Ni Nini Kinachowapata Babu na Nyanya?
NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA ITALIA
“Nilishangaa sana kwamba nikiwa babu ningeweza kuonyeshwa wororo kama huo na wajukuu wangu. Wao ni zawadi—wazuri, mabalozi wasio na hatia kwa ajili ya kutia nguvu vifungo vya shauku.”—Ettore, huyo babu.
LICHA ya uhusiano ulio juu wenye kujenga, wazazi-wakuu, wazazi, na wajukuu si kila wakati wao huwa na uhusiano mwema siku hizi. Badala ya kushirikiana, hivyo vizazi vitatu mara nyingi hugongana. Kukiwa na matokeo gani? Upweke ulioongezeka na kutokuwa na furaha miongoni mwa wazee-wazee, wazazi-wakuu—wale washiriki wa familia ambao mara nyingi wanaelekea kudhuriwa zaidi ya wote na kutengwa, wale wazazi-wakuu ambao huenda washiriki wa familia wakawageukia wanapokuwa na magumu ya kiuchumi. Hali katika familia yako ikoje? Je, wazazi-wakuu wanathaminiwa kikweli?
Katika miongo michache iliyopita, mabadiliko ya kijamii yenye kuonekana ya ulimwenguni pote yameathiri familia na yale mahusiano miongoni mwayo, yakitokeza karibu kutoweka kabisa kwa familia ya kiukoo. Katika Ulaya, ni asilimia 2 tu ya watu wazee-wazee inayoishi pamoja na watoto wao. Hata hivyo, katika mataifa yaliyovuvumuka kiviwanda, likiwa tokeo la ongezeko la sasa katika wastani wa kiwango kitarajiwacho cha kuishi na mshuko katika uzaaji, ulinganifu wa wazazi-wakuu kwa idadi ya watu kwa ujumla waongezeka kwa kuendelea. Wazazi-wakuu hufanyiza asilimia 26 ya idadi ya watu wa Ulaya, na kulingana na uchunguzi uliochapishwa na Muungano wa Ulaya, hiyo idadi “inatarajiwa kuongezeka.” Japani, lasema Asahi Evening News, “inajivunia desturi yayo ya kutunza wananchi wayo wenye umri mkubwa.” Hata hivyo, kuna zoea linaloongezeka na lililoenea sana, hasa katika majiji, la kuacha wazazi-wakuu katika mahospitali na kliniki maalum hata wakati ambapo hakuna uhitaji hasa wa kukaa hospitalini. Katika Afrika Kusini pia, ambapo wazee-wazee kulingana na desturi wametendewa kwa heshima, sasa kuna mwelekeo wenye kuhuzunisha wa kuwakataa waliozeeka, kulingana na gazeti la habari la Cape Town The Cape Times. Hiyo ripoti inataja kihususa kwamba familia zinataka kupata “furaha nyingi iwezekanavyo katika maisha” na “wakijidanganya kwamba baada ya kuweka babu au nyanya salama katika makao ya utunzaji, wamefanya kila kitu kilichohitajiwa kutoka kwao.”
Gazeti la habari hilohilo husema juu ya kisa hususa ambacho katika hicho nyanya mzee-mzee anawekwa na watoto wake watatu katika makao ya utunzaji kwa waliozeeka, “akipewa ahadi za utegemezo na ziara za kawaida.” Lakini ni nini kinachompata? “Mwanzoni ziara ni za kila siku. Baada ya majuma kadhaa zinapunguka hadi mara tatu kwa juma. Halafu zawa mara moja kwa juma. Baada ya mwaka zawa mara mbili au tatu kwa mwezi, hatimaye mara tano au sita kwa mwaka na mwishowe hakuna zozote kabisa.” Nyanya huyu alipitishaje siku zake zilizoonekana kutokuwa na mwisho? Ufafanuzi wenye kuhuzunisha sana waeleza hivi: “Chumba chake kilikuwa na dirisha ambalo kupitia kwalo kuna mti ulioonekana, na waandamani wake pekee walioishi walikuwa hua na kwenzi waliotua katika huo mti. Yeye hungoja kuwasili kwa ndege hao kwa hamu sana kana kwamba walikuwa watu wa karibu wa ukoo.”
Likiwa tokeo la athari za Kimagharibi kwa mitindo-maisha ya Afrika Kusini, ambazo hushawishi wengi kutafuta kazi katika majiji, jambo lilo hilo latukia katika familia za kikabila. Licha ya hali za kijamiii zinazogeuka, sababu nyinginezo za kuachwa kwa wazazi-wakuu ni kutoweka kwa zile sifa za ubinadamu ambazo hutokeza maisha yenye furaha ya kijamii na familia—wema, staha kwa jirani ya mtu, shauku kwa washiriki wa familia—na mweneo wa roho ya ubinafsi, anasa, kiburi, na uasi. Kulingana na Maandiko, mshuko kama huo wa kiadili ni ishara kwamba tunaishi katika “siku za mwisho.” (2 Timotheo 3:1-5) Kwa hiyo, badala ya kuheshimu wazazi-wakuu wao wakiwa chanzo cha utajirisho na uimarisho, watoto na wajukuu mara nyingi huwaona kuwa kizuio chenye udhia, kisichojipatanisha na mabadiliko ya kijamii.a
Tofauti katika mtazamo na ukosefu wa uwasiliano baina ya vizazi yaendelea kuongezeka kwa mkazo zaidi, na hiyo husababisha mkazo wa kadiri, ikiwa hivyo hata zaidi wakati wazee-wazee wanapoishi pamoja na familia zao. Hata hivyo msaada ambao wazazi-wakuu wanaweza kutoa katika wafanyalo au wasemalo waweza kuwa wa manufaa kubwa kama nini! Basi, ni yapi baadhi ya matatizo makuu kati ya vizazi ambayo huzuia mahusiano yenye shauku kati ya wazazi-wakuu, watoto, na wajukuu? Na wazazi-wakuu wanaweza kusitawishaje upya fungu lao lenye thamani mnamo mambo ya kifamilia?
[Maelezo ya Chini]
a Ni lazima itambuliwe kwamba katika visa fulani vya ukongwe na matatizo makubwa mno ya kiafya, makao ya utunzaji yenye wafanyakazi stadi yaweza kuwa uandalizi wenye upendo na unaofaa zaidi ya wote kwa baadhi ya wazazi wazee-wazee.