Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 8/22 kur. 4-6
  • Sababu ya Kutoogopa Kusema kwa Ujasiri

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sababu ya Kutoogopa Kusema kwa Ujasiri
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Maovu ya Unazi Yafunuliwa
    Amkeni!—1995
  • Wewe Humtii Nani—Mungu Au Wanadamu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Sababu kwa Nini Makanisa Yalikaa Kimya
    Amkeni!—1995
  • Hatukuunga Mkono Vita ya Hitler
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 8/22 kur. 4-6

Sababu ya Kutoogopa Kusema kwa Ujasiri

KWA kurejeza kumbukumbu nyuma, ingeweza kusemwa kwamba mgongano baina ya Mashahidi wa Yehova na Unazi, ama Usoshalisti wa Kitaifa, ulikuwa bayana. Kwa nini? Kwa sababu ya madai ya Kinazi yasiyonyumbuka yaliyogongana na itikadi tatu za msingi za Mashahidi zinazotegemea Biblia. Hizi ni: (1) Yehova Mungu ni Mwenye Enzi Kuu wa Ulimwengu Wote Mzima. (2) Wakristo wa kweli ni wasiokuwamo kisiasa. (3) Mungu atawafufua wale ambao wamethibitika kuwa waaminifu kwake hadi kifo.

Itikadi hizi zitegemeazo Biblia ziliamua msimamo imara wa Mashahidi wa Yehova dhidi ya madai ya Kinazi yasiyo ya kimungu. Hivyo, wao walisema kwa ujasiri na kufunua Unazi kuwa uovu mkubwa.

Mashahidi wa Yehova walikataa kusema mwokozi ni Hitler. Walikataa kwa sababu wao huhesabia wokovu wao Mungu na wameweka maisha zao wakfu kwake peke yake. Biblia husema hivi kuhusu Yehova: “Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.”—Zaburi 83:18.

Kwa kweli, mtajo “Mwokozi ni Hitler” ulionyesha kwamba wokovu ulitokana na Hitler. Kwa hiyo Mashahidi hawangeweza kuwa waaminifu kwa Mungu na kwa wakati uleule kuhesabia wokovu binadamu yeyote. Uhai wao na vilevile uaminifu-mshikamanifu na utii wao ulikuwa mali ya Mungu.

Mashahidi wa Yehova walikuwa na watangulizi waliokuwa wazi kuhusu kukataa kutii madai yenye makosa ya Hitler. Kwa kielelezo, mitume wa Yesu wa karne ya kwanza walipoamrishwa kukoma kutangaza habari njema kuhusu Kristo, wao walikataa. Walisema hivi: “Ni lazima tumtii Mungu akiwa mtawala kuliko wanadamu.” Biblia yasema kwamba kwa sababu ya msimamo wao wenye azimio, hizo mamlaka “ziliwacharaza viboko, na kuwaamrisha kuacha kusema kwa msingi wa jina la Yesu.” Hata hivyo, mitume walikataa kutii amri hiyo yenye kumkana Mungu. “Waliendelea kutangaza habari njema bila kuacha.”—Matendo 5:29, 40-42, New World Translation.

Wakristo wengi wa mapema walikufa kwa sababu walitii Mungu badala ya wanadamu. Wengi waliangamia katika nyanja za Kiroma za mashindano kwa sababu walikataa kuhesabia wokovu wao Kaisari kwa kumfanyia tendo la ibada. Lakini kwa watu kama hao ilikuwa heshima na ushindi kuthibitika waaminifu kwa Mungu kufikia kifo, sawa na vile mwanajeshi shujaa mwenye hiari hufa kwa niaba ya nchi yake.

Kwa sababu Mashahidi wa Yehova hutetea serikali moja tu, Ufalme wa Mungu, watu wengine wamewaona kama wenye nia ya kupindua serikali. Lakini hiyo si kweli kamwe. Kwa kuwaiga mitume wa Yesu, “wao si sehemu ya ulimwengu.” (Yohana 17:16, NW) Wao ni wasiokuwamo kisiasa. Kwa sababu ya uaminifu-mshikamanifu wao kwa Mungu, wao hutii sheria za serikali za kibinadamu zilizopo. Kwa kweli, wao ni kielelezo bora katika ‘utii wao kwa mamlaka zilizo kuu.’ (Warumi 13:1) Wao hawajapata kamwe kuunga mkono uasi dhidi ya serikali yoyote ya kibinadamu!

Hata hivyo, kuna mstari ambao hauwezi kuvukika katika hali zozote zile. Huo ni mstari kati ya daraka la Mashahidi wa Yehova kwa mwanadamu na daraka lao kwa Mungu. Wao humtolea Kaisari, au mamlaka za kiserikali, kile ambacho ni cha Kaisari, lakini kwa Mungu kile ambacho ni Chake. (Mathayo 22:21) Mtu yeyote akijaribu kutaka kutoka kwao kile ambacho ni cha Mungu, jaribio hilo litashindwa.

Vipi ikiwa Shahidi anatishwa kwa kifo? Mashahidi wa Yehova wana usadikisho usioyumbayumba katika uwezo wa Mungu wa kuwarudisha kwenye uhai. (Matendo 24:15) Kwa hiyo Mashahidi wana mtazamo sawa na ule wa vijana watatu Waebrania waliokuwa nao katika Babiloni ya kale. Walipotishwa kwa kifo katika tanuru yenye moto, wao walimwambia Mfalme Nebukadreza hivi: “Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa. . . . Ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”—Danieli 3:17, 18.

Hivyo, kama ilivyotajwa mapema, Hitler alipoanza kupanda kwenye cheo chake kikuu akiwa mungu aliyejiweka rasmi, pambano la kimawazo lilikuwa bayana. Upanga wa Utawala wa Nazi, ulipovutwa kutoka alani, ulijipata wenyewe katika mkabala wa ana kwa ana na kikundi kidogo mno cha Mashahidi wa Yehova ambao walikuwa wameapa uaminifu-mshikamanifu wao kwa Mungu wa kweli, Mungu Mweza Yote, Yehova. Hata hivyo, hata kabla ya pambano kuanza, matokeo yalikuwa yameamuliwa.

[Sanduku katika ukurasa wa 5]

Waaminifu Hadi Kifo

WOLFGANG KUSSEROW alikuwa mmoja wa wale waliouawa kwa sababu alidumisha uaminifu kwa Mungu na kukataa kuunga mkono Unazi. Muda mfupi kabla ya kunyongwa Machi 28, 1942, aliwaandikia wazazi na ndugu zake hivi: “Sasa, nikiwa mwana wenu wa tatu na ndugu, lazima niwaache kesho asubuhi. Msihuzunike, kwani wakati utakuja tutakapokuwa pamoja tena. . . . Itakuwa shangwe iliyoje wakati huo, tutakapounganishwa tena! . . . Sasa tumetenganishwa, na kila mmoja wetu lazima aushinde huo mtihani; ndipo tutathawabishwa.”

Muda mfupi kabla ya kufishwa kwake katika Januari 8, 1941, Johannes Harms aliandika katika barua ya mwisho kwa baba yake hivi: “Uamuzi wa kuuliwa kwangu tayari umetangazwa na nimefungwa kwa minyororo mchana na usiku—hizo alama (kwenye karatasi) zatokana na pingu . . . Baba yangu mpendwa, ambaye niko nawe kiroho nakusihi, ubaki mwaminifu, kama nilivyojaribu kubaki mwaminifu, nasi tutaonana tena. Nitakuwa nikikufikiria mpaka nife.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki