Mahali Ambapo Fedha Hukaa Kwenye Miti
EBU fikiria kwamba fedha zilikua kwenye miti na kwamba ulikuwa na mti kama huo. Sasa wazia kwamba mti wako ulipandwa kandokando ya kijia kipitiwacho na dazani za majirani kila siku. Ni kwa muda gani wafikiri hizo fedha zingebaki kwenye mti wako?
Ikiwa majirani wako walikuwa Mashahidi wa Yehova, mti wako wa fedha ungekuwa salama. Kwa nini twasema hivyo? Kwa sababu Mashahidi wa Yehova hufuata onyo la Kibiblia la kujiendesha wenyewe kwa ufuatiaji-haki katika mambo yote. (Waebrania 13:18) Tukio la majuzi latolea hili kielezi.
Katika Nigeria, Afrika Magharibi, noti ya naira tano ilipatikana kwenye barabara meta 91 kutoka kwenye jumba lililo karibu zaidi la jengo la ofisi ya tawi ya Watch Tower Society. Mwenye kuipata aliifunga kwenye kitawi cha mnazi ulio karibu, akifikiri kwamba mwenye kupoteza hizo fedha huenda akarudi kuitafuta.
Ingawa hizo fedha zingeweza kuonekana kwa wazi na dazani za Mashahidi wa Yehova waliopita kila siku, hakuna yeyote aliyezidai. Baada ya siku nyingi iliondolewa na kuwekwa katika sanduku la michango la Sosaiti.