Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 9/22 kur. 3-5
  • Uchezaji Kamari—Uraibu wa Miaka ya 1990

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uchezaji Kamari—Uraibu wa Miaka ya 1990
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kuna Ubaya Gani Kucheza Kamari?
    Amkeni!—2002
  • Wazoezwaji Wapya wa Uchezaji Kamari—Vijana!
    Amkeni!—1995
  • Je! Kucheza Kamari Kwafaa Wakristo?
    Amkeni!—1994
  • Je, Biblia Inashutumu Kucheza Kamari?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 9/22 kur. 3-5

Uchezaji Kamari—Uraibu wa Miaka ya 1990

KAMERA iliyotiwa filamu yenye rangi yatokeza wazi tamasha. Picha yajaa kurasa mbili zinazoangaliana katika gazeti la habari la Jumapili—kwa karibu umbali uwezao kuonwa na jicho, bohari kubwa mno lililogeuzwa kuwa ukumbi wa kuchezea kamari, maelfu ya futi-mraba zalo, zina ukelele wa wateja wa umri wote na rangi zote wakicheza kamari. Waona nyuso zao zilizochoka na macho yao mekundu, ishara za saa nyingi za mchezo usiokwisha. Wanangojea kwa hamu kutangazwa kwa nambari ifuatayo ambayo, ni matumaini yao, itamaanisha kwamba hatimaye wanashinda katika kile ambacho kimekuwa usiku usiowezekana kushinda.

Fungua kurasa za hilo gazeti la habari. Waona nyuso zenye hangaiko za watu viganja vikiwa vimejaa karata, wakiwa na hofu kwamba huenda wameshikilia karata zenye kupoteza. Katika visa vingi watu hujishindia na kupoteza maelfu ya dola kwenye duru ifuatayo. Wazia zaidi ya picha. Je, waweza kuona vile viganja vyenye jasho-jasho vya mikono yenye wasiwasi? Waweza kusikia ule mpigo wa kasi wa moyo, sala ya kimya ya kuomba karata bora wakati ufuatao na ya kupoteza kwa wale wachezaji wengine?

Ingia ndani ya majumba ya kamari yenye ustarehe mwingi katika hoteli zenye fahari na mashua za mitoni. Je, umepotea katika mashine nyingi mno za kutumbukizia visarafu zilizojaa kelele za kusherehekea? Je, unatiwa uziwi na sauti za vishikio vyazo vikivutwa na zile kelele za duara zenye kuzunguka? Bila kujali kushinda au kupoteza, hiyo ni sauti ya muziki masikioni mwa wachezaji. “Msisimko wao ni raha ya kile kitakachotokea katika kuvutwa kufuatako kwa kishikio cha mashine ya kutumbukizia visarafu,” akasema msimamizi wa jumba moja la kuchezea kamari.

Pita katikati ya watu wengi mno hadi kwenye meza zenye watu wengi za kizungushi duara. Waweza kutiwa kiwi na mzunguko wa duara lenye sehemu nyekundu na nyeusi likizunguka vuruvuru mbele yako. Sauti ya kipira chenye kutapa-tapa yaongezea hali hiyo. Duara lazidi kuzunguka, na mahali linaposimama yamaanisha kati ya kushinda na kupoteza. Mara nyingi maelfu ya dola hupotezwa kwa mzunguko mmoja wa duara.

Jumlisha hizo picha na mandhari kwa makumi ya maelfu, wachezaji kwa mamilioni yasiyohesabika, na maelfu ya mahali pa kuchezea ulimwenguni pote. Watu huja kwa ndege, gari-moshi, meli, na magari kutoka sehemu zote za ulimwengu ili kutosheleza hamu yao nyingi ya kucheza kamari. Kumeitwa “ugonjwa uliofichika, uraibu wa miaka ya 1990: Shurutisho la Kucheza Kamari.” “Natabiri kwamba uchezaji kamari uliohalalishwa utafikia upeo wa kihistoria ulimwenguni pote katika miaka ya 1990,” akasema mtafiti Durand Jacobs, mtaalamu wa kitaifa kuhusu tabia ya uchezaji kamari.

Kwa kielelezo, katika Marekani, katika 1993 Wamarekani zaidi walienda kwenye majumba ya kuchezea kamari kuliko kwenye stediamu ya ligi kuu ya besiboli—ziara milioni 92. Yaonekana hakuna mwisho wa kujengwa kwa majengo mapya ya kuchezea kamari. Waendesha hoteli katika Pwani ya Mashariki ya Marekani wamejawa na shangwe. “Yaelekea hakuna vyumba vya kutosha kukaa watu wapatao 50,000 wanaozuru majumba ya kamari kwa siku.”

Katika 1994, katika majimbo mengi ya kusini, ambapo ni muda mfupi tu uliopita uchezaji kamari ulionwa kuwa utendaji wenye dhambi, sasa wakaribishwa kwa mikono yote na kuonwa kuwa mwokozi. “Leo, eneo la Marekani liitwalo Ukanda wa Biblia laweza pia kupewa jina upya kuwa Ukanda wa Uchezaji Karata, kukiwa na majumba ya kamari yaliyojengwa kwenye mashua na kwenye bara kotekote Mississippi na Louisiana na mipango ya mengine zaidi katika Florida, Texas, Alabama na Arkansas,” likaonelea U.S.News & World Report. Baadhi ya viongozi wa kidini sasa wamebadili kabisa maoni yao kuhusu uchezaji kamari kuwa dhambi. Kwa kielelezo, maofisa wa jiji la New Orleans, Louisiana, walipozindua jumba lao la kamari la kwanza la mashuani kwenye Mto Mississippi katika 1994, kasisi mmoja alitoa sala, akimshukuru Mungu kwa “kipawa cha kucheza kamari: sifa ambayo kwayo,” yeye akasema “umebarikia jiji.”

Inatarajiwa kwamba kufikia mwaka 2000, asilimia 95 ya Wamarekani wote wataishi umbali wa mwendo wa gari wa saa 3-4 kutoka majumba ya kuchezea kamari. Wahindi-Waamerika pia wamepata sehemu kubwa mno ya uchezaji kamari. Hivyo serikali ya Marekani imeidhinisha Wahindi-Waamerika kuendesha majumba 225 ya kamari na kumbi za uchezaji kamari wa kutumia fedha nyingi kotekote taifani, likaripoti U.S.News & World Report.

Wakati vyumba vya kuchezea karata, kubahatisha pesa kuhusu matokeo ya michezo, mashindano ya farasi na mbwa, kamari za kanisa, na vitu kama hivyo vyaongezwa katika huo mchanganyiko, inakuwa dhahiri jinsi Wamarekani walibahatisha kihalali dola bilioni 394 katika 1993, ongezeko la asilimia 17.1 kupita mwaka uliotangulia. Wale wanaopinga uchezaji kamari wanashikwa na bumbuazi. “Vitu vikubwa tulivyo navyo ili kusaidia watu ni makanisa na mahekalu na serikali,” akasema mkurugenzi mkuu wa Shirika moja la Shurutisho la Kucheza Kamari. “Na sasa hivyo vyote vimo katika biashara ya uchezaji kamari.” Gazeti moja la habari la Marekani liliita Marekani “Taifa la Kucheza Kamari” na kusema kwamba kucheza kamari ni “kipitisha-wakati kikubwa zaidi cha kitaifa cha Marekani.”

Uingereza imeanza bahati nasibu yayo ya kwanza tangu 1826, na mauzo yanasemwa kuwa yenye ufanisi. Hiyo pia yapata ongezeko kubwa mno na la haraka la kamari ya karata, likaripoti The New York Times Magazine. “Moscow sasa imejawa na majumba ya kamari yenye shughuli nyingi. Na wacheza-kamari wa Lebanoni wanahatarisha kihalisi maisha zao ili kwenda kwa ukawaida katika majumba ya kuchezea kamari ya West Beirut ambayo hushambuliwa kwa usawa na wanamgambo na washikilia dini sana,” likaripoti Times. “Wanaoshinda pesa nyingi wasindikizwa nyumbani na walinzi wa majumba ya kamari waliojihami kwa bunduki zenye kumimina risasi.”

“Wakanada hawatambui kwamba wao ni taifa la wacheza-kamari,” akasema msimamizi wa mchezo wa kimkoa wa Kanada. “Kuhusiana na mambo fulani, yaelekea kuna kiwango cha juu zaidi cha kucheza katika Kanada kuliko kilivyo katika Marekani,” yeye akaongeza. “Wakanada walitumia zaidi ya bilioni 10 katika kubahatisha na kuweka sharti kwa halali mwaka uliopita—karibu mara 30 kuliko fedha watumiazo kwenda sinemani,” likaripoti gazeti la habari The Globe and Mail. “Biashara ya kamari katika Kanada imesitawi zaidi kuliko ilivyo au ilivyopata kuwa katika Marekani. Biashara ya bahati nasibu imesitawi sana katika Kanada. Na ndivyo ilivyo pia, kuhusu uendeshaji farasi,” hilo gazeti likasema.

“Hakuna ajuaye ni waraibu wangapi wa uchezaji kamari walioko Afrika Kusini,” likaandika gazeti la habari la Afrika Kusini, “lakini kuna ‘maelfu’ angalau.” Hata hivyo, serikali ya Hispania inajua vema tatizo layo na idadi inayoongezeka ya wacheza-kamari. Tarakimu rasmi zaonyesha kwamba wengi wa wakazi wayo milioni 38 walicheza kamari na kupoteza dola bilioni 25 katika mwaka mmoja, ikipatia Hispania moja ya viwango vya juu zaidi vya kucheza kamari ulimwenguni. “Wahispania ni wacheza-kamari sugu,” akasema mwanamume mmoja aliyeanzisha shirika fulani la kusaidia wacheza-kamari. “Wamekuwa hivyo sikuzote. . . Wao huchezea kamari mbio za farasi, kandanda, bahati nasibu na, bila shaka kizungushi duara, michezo ya karata, na mashine hizo mbaya sana zenye kumeza pesa.” Ni katika miaka ya majuzi tu kwamba shurutisho la kucheza kamari limetambuliwa katika Hispania kuwa dhara la kisaikolojia.

Uthibitisho unaopatikana wadokeza kwamba Italia pia imechukuliwa na hicho kichaa cha uchezaji kamari. Kiasi kikubwa mno cha fedha hakimwagwi katika bahati nasibu na michezo tu bali pia katika mashindano ya magazeti na meza za kuchezea kamari. “Uchezaji kamari umepenya maisha ya kila siku katika kila sehemu,” ikasema ripoti iliyotolewa na kikundi fulani cha utafiti kilichotegemezwa na serikali. Leo “kiwango cha kucheza kamari kimefikia vimo vilivyoonekana wakati mmoja kuwa visivyowazika,” likaandika The New York Times, “na kutoka maofisa wa Serikali hadi makasisi wa parokia kuna mashindano ya kutafuta njia za kupata faida za kifedha.”

Jinsi ilivyo kweli! Katika visa vingi kucheza kamari huathiri kila sehemu ya maisha za watu, kama makala zifuatazo zitakavyoonyesha.

[Blabu katika ukurasa wa 4]

Wakati mmoja ulikuwa utendaji wenye dhambi—sasa ni “mwokozi”

[Blabu katika ukurasa wa 5]

Ueneaji wa uchezaji kamari unaenea tufeni pote

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki