Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 6/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Vyombo vya Ushetani Dawa za Kulevya na Muziki wa Vyuma Vizito
    Amkeni!—1994
  • Jilinde na Muziki Usiofaa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Muziki Waweza Kweli Kuniumiza?
    Amkeni!—1993
  • Ninaweza Kuwa na Usawaziko Jinsi Gani Kuhusu Muziki?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 6/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Dini na Vita Nataka kuonyesha shukrani zangu kwa mfululizo wa Oktoba 22, 1994, “Wakati Dini Ijiungapo na Vita.” Ingawa nilijionea machinjo ya Waserbia katika Kroatia, nilikuwa mchanga sana kuweza kukumbuka. Kwa hiyo hali hii iliyo tata na yenye msiba ni jambo la ufikirio na upendezi kwangu. Nilithamini jinsi mlivyoelewesha fungu la dini na jitihada zayo zisizolegea katika kuchochea zaidi migawanyiko na chuki miongoni mwa vikundi hivi vya kitaifa.

M. K., Marekani

Nilisukumwa kuhisi huruma na ile makala “Hatukuunga Mkono Vita ya Hitler.” Iliandikwa kwa njia nzuri mno hivi kwamba ilibaki kidogo nilie. Nina umri wa miaka 15, na nahisi nikitiwa moyo kujua kwamba mnyanyaso wowote ambao huenda nikapata shuleni au katika kazi ya kuhubiri, naweza kuushinda kwa mafanikio.

A. M., Marekani

Sikuweza kuepuka kumwaga machozi kidogo juu ya majaribu ambayo familia ya Wohlfahrt ilipata. Majaribu yao yafanya mivunjiko-moyo yangu midogo kutokuwa na maana. Hiyo makala ilinitia moyo kuendelea kuvumilia, nikijua kwamba tukiwa Wakristo, twaweza kukabili upinzani kama huo mfumo huu ujapo kwenye mwisho wao.

M. S., Marekani

Jitihada za Msaada Nilihofia sana Mashahidi wa Yehova katika Rwanda. Nikiwa nimesoma makala “Kutunza Majeruhi wa Msiba wa Rwanda” (Desemba 22, 1994), sasa najua kitu fulani kuhusu magumu wanayopata. Hiyo makala ilisema kwamba kulikuwa na wengi huko ambao walikufa. Kile kilichonisaidia kuhisi vyema kidogo kuhusu jambo hili kilikuwa tumaini la kukutana nao katika Paradiso. Kwa wakati huu, nitasali kwa ajili ya waamini wenzangu katika Rwanda.

J. D., Japani

Yule Mbwa-Mwitu Mwepaji Asanteni kwa makala zenye kuelimisha na mara nyingi zenye kuchekesha mnazochapisha kuhusu uumbaji wa Yehova. Ile makala “Kiumbe Mwepaji—Mchukiwa Tena Mpendwa” juu ya Canis lupus (Septemba 8, 1994) ilikuwa yenye kupendeza mno. Lakini katika picha kwenye ukurasa wa kwanza wa hiyo makala, huyo mnyama aonekana mdogo sana kuweza kuwa mbwa-mwitu.

S. W., Ujerumani

Twatambua kwa shukrani hayo maoni ya msomaji huyu mwenye jicho kali. Inathibitika kuwa tokeo kwamba umbo hilo lililo kama kivuli cheusi lilitegemea hasa picha ya koyoti, si mbwa-mwitu. Twaomba radhi kwa hilo kosa.—Mhariri.

Ibada ya Shetani Naona kule kurudiwa-rudiwa kwa namna ileile na kukatwa shauri kwa ujumla kunakofanywa kuhusu muziki wenye mdundo mzito kotekote katika mfululizo wenu “Uvutio wa Ushetani” (Septemba 22, 1994) kuwa kwenye kufadhaisha. Ingawa ni kweli kwamba kuna bendi zinazofaa mrudio-rudio huu, makala yenu yakosa kutaja ujumbe mwingine wenye kujenga katika muziki wa mdundo mzito.

C. C., Marekani

Yaweza kuwa kweli kwamba si miziki yote yenye midundo mizito huchochea moja kwa moja Ibada ya Shetani. Hata hivyo, sura ya jeuri na hata mwenendo wa bendi kubwa za mdundo mzito wajulikana vyema sana. Na ndivyo na ushirika wa muda mrefu ambao aina hii ya muziki imekuwa nao na dawa za kulevya na jeuri. Kwa kufikiria mambo haya ya hakika, tulihisi kuwajibika kuonya wasomaji kuhusu kujihusisha na namna yoyote ya muziki huu.—Mhariri.

Chote mlichoandika kilikuwa sahihi. Binti yetu mkubwa zaidi alilelewa akiwa Mkristo. Halafu akazidi kuwa mwasi. Tuligundua kwamba alikuwa akishiriki na watoto ambao walisikiliza muziki wenye mdundo mzito. Yeye angeficha kaseti za muziki wenye mdundo mzito na kusikiliza hizo nyimbo usiku akiwa na hedifoni. Baadhi ya maneno yalikuwa ya nyimbo za kishetani! Baadaye tuligundua mifano ya kishetani iliyofichwa katika chumba chake. Hatimaye alihama kutoka nyumbani mwetu na anaendelea kuwa mfu kiroho. Na shida yote ilianza na muziki wenye mdundo mzito.

D. B., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki