Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 6/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Kanisa la Mormon—Je, Ni Urejesho wa Mambo Yote?
    Amkeni!—1995
  • “Walitaka Nijithibitishie Ukweli”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Utafutaji wa Majibu wa Mwanamume Kijana
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 6/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Msanii Mkuu Kuliko Wote Asanteni kwa mfululizo wa makala “Kumtafuta Msanii Mkuu Kuliko Wote.” (Novemba 8, 1995) Mimi binafsi nikiwa msanii, nilithamini sana makala hizo. Unamna-namna mwingi wa uumbaji wa Mungu, sanaa ya kishairi ya Zaburi, na mafungu mengine yenye maneno matamu ya Biblia yote yaonyesha kwamba Yehova hafanyizi tu sanaa bali yeye huifurahia vilevile!

B. R., Marekani

Nikiwa nimehusika na sanaa kwa zaidi ya miaka 30, nataka kuwapongeza wale wote waliohusika katika kutayarisha makala nzuri ajabu kama hiyo! Ilikuwa kurasa tisa za ukweli na kusababu kuzuri kuhusu Mungu wetu mkuu, Yehova, na uwezo wake wenye nguvu sana wa kubuni.

P. M., Marekani

Wamormon Nilisoma makala “Kanisa la Mormon—Je, Ni Urejesho wa Mambo Yote?” kwa hamu. (Novemba 8, 1995) Nililelewa katika familia ya Wamormon nikabatizwa na kutawazwa kwa ukuhani wa Mormon kabla ya kuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Hata hivyo, kuna taarifa moja iliyonasa akili yangu. Mwasema kwamba “fasili [ya Mormon] ya dhambi ya mume na mke wa kwanza ilihusisha ngono na kuzaa watoto.” Nakumbuka tulifundishwa kwamba Adamu na Hawa walifanya dhambi kwa kula tunda halisi.

D. A., Marekani

Twaomba radhi ikiwa taarifa hiyo ilitokeza mvurugo fulani. Hatukumaanisha kwamba Wamormon wanaamini dhambi yenyewe ilikuwa ngono, ingawa mtu aweza kupata wazo hilo kutoka kwa simulizi la “Book of Mormon.” (2 Nephi 2:22, 23, 25) Badala ya hivyo, tulisema kwamba dhambi hiyo “ilihusisha” ngono. Kwa njia gani? Kwa njia ya kwamba, kulingana na theolojia ya Mormon, dhambi ilifungua njia kwa wanadamu kuzaa. Kulingana na kitabu “Mormon Doctrine,” cha Bruce R. McConkie, kabla ya kufanya dhambi, Adamu “hakuweza kupata watoto. . . . Kulingana na mpango uliofanywa kimbele, Adamu alipaswa kuangukia dhambi . . . Kwa kuwa mtu awezaye kufa, sasa angeweza kupata watoto.” Kwa kutofautisha, Biblia haifundishi kwamba Adamu alipaswa kufanya dhambi ndipo azae. (Mwanzo 1:28) Wala haisemi kwamba walianguka kwa sababu walipangiwa kimbele na Mungu. Badala ya hivyo inasema wao walianguka kwa sababu ya tamaa yao wenyewe ya kutaka uhuru. (Mhubiri 7:29) Hivyo, ingawa twastahi haki za Wamormon kuamini mambo wachaguayo, jambo hili laonyesha kwamba mafundisho ya “The Book of Mormon” hayapatani na Biblia hata kidogo.—Mhariri.

Nikiwa mtu ambaye hakujua kabisa jambo la kusema na Wamormon, naweza kusema kwamba nimearifiwa kabisa juu yao, kwa sababu ya makala hizo. Wamormon waweza kusemaje wanaamini kwamba Biblia na The Book of Mormon vyote viwili vyatoka kwa Mungu bila kuona kwamba vinapingana?

J. M., Marekani

Pornografia ya Kompyuta Nataka kuwashukuru kwa ajili habari “Pornografia ya Kompyuta Yapatikana kwa Watoto” katika “Kuutazama Ulimwengu.” (Novemba 8, 1995) Nilisoma habari hiyo nikashtuka sana! Ilionyesha kikweli jinsi programu hizo za kompyuta zilivyo hatari na jinsi ziwezavyo kufikia watoto kwa urahisi. Makala hiyo itawasaidia Wakristo wapime mafaa na mabaya yahusikayo na tekinolojia ya kompyuta.

D. P., Marekani

Ugonjwa Utokanao na Chakula Nilifurahia makala yenu “Jilinde na Ugonjwa Utokanao na chakula.” (Novemba 22, 1995) Ninafanya kazi ya mpishi mkuu na ningependa kuongeza jambo. Mtu akipenda kula nyama isiyopikwa sana, huenda haitawezekana kuepuka ugonjwa utokanao na chakula mahali ambapo kuna tatizo hilo. Ni kweli kwamba kupika nyama kwa moto mwingi huelekea kukausha nyama na huenda ukafanya iwe vigumu kuyeyushwa. Njia nzuri ya kupika nyama vizuri na kuhifadhi unyevu wayo ni kuipika kwa mchuzi au kuipika polepole ikiwa imefunikwa.

J. P. K., Marekani

Asante kwa dokezo hilo la upishi.—Mhariri.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki