Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 2/8 uku. 15
  • Robini Mwenye Urafiki

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Robini Mwenye Urafiki
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Je, Mungu Ataendelea Kuwa Rafiki Yangu?
    Amkeni!—1997
  • Sababu Hatukutoa Mimba
    Amkeni!—2009
  • 8 Kielelezo
    Amkeni!—2018
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 2/8 uku. 15

Robini Mwenye Urafiki

NA MLETA-HABARI ZA AMKENI! KATIKA UINGEREZA

MUDA mrefu kabla ya rangi za hudhurungi kubadili misitu yetu ya Northumberland kuwa yenye uzuri wa wakati wa vuli, robini hufanya kuwapo kwake kujulikane. Kifua chake chekundu na sauti tamu ya nyimbo nyororo zake huongeza upendezi na shangwe kwenye bustani yetu. Yeye ni kiumbe mwenye kufurahisha kama nini!

Robini hutambuliwa kwa wepesi kwa mabega yake na kichwa chake vyenye rangi ya zeituni-hudhurungi; kifua chake, koo, na kipaji cha uso vikiwa na rangi ya machungwa; na tumbo lenye rangi nyeupe-nyeupe. Ndege huyu aliye mnene kiasi, aliye chonjo nyakati zote, husimama wima kwa uchangamfu, akiwa sentimeta 14 kuanzia mwisho hadi kwenye mkia. Bila kushangaza, katika 1961 robini alichaguliwa kuwa ndege wa taifa wa Uingereza.

Robini wa Uingereza ni mdogo kuliko mwenzake wa Marekani, ambaye wakoloni wa mapema kutoka Uingereza walimpatia jina robini, jina walifahamulo. Hata hivyo, robini wa Uingereza ana tabia yake ya kipekee.

Vuli ikaribiapo, robini huonekana katika hali yake nzuri zaidi katika bustani ya Uingereza. Yeye husimama karibu na mtu anayelima mchanga na kuangalia nyungunyungu atokezee. Wakati mwingine, mtunza-bustani apumzikapo, robini atatulia juu ya sepeto akichungua mahali hapo. Ndege huyu shupavu hata amejulikana kwa kufuata mburuzo wa fuko ili kupeleleza vichuguu vipya vilivyochimbwa. Mlo wa robini ni wa aina mbalimbali—wadudu, mbegu, na beri, pamoja na nyungunyungu.

Hufurahisha kama nini kupata kiota cha robini! Mlango au dirisha lolote lililo wazi ni mwaliko kwa wenzi wenye kujamiiana. Viota vyaweza kujengwa haraka katika nyungu za maua za zamani au birika zilizotupwa, waya zilizopindana, au hata kwenye mifuko ya koti la kufanyia kazi kwenye bustani! Umahiri wa robini wa kutafuta mahali pasipo pa kawaida pa kujenga kiota ni mkubwa mno.

Robini ni mojawapo ndege walio rahisi zaidi kuzoeza kuwalisha mkononi mwako. Kipupwe kinapokaribia na ugavi wake wa asili wa chakula kupungua, weka chakula kwenye kiganja chako kilicho wazi—vipande vya jibini au nyungunyungu—na kingine kwenye kifaa kisichoondoleka kilicho karibu na hapo. Baada ya kula mara mbili au tatu wakati ambapo robini hula ugavi wa chakula ulio kwenye kifaa kisichoondoleka, atapata ujasiri na kutwaa vingine kutoka mkono wako ulionyooshwa. Ijapokuwa huenda asitue kwenye vidole vyako, kuanzia hapo na kuendelea robini atakuona kuwa rafiki yake sikuzote. Hatakuwa amekusahau arudipo tena majira yafuatayo—kama tu vile wewe hutakuwa umemsahau rafiki yako, robini!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki