Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 8/8 kur. 21-24
  • Maana ya Kinyago cha Kufunika Uso

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maana ya Kinyago cha Kufunika Uso
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Umaana wa Kinyago cha Kufunika Uso Katika Afrika
  • Matumizi ya Kinyago cha Kufunika Uso
  • Maana ya Kinyago cha Kufunika Uso kwa Mkusanyaji
  • Maana ya Kinyago cha Kufunika Uso kwa Wakristo
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Je, Kweli Kuna Ibilisi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Kuvinjari kwa Usalama Ulimwengu Ulio Chini ya Mawimbi
    Amkeni!—1995
  • Mashetani Wacheza-Dansi wa Yare
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 8/8 kur. 21-24

Maana ya Kinyago cha Kufunika Uso

MKATA-MITI AUENDEA MTI KATIKA MSITU WA AFRIKA YA KATI, AKIWA NA SHOKA MKONONI. KAZI YAKE NI YA KIDINI, MOJA AMBAYO IMEFANYWA MARA ZISIZOHESABIKA KATIKA AFRIKA KWA MILEANI NYINGI.

HUYO mkata-miti aamini kwamba katika huo mti hukaa kiumbe-roho ambacho chastahili staha yenye kina. Ili kujilinda kutokana na hasira ya kiumbe-roho hicho, huyo mkata-miti alimwendea mganga kabla ya kuingia msituni. Halafu alipitia sherehe ya kutakaswa na kutoa dhabihu kwa kiumbe-roho cha huo mti.

Yeye aupiga mti dharuba kwa shoka lake. Akiweka midomo yake mahali alipokata, kisha anyonya utomvu ili kupata uhusiano pamoja na huo mti. Baada ya mti kuangushwa, yeye auacha ardhini kwa siku kadhaa ili kupatia kile kiumbe-roho wakati wa kutosha kutafuta makao mahali pengine. Yeye aamini kwamba huo mti una nguvu yao wenyewe, licha ya kuondoka kwa kiumbe-roho. Nguvu ya huo mti ni nyingi mno hivi kwamba wale wanaoshika mbao za huo lazima, kwa ajili ya ulinzi wao wenyewe, wafuate kwa uangalifu desturi za kimapokeo walizoelezwa.

Katika mikono yenye ustadi ya mchongaji, hiyo mbao yawa kinyago cha kufunika uso. Kadiri kinyago cha kufunika uso kipatavyo umbo, ndivyo mbao inaaminika kuwa inapata uwezo wenye kuongezeka. Mchongaji hayuko huru kufanya umbo lolote apendalo; lazima yeye afuate michoro ya kitamaduni ya kikundi chake cha kabila. Asipofanya hivyo, ajihatarisha kushutumiwa na jamii yake na ghadhabu ya uwezo wa roho wa hicho kinyago cha kufunika uso.

Kinyago cha kufunika uso kimalizikapo, mganga hufanya sherehe ya kutakasa ambayo kwayo yeye hupaka kinyago cha kufunika uso michanganyo ya kimizungu. Sasa kinyago cha kufunika uso chafikiriwa kuwa na uwezo mkubwa usio wa asili na kinakuwa makao ya kiumbe-roho ambacho kinawekewa wakfu. Sasa hicho kinyago cha kufunika uso kiko tayari kutumiwa katika sherehe za kidini.

Umaana wa Kinyago cha Kufunika Uso Katika Afrika

Vinyago vya kufunika uso hutumiwa katika ibada kotekote katika sehemu kubwa ya kontinenti ya Afrika. Kitabu Masks—Their Meaning and Function chataarifu hivi: “Kinyago cha kufunika uso chaweza kuwa na kazi mbili: chaweza kutumiwa kama hirizi, kama ilivyo na kile kinyago kidogo cha kufunika uso; au chaweza kuvaliwa, ambapo kazi yacho ni kusihi kwa juhudi mababu wa kale, viumbe-roho au viumbe vingine vyenye nguvu zipitazo za asili.”

Akitoa maelezo ya kina zaidi, msomi Geoffrey Parrinder ataarifu hivi katika kitabu chake Religion in Africa: “[Vinyago vya mbao vya kufunika uso vya Kiafrika] ni vya kidini, viwe ni vya uhalisi katika sanaa, desturi za kufuata kikamili mambo au vya kuwazika tu. Hivyo huwakilisha wafu au viumbe-roho wahudumiao katika desturi zao, au ‘jamii za kisiri’ zinazohusianishwa na wafu au kutumika katika kukandamiza uchawi. Visivyojieleza au vyenye kuogofya, vilivyorembuka au vya kifumbo, vinyago vya kufunika uso hudhihirisha kwa uwezo mkubwa uwezo wa kuchochea ogofyo la wafu na vilevile usadikisho kwamba kifo sio mwisho. Hivyo hufanyizwa ili kuvaliwa na watu wanaoigiza wafu, miili yao ikiwa kwa kawaida imefunikwa kwa majoho chini ya vinyago vya kufunika uso, na hawapaswi kusemwa kuwa binadamu bali kuwa viumbe-roho.”

Licha ya matumizi yavyo katika desturi za maziko na katika ulinzi dhidi ya ulozi, vinyago vya kufunika uso huwa na fungu muhimu katika sherehe za kimapokeo, dansi za kitamaduni, mambo ya kihukumu, desturi za sherehe za uwezo wa uzaaji, na kama njia ya “uwasiliano na wafu.” Nyakati fulani vinyago vya kufunika uso hata huonekana katika maadhimisho na sherehe za Jumuiya ya Wakristo. Kwa kielelezo, katika Sierra Leone, “mashetani” yaliyovikwa vinyago vya kufunika uso hucheza hadi kwenye ua wa kanisa ili kuonyesha staha zao kwenye harusi. Katika matumizi yote haya, vinyago vya kufunika uso vina maana ileile ya msingi. Hivyo, chasema kitabu African Masks, ni “viwekeo vya uwezo wa kimungu, iwe kazi yavyo inakusudiwa kuwa ya umaana mkubwa, au isiyo na maana na yenye kutumbuiza.”

Miongoni mwa vile vikundi vya kikabila zaidi ya 1,000 katika Afrika, ni 100 hivi ambavyo hutengeneza vinyago vya kufunika uso. Vinyago vya kufunika uso hutofautiana sana katika umbo kutoka kikundi kimoja hadi kingine, navyo hutofautiana kulingana na kusudi vinavyotimiza. Na bado, licha ya unamna huu, kuna vigezo vilivyowekwa vinavyoeleweka na watu wa maeneo mengi sana ya Afrika. Kwa kielelezo, vinyago vya kufunika uso vinavyowakilisha roho za mababu wa kale kwa uhalisi huwa na sura tulivu, hali vinyago vya kufunika uso vinavyowakilisha roho zisizo za kibinadamu kwa kawaida huwa na sura geni. Kipaji kirefu kilichochongoka huwakilisha hekima na ukiroho wa kina. Macho yaliyotokeza au wonyesho wa uso ulio imara huashiria hali ya kupagawa na roho. Rangi nyeupe hudokeza roho za wafu na sifa ya ‘hali ya ulimwengu mwingine.’ Vinyago vya kufunika uso vinavyoonyesha wanyama wenye pembe, hasa nyati wa Afrika na paa, hurejezea sherehe za kupunga pepo, kuingia kwa roho katika mwili mwingine baada ya kufa, na uchawi.

Matumizi ya Kinyago cha Kufunika Uso

Katika Afrika vinyago vya kufunika uso havining’inizwi tu ukutani; hivyo hutumika katika sherehe na dansi. Hivyo vyaweza kufunika uso au kichwa kizima cha yule anayekivaa. Sehemu iliyobaki ya mwili wa mtu hufunikwa kwa majoho marefu au chane za ukindu au nyuzi-nyuzi za mti.

Mvaaji hufikiriwa kuwa katika ushirika wa moja kwa moja na kani-roho ya hicho kinyago cha kufunika uso. The New Encyclopædia Britannica hufafanua kile kinachotukia hivi: “Anapojivika kinyago cha kufunika uso, mvaaji nyakati fulani hupitia badiliko la kiwasiliani-roho na kama katika hali ya kutoweza kufahamu kitu huigiza kiumbe-roho kinachofafanuliwa na hicho kinyago cha kufunika uso. Hata hivyo, kwa kawaida mvaaji kwa ustadi huwa ‘mwenzi’ wa mhusika anayeigiza . . . Lakini ingeonekana kwamba mvaaji mara nyingi huwa kisaikolojia ameshikanishwa kwa mhusika anayesaidia kubuni. Yeye hupoteza akili yake kabisa na kuwa kama mtu afanyaye mambo bila kufikiri, bila hiari yake, ambaye amekuwa akitumiwa kwa mtu anayefananishwa na hicho kinyago cha kufunika uso.”

Kwa watazamaji waliokubaliwa—yaelekea sikuzote wakiwa waume pekee—hicho kinyago cha kufunika uso hakiwakilishi tu mtu apitaye uwezo wa asili. Wanaamini kwamba mtu apitaye uwezo wa asili hupata maisha mapya ndani ya kinyago cha kufunika uso. Hivyo, kinyago cha kufunika uso chenyewe ni kitakatifu, na uvunjaji wowote wa maagizo unaadhibiwa vikali na jamii, nyakati fulani kwa kifo. Kwa ajili ya ulinzi wake, mvaaji, kama vile mkata-miti na mchongaji, ni lazima afuate taratibu zilizokubaliwa.

Maana ya Kinyago cha Kufunika Uso kwa Mkusanyaji

Hasa wakati wa miaka 100 iliyopita, vinyago vya kufunika uso vya Kiafrika vimekusanywa kwa idili kotekote ulimwenguni. Kwa mkusanyaji, kinyago cha kufunika uso humaanisha kitu tofauti kabisa na kile kinachomaanisha kwa wale wanaozoea dini ya kimapokeo katika Afrika.

Badala ya kukiona kuwa kitu kitakatifu, cha kidini, wakusanyaji huona kinyago cha kufunika uso kuwa kazi ya sanaa inayoonyesha tamaduni ya Kiafrika. Badala ya kuchanganua kinyago cha kufunika uso kulingana na kazi yacho katika jamii, wao huona kinyago cha kufunika uso kulingana na uwazi wacho, hali yacho ya kuwa kama kitu kilicho hai, na kina cha kihisia-moyo. Wakusanyaji huuliza hivi: Ni kwa kadiri gani mchongaji huwa na hisia kwa mbao yenyewe, nyuzi zayo, kigezo chayo cha kiumbo? Ni kwa ustadi jinsi gani mchongaji hutumia ubuni na umahiri na bado abaki mnamo mtindo uliowekwa na mapokeo ya kitamaduni?

Bila shaka, mkusanyaji hapuuzi fungu la dini katika ubora wa hiyo kazi. Kwa kawaida, kwa sababu ya tofauti katika kichocheo cha mchongaji, kuna tofauti kubwa kati ya vinyago vya kufunika uso vitumiwavyo katika ibada na visanamu vilivyochongwa kwa ajili ya biashara ya watalii. Kitabu Masks of Black Africa chataarifu hivi: “Mchongaji . . . alitoa sehemu zenye kuchochea kutokana na itikadi zake za kina, staha ya kina kwa kazi yake ya kutoa umbo kwa kiumbe-roho chenye nguvu zote, katika kiwango hiki, ili kutimiza daraka lake la pekee la kijamii. Mara tu itikadi hii ya kidini . . . iliposhushwa, kazi yake, licha ya matokeo yayo ya kiufundi, ilikuwa bila maana na ya ubora wa chini wa kisanaa.”

Wale wanaokusanya vinyago vya kufunika uso kwa ajili ya majumba ya hifadhi kwa kawaida hutoa uangalifu wa karibu zaidi kwa fungu ambalo kinyago cha kufunika uso kimetimiza katika jamii kilikotoka kuliko wakusanyaji wa sanaa. Hata hivyo, habari hususa kama hiyo mara nyingi hukosekana kwa sababu ya namna ambayo vinyago vingi vya kufunika uso vimepatwa kwa miaka mingi iliyopita. Vingine vilikusanywa kama vikumbusho, vingine vilikuwa sehemu ya nyara kutoka safari za kijeshi, na bado vingine vilikusanywa kwa wingi vikauzwe. Kama tokeo, maana ya asili na utumizi wa vinyago mbalimbali vya kufunika uso mara nyingi haijulikani.

Maana ya Kinyago cha Kufunika Uso kwa Wakristo

Hivyo, vinyago vya kufunika uso vina maana moja kwa wale wanaozoea dini ya kimapokeo ya kitamaduni na maana nyingine kwa wale wanaovikusanya kama kazi ya sanaa na utamaduni. Kwa Wakristo, hivyo humaanisha kitu kingine.

Biblia huweka wazi kwamba hakuna nguvu ipitayo ya kibinadamu katika ama kinyago cha kufunika uso ama mti ambako kinatoka. Nabii Isaya anafafanua upumbavu wa mtu ambaye anatumia sehemu ya mbao kutoka mtini ili kupika chakula na kujipasha joto halafu anachonga sehemu iliyobaki kuwa kijimungu ambacho kwacho yeye hutazamia kupata msaada. (Isaya 44:9-20) Kanuni iyo hiyo hutumika kwa vinyago vya kufunika uso vya kidini.

Hata hivyo, Wakristo wanatambua kwamba kuna “majeshi ya roho waovu katika mahali pa kimbingu.” (Waefeso 6:12, New World Translation) Chini ya uwezo wa Shetani, hao hupoteza watu kwa njia ya dini bandia.—Ufunuo 12:9.

Wakristo wanakubali pia kwamba mashetani hutumia vitu vinavyoonekana ili kuwasiliana na binadamu. Hivyo, watumishi wa Mungu hawaweki chochote kinachohusiana na dini ya uwasiliani-roho, iwe ni hirizi, talasimu, pete ya kimizungu, au kinyago cha kufunika uso. Katika hili wao hufuata kigezo cha Wakristo wa mapema katika Efeso. Kuwahusu Biblia husema hivi: “Idadi kubwa ya wale waliozoea kufanya ufundi wa mazingaombwe wakaleta pamoja vitabu vyao wakavichoma kabisa mbele ya kila mtu. Nao wakapiga pamoja hesabu za bei zavyo na kukuta vikiwa na thamani ya vipande elfu hamsini vya fedha.”—Matendo 19:19, NW.

Wale wanaotamani kumtumikia Yehova hawatumii au kuweka vinyago vya kufunika uso au cho chote kinachohusiana na ibada bandia. Ni la kawaida elezo la Pius, mzee Mkristo katika Nigeria: “Vinyago vya kufunika uso huonyesha mawazo ya kidini ya wale wanaovitumia. Vinyago vya kufunika uso vina majina na hupewa kicho au kustahiwa kwa kutegemea kijimungu vinachowakilisha. Singeweka kinyago cha kufunika uso kamwe nyumbani mwangu kwa sababu hili lingemkasirisha Yehova na pia kwa sababu wageni huenda wakadhania mimi nakubali itikadi za kidini zinazowakilishwa na hicho kinyago cha kufunika uso.”

Wakristo wa kweli wanajua kwamba sheria ya Mungu iliyotaarifiwa waziwazi iliyopewa Waisraeli ilikuwa hii: “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu [“atakaye ujitoaji usiohusisha wengine,” NW].”—Kutoka 20:4, 5.

[Sanduku katika ukurasa wa 23]

Vinyago vya Kufunika Uso Katika Tamaduni Nyingi

Neno “kinyago cha kufunika uso” humaanisha nini kwako? Katika tamaduni fulani hilo neno ni nahau ya kuonyesha kufunikwa kwa kitu fulani. Ikiwa unapendezwa na michezo, huenda ukawazia kinyago cha kufunika uso kuwa kitu cha kulinda uso kutokana na umizo, kama vile katika besiboli na mchezo wa kupigana kwa upanga. Labda wawazia kisetiri cha gesi, kisetiri cha upasuaji, au kisetiri cha mchezo wa watu wanaovaa vinyago vya kufunika uso ili kuiga watu wengine.

Hata hivyo, kwa watu wengi leo, vinyago vya kufunika uso humaanisha dini. Yataarifu The New Encyclopædia Britannica: “Vinyago vya kufunika uso huwakilisha kani takatifu zenye mafaa na zenye laana katika dansi za kidini—hasa katika makao ya watawa ya Kibuddha ya Nepal, Tibet, na Japani na nyingi za jamii zisizostaarabika—hufanyizwa na kikundi cha vitu vitakatifu viwezavyo kuwakilishwa. Hivyo kwa kawaida huabudiwa tu kama sanamu zinavyoabudiwa.”

Vinyago vya kufunika uso vya kidini hupatikana katika tamaduni zote na ni vya tangu nyakati za mapema kabisa. Kwa mababu zetu wa kale yaelekea hivyo vilikuwa na fungu muhimu katika maisha ya kidini na kijamii. Kitabu Masks—Their Meaning and Function chataarifu hivi: “Mwanzoni, kila kinyago cha kufunika uso kilijazwa umaana, na kinyago cha kufunika uso chenyewe au mtu aliyekivaa kwa njia isiyojulikana aliwakilisha nguvu fulani au kiumbe-roho.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki