Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 5/22 uku. 24
  • Je, umepata kuona mmweko wa kijani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, umepata kuona mmweko wa kijani?
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Anga Ni Buluu?
    Amkeni!—1991
  • Angahewa Letu Lenye Thamani
    Amkeni!—1994
  • “Utukufu” wa Nyota
    Amkeni!—2012
Amkeni!—1996
g96 5/22 uku. 24

Je, umepata kuona mmweko wa kijani?

INAFURAHISHA kama nini kuaga siku nyingine kwa kutazama machweo yenye kuvutia! Mng’ao mwekundu wa jua huandaa tamasha ya rangi wakati nuru inapopenya angahewa la dunia. Lenye kukazia tukio hili lenye kusisimua ni jambo lisilo la kawaida liitwalo mmweko wa kijani. Ikiwa hali zafaa, mmweko huu wa nuru emeraldi hutukia kwenye dakika ya mwisho ya machweo. Tukio nadra sana liitwalo mmweko wa buluu husemekana kuwa lenye kuvutia hata zaidi.

Ni nini husababisha mimweko hii yenye rangi? Kwa nini hiyo hudumu kwa dakika tu? Na kwa nini hiyo ni nadra sana? Ili kujibu maswali haya, lazima kwanza tuwe na uelewevu wa msingi wa utendeano kati ya nuru ya jua na angahewa la dunia.

Nuru ya jua inayoshuka duniani ina rangi zote za upinde-mvua. Nuru hii inapopenya angahewa la dunia, angahewa hutenda kama mche mkubwa sana nalo hutawanya, au kueneza hiyo nuru. Hata hivyo kadiri ambavyo wimbi la nuru huenezwa, hutegemea lukoka yayo.

Mawimbi ya nuru ya buluu yana lukoka fupi zaidi na yametawanywa mbali zaidi kotekote katika angahewa. Hiyo ndiyo sababu anga huonekana kuwa buluu wakati jua lipo juu kabisa ya upeo-macho katika siku isiyo na mawingu. Lakini wakati jua lipo karibu na upeo-macho—kama vile wakati wa machweo—ni lazima nuru ya jua ipite sehemu kubwa zaidi ya angahewa ili kufikia macho yetu. Likiwa tokeo, nuru ya buluu yenye kuenezwa sana haitufikii. Kwa upande ule mwingine, mawimbi marefu, kama vile yale mekundu, yaweza kwa urahisi zaidi kupenya angahewa nzito. Hili hupatia machweo rangi nyekundu au ya machungwa ifahamikayo sana.a

Ingawa hivyo, chini ya hali fulani, mmweko wa kijani au wa buluu waweza kuonekana wakati wa machweo. Hili hutukiaje? Sehemu ya mwisho ya jua inapotokomea, nuru ya jua hupasuka kuwa spektra kama upinde-mvua. Nuru nyekundu huonekana kwenye sehemu ya chini ya spektra, nayo nuru ya buluu kwenye sehemu ya juu. Jua liendeleapo kushuka, nuru nyekundu ya spektra huanguka chini ya upeo-macho nayo sehemu ya buluu kwa kawaida hutawanywa na angahewa. Ni wakati huu ambapo sehemu ya mwisho ya nuru ionekanayo iwezapo kumweka rangi ya kijani. Lakini kwa nini rangi ya kijani? Kwa sababu rangi ya kijani ndiyo rangi ile nyingine ya msingi katika nuru.

Anga linapochafuliwa sana, mmweko wa kijani huonekana mara chache sana, nao mmweko wa buluu hutukia tu wakati ambapo angahewa limetakata sana na nuru ya kutosha ya buluu kupenya anga ili kusababisha mmweko wenye kung’aa kuonekana.

[Maelezo ya Chini]

a Ona Amkeni!, Desemba 8, 1987, ukurasa 16 (la Kiingereza), kwa habari zaidi juu ya machweo.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24]

Machweo: ©Pekka Parviainen/SPL/Photo Researchers

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki