Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 6/22 kur. 8-10
  • Furahia Likizo Bila Majuto!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Furahia Likizo Bila Majuto!
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Uwe na Usawaziko
  • Kudumisha Mahusiano Mema
  • Ni Nini Kinachopendekezwa Likizoni?
  • Fanya Likizo Iwe Wakati Wenye Kuthawabisha
  • Je, Uko Tayari kwa Ajili ya Likizo?
    Amkeni!—1996
  • Jinsi Uwezavyo Kuepuka Matatizo ya Likizo
    Amkeni!—1998
  • Kile Upaswacho Kulinda Dhidi Yacho
    Amkeni!—1996
  • Twaa Fursa Utoe Ushahidi Wakati wa Desemba
    Huduma Yetu ya Ufalme—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 6/22 kur. 8-10

Furahia Likizo Bila Majuto!

ALIPOULIZWA jinsi alivyofurahia ziara yake ya kwanza kwenye sehemu ya likizo ijulikanayo sana, Mmarekani mmoja ambaye sasa anaishi Ulaya, alijibu hivi: “Ni lazima pawe palikuwa pazuri sana kabla ya watu kuja.” Je, umepata kuwa na hisia kama hizo? Si kila mtu hufurahia mahali pa likizo palipo na mahoteli na majumba ya dansi yaliyo katika sehemu moja, ufuo uliochafuliwa na uliosongamana, na redio zenye kelele nyingi mno.

Kwa kusikitisha, si sikuzote ambapo likizo hutimiza matarajio yetu. Badala ya kutupatia nishati mpya hizo hutufanya tuhitaji pumziko zaidi. Hivyo swali hili lafaa, Twaweza kufurahiaje likizo bila majuto?

Uwe na Usawaziko

Sawa na vikolezo katika chakula chetu, likizo huwa na mafanikio bora zaidi zinapotumiwa kwa uchache. Ingawa maisha ya tajiri asafiriye kwa ukawaida hasa kwa ajili ya anasa huenda yakavutia, hayo hukosa usawaziko na hayatokezi furaha ya kweli.

Hasa kuhusiana na likizo, usawaziko katika kutumia fedha ni wa muhimu sana. Panga kwa uangalifu kabla ya kwenda, na ujaribu kufanya matumizi kulingana na bajeti yako. Epuka kudanganywa na matoleo ya pekee yafanywayo na maajenti wa usafiri ambao hukutia moyo “furahia sasa, lipa baadaye.”

Pia, usijawe kupita kiasi na hisia za hatari ziwezazo kutokea hivi kwamba hali ya uhuru na starehe ambayo hufanya likizo zivutie ikandamizwe. Kwa kuongezea, usawaziko ufaao hutia ndani kutambua hatari kubwa zaidi ambayo yaweza kutufanya tutazame nyuma kwa likizo yetu tukiwa na majuto. Haihusiani kwa vyovyote na aksidenti, ugonjwa, au uhalifu, bali na mahusiano ya kibinafsi.

Kudumisha Mahusiano Mema

Likizo pamoja na familia au marafiki zaweza kuimarisha vifungo vya upendo. Kwa upande ule mwingine, likizo zaweza kusababisha mvunjiko katika uhusiano uwezao kuwa vigumu sana kurekebisha baadaye. Mwandikaji wa habari Lance Morrow alisema hivi: “Hatari halisi ya likizo iko katika uwezo wayo wa kufanya kutoafikiana katika familia kuwe dhahiri zaidi. . . . Watu katika maisha yao ya kawaida wana kazi, madaraka, marafiki na taratibu ambazo hueneza na kufyonza hisia-moyo. Katika mazingira ya nyumba inayotumiwa kwa ajili ya likizo, masuala ya familia yaliyokandamizwa kwa miaka 20 yaweza kuzuka kama mlipuko.”

Kwa hiyo kabla ya kwenda likizoni, azimieni kikweli kuifanya iwe pindi yenye kufurahisha. Kumbukeni kwamba mapendezi hutofautiana. Huenda watoto wakawa wanatafuta utendaji wenye kujasiria, wazazi huenda wanatafuta pumziko. Uwe tayari kuacha mapendezi ya kibinafsi ya jambo la kufanya au mahali pa kwenda. Ikiwa ni jambo la hekima na la kiakili, afikianeni kuruhusu kila mtu kwa kipindi fulani afuatie kile ambacho kinampendeza hasa. Jifunzeni kudhihirisha sifa za roho ya Mungu kila siku katika mwaka wote, kisha haitakuwa vigumu kuendelea kufanya hivyo wakati wa likizo yenu.—Wagalatia 5:22, 23.

Ingawa kudumisha uhusiano mzuri pamoja na familia na marafiki ni jambo la maana, uhusiano wetu pamoja na Mungu ni wa maana hata zaidi. Tukiwa likizoni mara nyingi sisi hukutana na watu ambao hawashiriki maoni yetu ya Kikristo juu ya Mungu na matakwa yake. Kushirikiana karibu nao—labda hata kwenda mara kwa mara mahali penye vitumbuizo vyenye kutilika shaka—kwaweza kutuongoza kwenye matokeo yenye kuleta majuto. Kumbuka Biblia huonya: “Msiongozwe vibaya. Mashirika mabaya huharibu mazoea yenye mafaa.”—1 Wakorintho 15:33, NW.

Unapokuwa likizoni, wakati wowote ukigundua ndani yako mwenyewe tamaa ya kutoroka viwango na mazoea ya Kikristo, kwa hekima kabili udhaifu huo bila woga ukiomba msaada wa kimungu ili kupambana na tamaa hiyo!

Ni Nini Kinachopendekezwa Likizoni?

Watu wasiofinyanga maisha zao kulingana na kanuni za Kikristo huenda wakahisi kwamba wanapokuwa likizoni mwenendo wowote unakubaliwa. Katika nchi fulani za Ulaya, utalii wa ngono ni biashara yenye faida kubwa, na baadhi ya maajenti wa usafiri huipendekeza. Gazeti The European laandika kwamba ‘mambo yenye kuchukiza ambayo wanaume wa Ulaya hufanya katika makao fulani ya waenda-likizo ya Asia yamejulikana kwa muda mrefu.’ Likirejezea kwa nchi moja ya Asia, gazeti la Ujerumani Der Spiegel lilikadiria kwamba kufikia asilimia 70 ya wageni wote wanaume ni “watalii wa ngono.”

Watalii wanawake sasa wanafuata kielelezo cha wenzao wa kiume. Kampuni ya Ujerumani ya ndege za kukodiwa ambayo husafiri hasa safari za kwenda Karibea hukadiria kwamba asilimia 30 ya abiria wayo wa kike huenda huko likizoni kwa kusudi dhahiri la ngono haramu. Gazeti The European lilimnukuu mwandikaji habari Mjerumani akisema: “Wanaiona kuwa njia rahisi na isiyo tata ya kupata raha—mchezo wa kigeni.”

Hata hivyo, Wakristo wa kweli hawaioni ngono haramu kuwa njia inayokubalika ya kupata raha. Hiyo huvunja kanuni za Kikristo na imejawa na hatari. Ingawa hatari hutambuliwa kwa kawaida, watu wengi hujaribu tu kuepuka matokeo badala ya zoea hilo. Mfano mzuri ni tangazo katika magazeti ya habari ya Ujerumani lionyeshalo mwavuli na viti viwili vya ufuoni vilivyo vitupu. Maelezo husomeka hivi: “Safiri salama, na urudi bila UKIMWI.”

Tokeo baya sana la utalii wa ngono ni kutendwa vibaya kingono kwa watoto. Kwa kupendeza, katika 1993 serikali ya Ujerumani ilipitisha sheria ifanyayo Wajerumani waweze kupata adhabu wapatikanapo na hatia ya kufanya ngono na watoto—hata wakiwa likizoni katika nchi za kigeni. Hata hivyo, kufikia sasa matokeo mazuri yamekuwa ya chini sana. Umalaya wa watoto umekuwa—na wabaki ukiwa—uhalisi wenye kuumiza na kutaabisha jamii ya kibinadamu.

Fanya Likizo Iwe Wakati Wenye Kuthawabisha

Kusoma, kujifunza Biblia, na kushiriki katika huduma ya Kikristo ni utendaji wenye kufurahisha, na wenye kuthawabisha kwa Wakristo wa kweli. Lakini wengi hujikakamua kupata wakati wa kutosha kufanya mambo kwa kadiri wanayotaka. Kwaweza kuwa na wakati gani bora zaidi wa kufikia ratiba ya usomaji kuliko wakati wa likizo ambapo vizuizi vikali vinavyowekwa na saa havipo?

Ni kweli, likizo yenye shughuli nyingi na yenye kutosheleza huenda isikuruhusu ufuatie masilahi ya Kikristo kwa kiwango cha kawaida. Lakini kwa nini usijaribu kuweka kando wakati fulani angalau kwa ajili ya utendaji wa kiroho wenye kujenga? Hilo bado litaacha wakati kwa ajili ya pumziko. Kwa kweli, wengine hata hutumia kwa faida wakati ulioongezeka upatikanao wakati wa likizo ili kupanua huduma yao. Kama alivyosema Yesu, “wenye furaha ni wale wenye kuona uhitaji wao wa kiroho.”—Mathayo 5:3, NW.

Baada ya muda huenda pia wewe utaenda likizoni. Ikiwa ndivyo, hakikisha unaifurahia! Usiwe na wasiwasi mno juu ya hatari ziwezazo kutokea, lakini uwe mwangalifu. Kumbuka madokezo kama yale yapatikanayo katika kisanduku kwenye ukurasa huu. Baada ya likizo, rudi ukiwa umeburudika, umepumzika, na ukiwa na hamu ya kuendelea na utendaji wa maisha wenye umaana mkubwa zaidi. Muda si muda, likizo imekwisha, lakini baadhi ya kumbukumbu zenye kuthaminiwa zaweza kubaki milele. Jinsi zilivyo na thamani—likizo zilizofurahiwa bila majuto!

[Sanduku katika ukurasa wa 10]

Vidokezo Vichache vya Likizo

Pambana na Uhalifu

1. Panga mtu alinde vitu nyumbani.

2. Kaa mbali na maeneo yaonwayo kwa kawaida kuwa hatari.

3. Uwe chonjo kuhusu sinzia, weka fedha mahali salama mwilini mwako, na uache fedha za ziada mahali salama kule unakokaa.

4. Jihadhari na watu usiowajua watoao msaada bila kuombwa.

Epuka Aksidenti

1. Ikiwa waendesha gari, uwe chonjo, na kupumzika mara kwa mara.

2. Unapokaa hotelini au kusafiri kwa ndege, tazama kwa uangalifu vifaa kwa ajili ya wakati wa dharura.

3. Baada ya kufika ruhusu wakati ili ujirekebishe kimwili kabla ya kuingia katika utendaji wenye kujikaza.

4. Uwe na mavazi, viatu, na vifaa vifaavyo kwa ajili ya utendaji wako.

Dumisha Afya Nzuri

1. Mwombe daktari wako shauri kuhusu uhitaji wa chanjo au dawa zozote zihitajiwazo.

2. Nenda pamoja na kisanduku cha kusafiri cha dawa za muhimu.

3. Pumzika vya kutosha, na uwe mwangalifu na kile unachokula na kunywa.

4. Beba mwilini mwako nyakati zote hati za muhimu kuhusu mahitaji yako ya kitiba na matamanio yako.

Dumisha Mahusiano Yakiwa Yenye Furaha

1. Onyesha upendo na ufikirio kwa wale walio pamoja nawe.

2. Weka viwango vya ushirika wa kibinafsi vikiwa juu.

3. Usiruhusu waenda-likizo wengine wakuongoze kwenye matendo unayotilia shaka.

4. Weka kando wakati kwa ajili ya kujazilia mahitaji ya kiroho.

[Picha katika ukurasa wa 9]

Chagua utendaji wenye kujenga unapokuwa likizoni

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki