Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 8/22 uku. 31
  • Ubikira—Kwa Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ubikira—Kwa Nini?
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Viapo vya Ubikira Ni Nini?
    Vijana Huuliza
  • Je, Mashahidi wa Yehova Ni Dhehebu?
    Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi Kuhusu Mashahidi wa Yehova
  • Vidhehebu—Hivyo Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Vipi kuhusu viapo vya kujiepusha na ngono?
    Amkeni!—2007
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 8/22 uku. 31

Ubikira—Kwa Nini?

“MADHEHEBU ya ubikira”—ndivyo Randall Balmer, ambaye ni profesa-mshiriki wa dini kwenye Chuo cha Barnard na Chuo Kikuu cha Columbia, anavyoita mwelekeo unaoongezeka miongoni mwa matineja wa kuepuka ngono mpaka wawe na umri mkubwa zaidi.

Si ajabu kwamba sihi nyingi za kuepuka ngono zatoka kwa matengenezo ya kidini. “Lakini madhehebu ya ubikira inachochewa na sababu za kilimwengu, si za kidini,” aeleza Dakt. Balmer. “Kichocheo chenyewe cha kubaki bikira ni hofu—si hofu ya kuadhibiwa na Mungu, bali hofu ya kupatwa na maradhi hatari.” Hivyo, yeye atofautisha “madhehebu ya Bikira Mariamu,” ambayo inaepuka ngono kwa sababu za kidini, na “madhehebu ya ubikira” ya kisasa, ambayo huepuka ngono hasa kwa sababu ya afya.

“Ni hali ya kuhuzunisha kuhusu dini katika miaka ya 1990 kwamba hofu ya maradhi inaongoza maadili,” Dakt. Balmer aendelea kusema. “Viongozi wa kidini, wakitamani sana kuepuka kuudhi, wameendeleza maadili ya kijuu-juu au hawaendelezi kamwe maadili yoyote. Na basi ni wanasayansi tu na maofisa wa afya ya umma ndio wameachiwa daraka la kuwashauri matineja jinsi ya kuongoza maisha zao za ngono.”

Lakini, hali si hivyo na Wakristo wa kweli. Fikiria Chad, tineja mmoja anayelelewa akiwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Chad alifikiwa na msichana mmoja ambaye alianza kuzungumza naye. Lakini upesi ikawa wazi kwamba alikusudia mambo mengi zaidi ya mazungumzo tu. “Ndipo nikang’amua,” asema Chad. “Nisingeweza kumvunja moyo Yehova. Nikiwazia kumpendeza Yehova sikuzote, nikamwambia msichana huyo ni lazima niondoke.”

Kama Chad, vijana wengi miongoni mwa Mashahidi wa Yehova wanadumisha maadili safi si tu kwa ajili ya kuwa na afya nzuri bali hasa ili kumpendeza Muumba wao, Yehova Mungu. Si hofu ya kupatwa na maradhi inayoongoza maadili yao. Badala ya hivyo, vijana hao hufuata shauri la Mhubiri 12:1: “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki