Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 11/22 uku. 27
  • Mahakama Kuu Zaidi ya Norway Yatetea Haki za Kidini

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mahakama Kuu Zaidi ya Norway Yatetea Haki za Kidini
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kupigania Uhuru wa Kuabudu
    Ufalme wa Mungu Unatawala!
  • Malezi ya Mtoto—Dini na Sheria
    Amkeni!—1997
  • Wahubiri wa Ufalme Wanapeleka Kesi Mahakamani
    Ufalme wa Mungu Unatawala!
  • Mashahidi wa Yehova Watetewa Katika Vita ya Kutunza Watoto
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 11/22 uku. 27

Mahakama Kuu Zaidi ya Norway Yatetea Haki za Kidini

NI HALI zipi zingeweza kumfanya mzazi asistahili kulea mtoto? Swali hili linajadiliwa sana katika kesi za utunzi wa ulimwenguni pote. Hali nyingi hufikiriwa, kutia ndani afya ya kila mzazi, hali za mahali pa kuishi, na uhusiano na mtoto.

Lakini vipi kuhusu dini? Je, mzazi aweza kutangazwa kuwa hastahili kwa sababu tu ya dini yake? Swali hili lilikuja kukaziwa uangalifu katika pambano la utunzi wa mtoto katika Norway lililohusisha mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Zaidi ya miaka miwili ilipita na mara tatu kesi ilisikilizwa kabla ya hilo suala kusuluhishwa katika Mahakama Kuu Zaidi ya Norway.

Ilianzia 1988. Wazazi walikuwa wametengana kabisa kufikia Machi 1989, na mama alipata utunzi wa bintio. Baba alipeleka suala hili mahakamani, akidai kwamba apaswa kupewa daraka kamili la kimzazi la kumtunza huyo msichana. Yeye alidai kwamba mama alikuwa hawezi kuandaa malezi ya kawaida, yanayofaa ya mtoto na hivyo apaswa kupewa haki za kumzuru tu. Kwa nini alidai hivyo? Huyo mwanamke alikuwa akishirikiana na Mashahidi wa Yehova.

Akiomba ule ushahidi wa “wataalamu” wa wapinga Mashahidi wa Yehova, baba alianza kusadikisha mahakama kwamba mafundisho na mtindo-maisha wa Mashahidi wa Yehova zapingana na mitazamo na kanuni zihitajiwazo katika malezi mazuri. Mahakama ya wilaya iliamua 2 kwa 1 kwamba mtoto apaswa kubaki na mama yake kwa utunzi wake wa kila siku, ikimpa baba haki za kumzuru. Baba alikata rufani katika mahakama kuu. Tena, uamuzi wa 2 kwa 1 ukatetea utunzi wa kila siku wa mama kwa mtoto. Hata hivyo, wakati huu baba alipewa haki za kumzuru kwa muda mrefu zaidi. Isitoshe, hata mahakimu walioamua kwa kupendelea mama walionekana kuwa na mashaka kuhusu wakati ujao wa huyo mtoto. Akiwa na motisha hii mpya, baba alikata rufani katika Mahakama Kuu Zaidi ya Norway.

Mara nyingine tena, baba alitaka kulaumu itikadi za Mashahidi wa Yehova. Yeye alidai kwamba, ingedhuru bintiye kukulia katika uvutano kama huo.

Hata hivyo, Mahakama Kuu Zaidi ilitazama jambo hilo kwa njia tofauti. Kwa kuunga mkono uamuzi uliotolewa mnamo Agosti 26, 1994, hakimu wa kwanza wa mahakama alitangaza hivi: “Ushirika wa mama na Mashahidi wa Yehova si kizuizi cha kumpa daraka la kumtunza mtoto kila siku.” Pia alisema: “Naona kwamba mtoto anaendelea vizuri na ni msichana mwenye furaha. Yeye aonekana akiishughulikia vizuri matatizo ambayo ni lazima yatokee kwa sababu babaye na mamaye wana mtazamo tofauti sana wa maisha.” Bila kupingwa mkataa wake uliungwa mkono na mahakimu wale wengine wanne.

Wapenda kweli katika Norway wathamini kwamba mahakimu wa Mahakama Kuu Zaidi walitambua shutuma za uwongo zilizotolewa dhidi ya Mashahidi wa Yehova. Kwa uamuzi huu mahakama ilihakikisha uhuru wa kila mtu wa kuabudu Mungu na kuwapa watoto wake malezi mazuri yanayohimizwa na kanuni za Biblia.a

[Maelezo ya Chini]

a Kesi kama hizo zimeripotiwa katika matoleo ya Amkeni! ya Aprili 8, 1990, ukurasa 31, (Kiingereza), na Oktoba 8, 1993, ukurasa 15.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki