia ya nusu-kipenyo, ambayo ilielekea kusababisha mabadiliko katika baadhi ya watu wakati wa miaka ya mapema,” makala hiyo ilisema. “Watu wapaswa kutambua kwamba kuna masuala yasiyosuluhishwa,” asema Dakt. Peter J. McDonnell, mwenyekiti msaidizi wa chunguo hilo. “Hakuna uhakikisho wa mwono mkamilifu.”

Kitulizo kwa Wenye Mzio

Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, asilimia 20 ya idadi ya ulimwenguni wana namna ya mzio, laripoti gazeti la Brazili Globo Ciência. “Viishara vyote vyaonyesha kwamba mizio ni magonjwa ya ustaarabu,” asema mtaalamu wa kinga za mwili Júlio Croce. “Katika anga kuna zaidi ya vijidutu elfu kumi vyenye kudhuru.” Vya kuongezwa katika visababishi vya kawaida, kama vile vidudu na uchafuzi, ni mkazo, utumizi wa kupita kiasi wa madawa, na bidhaa za kikemikali zitumiwazo katika chakula, virembeshi, na vinywaji. Hata mazoezi ya mwili yanayopita kiasi yaweza kuongoza kwenye au kusababisha pumu. Hata hivyo, ikiwa watu watajifunza kupumua kufaako, “mazoezi ya mwili yaweza kusaidia kupunguza kiwango na mara za kupatwa na pumu,” asema Dakt. Croce. Wenye mzio wapaswa kuweka vyumba vyao vya kulala vikiwa safi na vyenye hewa ya kutosha na waepuke migusano na wanyama wa kufugwa kama vile, mbwa, paka, au ndege, na vilevile marashi na bidhaa nyingine zilizo na harufu kali. Wanapaswa pia kuepuka mabadiliko ya ghafula ya hali-joto, uvutaji sigareti, na vileo na wanapaswa kutumia dawa walizoandikiwa tu.

Kufumbua Ubwana Mkubwa Usio Yakini Katika Japani

Katika Tokyo, mabwana wakubwa wasemapo, “Maoni yako ni shauri lenye thamani” au, “Tutaitikia dokezo lako kwa busara,” yamaanisha kwamba hakuna hatua itaelekea kuchukuliwa. Vivyohivyo, ahadi za “kufikiria kwa ufahamivu” au “kufikiria kutoka pande zote za maoni” pia huelekea kutotokeza matokeo dhahiri. “Tutachunguza jambo lako” kwa kawaida humaanisha kwamba hakuna kitu kitabadilika karibuni. Ahadi za “kufikiria” ni chanya kidogo zaidi ya “kuchunguza,” na “kufikiria kwa uangalifu sana” kwamaanisha kwamba wazo hata laweza kutumiwa. Hivyo afisa wa kiserikali wa cheo cha juu alieleza maneno yanayotumika kwa ukawaida wakati wa mikutano ya kusanyiko la Tokyo City, lasema The Daily Yomiuri, katika kujibu malalamiko ya wananchi kwamba hawana “habari kamili kama serikali yaunga au haiungi mkono” mambo yaliyopeanwa. Sababu ya kutokuwa yakini, lataarifu gazeti hilo, ni kwamba “mabwana wakubwa wanatahadhari kufanya washiriki wa kusanyiko wasiaibike kwa kukataa madokezo yao.”

Dawa Pipani

Kulingana na kampuni moja ya bima ya afya katika Ujerumani, kiwango cha dawa kinachouzwa na kuandikiwa katika Ujerumani ni cha juu zaidi hivi kwamba kila mwanamume, mwanamke, na mtoto angaliweza kumeza vidonge 1,250 kwa siku. Watu hufanya nini na bidhaa zote hizi? Idadi kubwa hazitumiwi, laripoti Süddeutsche Zeitung, bali zatupwa tu. “Hatuwezi kuruhusu dawa zinazogharimu mamilioni ziishie pipani mwaka baada ya mwaka,” aomboleza mkuu wa ushirika fulani wa makampuni ya bima ya afya. Kampuni za bima ya afya zimeomba kwamba madaktari na viwanda vya madawa kupeana wagonjwa habari ya kina zaidi kuhusu dawa wanazopata na wafanye hivyo kwa “Kijerumani kinachoeleweka.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki