Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 12/8 kur. 8-10
  • Kile Ambacho Wakati Ujao Unacho Hasa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kile Ambacho Wakati Ujao Unacho Hasa
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Zakosa Kutimia
  • Je, Ni Kudhibiti Anga za Nje?
  • Wakati Ujao wa Familia ya Kibinadamu
  • Uvumbuzi wa Kweli wa Kisayansi
  • Kutazama Ubuni wa Sayansi wa Leo
    Amkeni!—1995
  • Ubuni wa Sayansi—Kuzuka Kwao Kufikia Umaarufu
    Amkeni!—1995
  • Imani na Wakati Ujao Wako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Chanzo Kisicho na Kifani cha Hekima Bora
    Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai?
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 12/8 kur. 8-10

Kile Ambacho Wakati Ujao Unacho Hasa

MASHABIKI wengi wa ubuni wa sayansi wana akili yenye kudadisi, tamaa ya badiliko katika jamii ya kibinadamu, na upendezi mwingi katika wakati ujao. Biblia ina mengi ya kusema kuhusu wakati ujao, lakini maoni ya Biblia kuhusu wakati ujao wa mwanadamu hayalinganiki na ukisiaji wa waandikaji wa ubuni wa sayansi.

Ubuni wa sayansi hutoa, fasiri nyingi sana za vile wakati ujao huenda ukafanana. Lakini je, ungehatarisha uhai wako kwa ajili ya moja ya hizi? Ungetegemeza uchaguzi wako juu ya nini? Mandhari hizi, au taratibu zilizoratibiwa za matukio, zote haziwezi kuwa kweli. Kwa hakika, kwa kuwa zote huhusisha makisio—ubuni—je, waweza kusema kwa uhakika kwamba hata moja yazo ni kweli? Kuna uwezekano mkubwa kwamba hakuna moja yazo ambayo ni kweli.

Zakosa Kutimia

Tayari, nyingi za mandhari za ubuni wa sayansi zakosa kutimia. Kwa njia gani? Kwa vile mandhari ambazo hushughulika na jinsi sayansi ingeweza kuongoza kwenye ustaarabu bora zaidi hapa duniani hazijatimia. Mbali na ustaarabu ulioboreka, uhalisi wa hali ulivyo leo ni kinyume. Mwandikaji Mjerumani Karl Michael Armer aonelea hivi: “Wakati ujao umetushinda sisi.” Yeye aelekeza kwenye “tisho la tufeni la kifo kisababishwacho na mabomu ya atomu, misiba ya kimazingira, njaa, umaskini, matatizo ya kawi, [na] uharamia unaoungwa mkono na serikali.”

Kwa maneno mengine, wakati ujao wa dunia na wa familia ya kibinadamu uliofafanuliwa katika masimulizi mengi ya ubuni wa sayansi hauelekei kutimizwa. Kwa kinyume, kadiri hali zinavyoendelea kuzorota duniani, ndivyo hali ya binadamu inavyoelekea upande kinyume. Licha ya maendeleo yoyote ya kisayansi au kiufundi, jamii ya kibinadamu ulimwenguni pote inapatwa na uhalifu, jeuri, umaskini, chuki ya kikabila, na mvunjiko wa familia wenye kuongezeka mno.

Baadhi ya jitihada za kisayansi zimezidisha masaibu ya mwanadamu. Ebu fikiria vielelezo vichache tu: uchafuzi wa kikemikali wa hewa, maji, na chakula chetu; ule msiba wa Bhopal katika India, ambapo aksidenti katika kiwanda iliachilia gesi yenye sumu, ikisababisha vifo vya watu 2,000 na kujeruhi watu wapatao 200,000; uyeyukaji wa kiwanda cha nguvu za nyukilia kwenye Chernobyl katika Ukrainia, ukitokeza vifo vingi na ongezeko la kansa na matatizo mengine ya kiafya katika maeneo makubwa mno.

Je, Ni Kudhibiti Anga za Nje?

Idadi kubwa ya masimulizi ya ubuni wa sayansi kuhusu wakati ujao hutoa kitulizo kwa njia nyingine pia cha taabu za maisha na kushindwa kwa miradi ya kibinadamu duniani. Wao huhamisha mashabiki hadi kwenye mandhari za kuwazia katika anga za nje. Binadamu wanaotumia vyombo vya anga vyenye kuvuka magalaksi ili kuzidhibiti sayari nyinginezo na sehemu nyingine za ulimwengu wote mzima ni vichwa vya kawaida. Mambo kama hayo hufanya wengi kuhisi kama mtu aliyeandikia mhariri wa gazeti habari la New York alivyohisi: “Tumaini la wakati ujao la wanadamu lategemea uvumbuzi wa anga.”

Ni kweli, kusafiri angani kwaendelea kwa miruko ya vyombo vya angani karibu na dunia na kwa kuanzisha vifaa vya kupekua anga. Lakini vipi kuhusu kuishi katika anga za nje? Ingawa kuna mipango kuhusu vyombo vya angani kuruka mbali zaidi angani vikielekezwa na wanadamu, kwa sasa hakuna mipango hususa ya kudhibiti mwezi au sayari yoyote iliyo karibu—uwezekano ukiwa mdogo zaidi kuwapeleka mpaka magalaksi mengineyo. Kwa kweli kudhibitiwa kwa anga za nje kupitia jitihada za wanadamu si jambo halisi katika wakati wa usoni. Na programu za sasa za angani za mataifa mbalimbali hugharimu mno hivi kwamba zapunguzwa au kutupiliwa mbali.

Uhalisi ni kwamba wakati ujao wa jamii ya kibinadamu, wakati ujao wako, hauko katika safari za kujasiria za angani zinazodhaminiwa na wanadamu. Wakati wako ujao uko papa hapa duniani. Na wakati ujao huo hautaamuliwa na wanasayansi, serikali za kibinadamu, au waandikaji wa maigizo. Kwa nini tunaweza kuwa na uhakika hivyo?

Kwa sababu wakati ujao utaamuliwa na Muumba wa dunia, Yehova Mungu. Na hakuna mandhari ya ubuni wa sayansi ambayo inaweza kulinganishwa na ahadi zinazotolewa katika Biblia. Katika kitabu hicho—Neno la Mungu lililopuliziwa—ambacho amekiwasilisha kwa wanadamu, yeye atueleza vile wakati ujao utakuwa kwa binadamu. (2 Timotheo 3:16, 17; 2 Petro 1:20, 21) Hicho husema nini?

Wakati Ujao wa Familia ya Kibinadamu

Neno la Mungu huonyesha waziwazi kusudi la Muumba la kufanya marekebisho kamili kwa kutumia serikali mpya mikononi mwa Yesu Kristo. Katika Biblia serikali hiyo ya kimbingu huitwa Ufalme wa Mungu.—Mathayo 6:9, 10.

Kuhusu Ufalme huo unabii uliopuliziwa wa Danieli 2:44 hutangaza hivi: “Katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote [zilizopo leo] vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.”

Chini ya upulizio wa kani ya utendaji yenye nguvu ya Mungu, mtume Petro pia aliandika kuhusu maisha ya wakati ujao duniani chini ya Ufalme wa Mungu. Yeye alisema hivi: “Kama ilivyo ahadi yake [ya Mungu], mnatazamia mbingu mpya [Ufalme wa kimbingu wa Mungu] na nchi mpya [jamii mpya ya wanadamu chini ya Ufalme huo], ambayo haki yakaa ndani yake.”—2 Petro 3:13.

Maisha yatafananaje kwa wale ambao watapata pendeleo la kuishi duniani chini ya utawala wa Ufalme wa Mungu wa kimbingu? Ahadi ya Muumba ni: “[Mungu] atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.”—Ufunuo 21:4, 5.

Aina ya wakati ujao ambayo Muumba huahidi ni nzuri mno. Ni tofauti kabisa na mandhari zozote za kiubuni za waandikaji wa ubuni wa sayansi au wanasayansi ambazo mara nyingi huonyesha viumbe na mazingira yasiyo ya kawaida na ya kifantasia. Wakristo wa kweli huweka imani katika ahadi za Mungu ambazo ni hakika kuhusu wakati ujao. Kwa kweli, wao hufanya hata zaidi. Wao wako tayari kuhatarisha uhai wao kwa ajili yazo.

Wanaweza kufanyaje hivyo wakiwa na uhakika kama huo? Kwa sababu wanajua kutokana na Neno la Mungu kwamba “tumaini halitahayarishi,” kwa kuwa ‘Mungu hawezi kusema uwongo.’ Kwa hakika ‘Haiwezekani Mungu kusema uwongo.’ (Warumi 5:5; Tito 1:2; Waebrania 6:18) Kama vile Yoshua, mtumishi wa Mungu, alivyotaarifu zamani za kale: “Halikuwapungukia ninyi hata neno moja katika mambo hayo mema yote aliyoyanena BWANA, Mungu wenu, katika habari zenu, yote yametimia kwenu hapana neno lo lote mlilopungukiwa.”—Yoshua 23:14.

Mwingi wa ubuni wa sayansi huonyesha maoni ya mfumo huu mwovu wa kale. Jinsi gani? Ubuni wa sayansi ulianza katika kile kilichoitwa eti kipindi cha werevuko, wakati ambapo watu wengi walikataa mamlaka za kidesturi na waliamini kwamba mwanadamu angeweza kujipangia wakati ujao wake. Moja kwa moja na kwa haki walilaumu dini za ulimwengu kwa nyingi za taabu za jamii, kisha wakakataa ukweli kuhusu kuwapo kwa Mungu na kusudi lake pia. Waliudhiwa na jinsi mambo yanavyofanyika na hivyo basi wakatafuta maoni mengineyo.

Hata hivyo, maoni ya kibinadamu, hata yawe yamefikiriwa vizuri kadiri gani, ni yenye mipaka. Muumba wetu asema hivi: “Kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.”—Isaya 55:9.

Uvumbuzi wa Kweli wa Kisayansi

Katika ulimwengu mpya wa Mungu, kiu ya kiasili ya wanadamu kuelekea ujuzi kwa sehemu itaridhishwa na uchunguzi wa kweli wa kisayansi. Hakutakuwa na uhitaji wa kubuni mandhari, kwani uhalisi utanasa na kuelimisha akili katika njia inayofaa na ya kweli.

Wakati huo wengi watafahamu jinsi mwanasayansi anayejulikana sana Isaac Newton alivyohisi alipojifananisha na “mvulana achezaye kwenye ufuo wa bahari, . . . huku bahari ya ukweli ambayo haijavumbuliwa ikiwa imetanda mbele [yake].” Bila shaka, katika ulimwengu mpya wa Mungu, Yeye ataelekeza wanadamu waaminifu kwenye uvumbuzi wenye kusisimua mmoja baada ya mwingine.

Naam, utafiti wa kisayansi wakati huo utategemea kabisa kweli, kwani Yehova ni “Mungu wa kweli.” Yeye atukaribisha kujifunza kutokana na mazingira ya mwanadamu ya kidunia na pia ulimwengu wa wanyama. (Zaburi 31:5; Ayubu 12:7-9) Jitihada ya kisayansi ya moyo mweupe yenye kuongozwa na Mungu wa kweli kwa hakika itakuwa sehemu yenye kusisimua ya mfumo mpya wa Mungu. Kisha sifa kwa ajili ya ubuni, uvumbuzi, na maendeleo yote ya ajabu katika maisha mapya ya mwanadamu na viwango vya kuishi itapewa, si binadamu yeyote, bali Muumba wa ulimwengu wote mzima, Yehova Mungu.

Katika ulimwengu huo mpya unaokuja kwa kasi mno, binadamu wote wenye kutii watamtukuza Mungu kwa utunzi na mwongozo wake wenye upendo. Watamtumikia kwa shangwe kubwa na kusema kwake, kama inavyofafanuliwa kwenye Ufunuo 4:11: “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.”

[Picha katika ukurasa wa 9]

Wakati ujao wa wanadamu uko duniani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki